watanzania wenzangu wazalendo wana wa afrika mimi mtanzania halisi mwanawaafrika ,nashauri kuwa katika mchakato huo wanahabari na vyombo vya habari vipewe jukumu la kurekodi kila kitu anachochangia mtanzania popote alipo awe kisumba huko kalambo sumbawanga awe kifunda huko lufilyo rungwe mashariki awe paradiso huko mbinga ruvuma awe kilindi tanga ,manyoni singida yaani popote pale sasa picha hizo zipewe kipindi maalumu kirushwe kwenye tv zote bila upendeleo kwa kisingizio kuwa ipo tbc hapana tunataka tv zote zishiriki walipwe muda wa hewani ,radio zote kwenye mitandao ili wananchi wasikie waone kilichonenwa na watu wa bukombe ,watu wa mitumba huko gombe kigoma na kuingineko ,ili siku ya siku hawa wakina ramadhani tuwashitaki wasipotekeleza majukumu sawa na maoni ya wananchi.
Hawa mabwana wawili ndo wamechafua pilau iitwayo katiba,ni kama vile mtu una njaa halafu unaletewa chakula wakati unataka kula tonge unagundua kuwa hicho chakula mchuzi wake umechanganywa na mchuuzi wa samaki aliyevunda,ladha yote ya chakula na hamu inaisha.Tatizo huyo muandaaji wa chakula naamini kafanya makusudi ili watu tuzile kula huo mulo kwa kwa kuchanganya na mchuzi wa samaki waliovundaWajumbe hawa wawili ambao Rais amewaingiza katika tume ya kukusanya maoni, wana mushkeri. Judge Ramadhani anatuhumiwa kuhujumu kesi ya mgombea binafsi hivyo kuhujumu demokrasia na kuipa serikari ushindi wa kesi ambayo ilikuwa obvious kwa kuwa mgombea binafsi ni haki ya kimsingi ya kikatiba kwa katiba yetu hii kuukuu!
Prof Kabudi, pamoja na comments zake nyingi tata, anaonyesha pamoja na kuwa ni prof wa sheria hana msimamo, mfano pia ni kesi hiyohiyo ya mgombea binafsi, akiwa rafiki wa mahakama, alipendekeza pendekezo ambalo kwa mtu wa weredi wake, watu wasingetegemea hata kidogo, yaani alikuwa anapinga uwepo wa mgombea binafsi! Kwa kweli hawa wawili ni janga na tuwaangalie vizuri!
Kwakweli hawa wawili, na wengine ambao sijatoa wasifu wao kazi yao ni kukusanya maoni, lakini, ninakuwa na wasiwasi na kama ni kweli watakusanya maoni badala ya kishinikiza interest zao, anyway tunawajua wanasimamia msimamo gani, jamani tuweni macho na maoni yetu yasije nayo yakachakachuliwa.
Ofcourse upo sahihi mkuu, lakini kumbuka ile kamati ina wajumbe wengi ambao hawawezi kumezwa na vichwa viwili tu. Surely hukumu ile ilikuwa ya kisiasa zaidi na iliwapunguzia hadhi magwiji hawa katika taaluma ya sheria. Kumbuka marehemu Mwaikusa alikuwepo, zaidi ya hilo alibobea katika katiba na kesi ile ilikuwa ya kikatiba, unaweza kuona ni namna gani muhimili huu( mahakama ) ulivyoingiliwa na siasa. Ninadhani dawa pekee ni katiba mpya ambayo wajumbe watakaoratibu maoni wengi wao watatanguliza utaifa mbele kama tunavyowafahamu kwa uzalendo wao kwa taifa lao.
Ila nimeshangaa sana amemuacha gwiji aliyeanzisha hili vuguvugu katika midahalo profesa shivji na gwiji la habari Jenerali Ulimwengu, nimeshangaa sana kwa kuwa ndo vinara wa kwanza kabsa kulitafsiri hili suala kwa wanachi kuipitia mdahalo wa wazi pale UDSM.