Seif al Islam
JF-Expert Member
- Nov 14, 2011
- 2,156
- 640
Ni jambo ambalo wabashiri wa mambo na wafuatiliaji wa siasa za upinzani hapa Tanzania tulilibashiri mapemaaa.
Hili si jingine bali ni kudorora na baadae kufa kifo cha asili kwa kile kilichoitwa na CUF kuwa oparesheni mchakachaka hadi 2015 ikiwa na kauli mbiu ya dira ya mabadiliko yaani vision for change(V4C).
Oparesheni hii iliyoanzishwa kimamluki na bila utafiti wala dira inayoeleweka ililenga hasa kuiga(imitation) na pia kudhoofisha kile kinachoitwa movement for change(M4C) iliyoasisiwa kwa ustadi mkubwa na CHADEMA na kupata mwitikio chanya kutoka kwa wananchi.
Kuonyesha namna ambavyo ilikosa dira, oparesheni hii ilianzia huko Arusha (ngome ya CHADEMA) ambako pamoja na kukosa msisimko wowote wa maana CUF walifanya maigizo ya kuwapokea waliowaita vigogo wa CHADEMA na baada ya hapo mikutano na oparesheni zile zilififia(kama tulivyobashiri) na sasa sioni kama ntakuwa sijatenda haki kama nikisema wazi kuwa movement ile ya kimamluki imekufa kifo cha asili (natural death) cha kujifunza hapa ni kimoja tuu kuwa watanzania wamechoka maigizo ya CCM na vibaraka wao. Wanataka kuona mtu au chama kinachoonyesha mwelekeo wa kuwakomboa kwelikweli na sio kuwapotezea muda.