mchaka mchaka shule za msingi

LUBEDE

JF-Expert Member
May 7, 2013
4,320
6,683
wakuu kwa wale old schools wenzangu,hivi haya mambo ya mchaka mchaka mashuleni yalifia wapi?
kwanini walitukimbiza vile kipindi kile,hadi leo nimeshindwa kuelewa faida/hasara ya mchaka mchaka mashuleni,tusaidiane kwa faida ya kizazi hiki,wajue tulipotokea...
 
Faida Ni nyingi saana, kujenga mwili na pia kuwa mkakamavu, kukuza uzalendo kupitia nyimbo mbali mbali mfano zile za vita dhidi ya Nduli Amini.

Ilikuwa inajenga urafiki kupitia utani wakati wa kukimbia.

Siku hizi watoto hawakimbii shulen. Kuna mwalimu siku moja aliwatoa watoto wakimbie kuzunguuka madarasa kama wanne hivi walizimia mara sijui pressure..... Alitamani kuhama huyo mwalimu.

Chief Daby hii kitu ilikuwa inakera saana, paka kengele inaibiwa muda wa mchaka mchaka.....
 
Kimbungaa... ni cha niniii... jibu ni kuhamia mpakaniiii.... Mchakamchaka ulitufundisha uzalendo, heshima, kuwa wakakamavu,kupendana,kujaliana na mambo mengine kadha wa kadha
 
Mchakamchaka ulisaidia kutuweka active na attention darasani, ulichochea ukuaji wa uwezo wa misuli (mf. Endurance) na mapafu. Pia, kwenye nyimbo za mchakamchaka tulijifunza maneno mengi tu ya kiingereza, tukapata motisha ya kusoma kutimiza ndoto, tukagundua vipaji vya waimbaji wazuri shuleni, tukajenga confidence n.k

Yaani faida ni tele...

NB: Mi kwenye
mchakamchaka nyimbo ndo zilikuwa zinanipa raha..
 
Mchaka mchaka na kuwah namba asubuh duuh ni vitu nilikuwa navichukia kabisa shule
 
Yaaaan!!! Aiseee machaka
Mchaka raha sana hasa
Kipind cha bard kama
Hiki masika dhaaaa

Nakumbuka mbali kichz

Embu tulio maliza
Kwalamahondo

Piten hapa
 
Back
Top Bottom