Mc Mdachi awaangusha Maharusi katika Swimming pool

Jana kila nilipokua naangalia Swimming pool ile KICHEKO KILIKUWA HAKINIISHI... Na baada ya Muhudumu aliyekuwepo kunitajia kuwa General huyo ni Gaho ilibidi nikachekee chooni... LOL...
 
Ngoja niwaambieni yale ninayoyajua. Hiyo ilikuwa ni send off ya binti wa Meja General mstaafu ambaye kwao ni Tanga lakini hivi sasa ni mfanya biashara akimiliki kiwanda cha kushona nguo kule mwenge. Pia ni board member wa First Middle East Bank iliyopo Dar. Huyo siku za nyuma aliwahi kuwa mwambata wa jeshi huko Misri. Ni mzee mmoja ambaye ana nyodo sana na kupenda kuonekana na kusifiwa sifiwa. Alitaka send off hiyo iwe ya kipekee na kwa kweli palipambwa haswa.

Awali alietakiwa kuwa MC hakuwa Mdachi bali alikuwa dada mmoja naye maarufu sana. Dada mmoja wa Kitanga. Siku chache kabla ya siku ya shughuli kufika mawasiliano kati ya Meja General na huyo dada yakapotea. Basi General kumbe alikuwa kakerwa akaamua kumchukua MDachi ambaye pia ni mgosi wa kaya. Yule dada hana habari. Ikawa siku ya shughuli ilipofika yule dada kapeleka vyombo vyake na DJ wake pale city garden (zamani Gerezani Club). Jioni anafika kwenye ukumbi kamkuta Mdachi yuko kazini. Yule dada kuepuka aibu na shari kaondoka kimya kimya kaacha vyombo vyake na Dj wake wanatumiwa na Mdachi.

Sasa yule mjeshi kutokana na uzoefu wake wa kujenga madaraja wakati wa vita akabuni daraja ambalo lilikuwa linapita juu ya hiyo swimming pool. Kumbe hakufanya mahesabu ya kujua ni kiasi gani cha watu wangehimili kusimama juu ya lile daraja. Miongoni mwa waalikwa walikuwemo wahandisi. Wakawa wanajiuliza na kunongona kuwa jamani hili daraja litaweza kubeba watu wote wale.

Nirudi kwa dada MC. Yule dada ni mlokole wa kufanya maombi sana. Akiwa nyumbani kwake akamlilia sana Mola wake. Matokeo ndiyo hicho kituko cha kufungia mwaka cha maharusi na General mwenyewe kutumbukia kwenye pool. Simu zao mahela yao, ATM Cards zao zote zililowa. Hayo yaliyoandikwa kwenye gazeti si uwongo ni ukweli mtupu.

Kuchamba kwingi kushika mavi. Jamani wa kulaumiwa siyo kamati ya maandalizi wala si Mdachi bali ni General mwenyewe.
Naona kama wewe ndio mdada mwenyewe,maana ulovyoipigia mbizi hii mada, unanipa mashaka.
 
Back
Top Bottom