MC afariki akifanya mapenzi na mke wa mtu

Date: 1/5/2010
Daniel Mjema,Moshi

MSHEREHESHAJI maarufu katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, Willy Lema alifariki akiwa anafanya mapenzi na mwanamke ambaye ni mke wa mkazi mmoja wa Nzega mkoani Tabora, Mwananchi imebaini.

Lema, ambaye alifariki akiwa kwenye chumba cha Hoteli ya Newcastle mjini Moshi, ana mke mwenye watoto na familia yao inaishi jijini Arusha.

Uchunguzi wa Mwananchi wa tukio hilo ambalo limekuwa gumzo katika miji hii miwili, umebaini kuwa mwanamke huyo anashikiliwa na polisi kwa mahojiano baada ya tukio hilo.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinadai kuwa marehemu na mwanamke huyo walikuwa na mahusiano ya kimapenzi ya siri tangu mwaka 2001.

Vyanzo mbalimbali vilivyomkariri mwanamke huyo akitoa maelezo polisi, vimedai kuwa baada ya kufanya awamu ya kwanza ya tendo la ndoa, Lema alimuomba mwanamke huyo wafanye tendo hilo kwa staili nyingine, jambo ambalo alilitekeleza.

Baada ya marehemu kufanya tendo hilo kwa staili na kumaliza aliishiwa nguvu, amedokeza mpashaji wa Mwananchi ambaye pia alieleza kuwa kabla ya kufika hotelini, mshereheshaji huyo alichanganya pombe kali ili kupata nguvu ya kufanya tendo hilo.

Baadhi ya marafiki waliokuwa na marehemu kabla hajaelekea kwenye eneo la tukio na ambao wameomba majina yao yahifadhiwe, walidokeza kuwa marehemu alikuwa akinywa, bia lakini alipokaribia kuondoka alichanganya kwa wingi na pombe kali aina ya Konyagi.

Inadaiwa marehemu pamoja na mwanamke huyo wote ni wenyeji wa Machame wilayani Hai na walikuwa wamekuja mkoani Kilimanjaro kwa mapumziko ya mwisho ya mwaka ambao ni utamaduni uliozoeleka kwa wenyeji wa hapa.

Habari hizo zinadai kuwa baada ya marehemu kufanya tendo la ndoa kwa awamu ya pili na kuishiwa nguvu alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC ambako baada ya wauguzi kumpima waligundua alishafariki kitambo.

Inadaiwa kuwa baada ya kuarifiwa hivyo, mwanamke huyo alitaka kutimua mbio lakini yeye pamoja na dereva wa taxi waliompeleka MC huyo KCMC walizuiwa hadi polisi walipoitwa na kuwachukua kwa mahojiano.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Nghoboko alisema polisi hawawezi kuingilia starehe za watu bali walichokuwa wakichunguza ni kama marehemu alinyongwa shingo au la lakini wamegundua hilo halikuwepo.

Hayo mambo mengine ni faragha za watu... sisi tulichokuwa tunachunguza ni kama alinyongwa au vipi hayo mengine kwa kweli hatuhusiki nayo na hakuna dalili zozote za kunyongwa, alisema Kamanda Nghoboko.

Watalaamu wa afya wanahisi kuwa huenda marehemu alikunywa vidonge vya kuongeza nguvu (viagra) ambavyo pamoja na pombe nyingine alizokunywa zilisababisha kiwango cha sukari kushuka hadi chini kabisa.

Mwili wa marehemu ambao umehifadhiwa KCMC mjini Moshi kwa uchunguzi zaidi, utazikwa kesho kijijini kwake Machame.
Uzinzi haujawahi kumwacha mzinzi salama! Mwamba anateketea kwa moto mwaka wa 13 sasa!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom