Mbwiga sio mtangazaji by proffesional na hata pale Clouds kwenye kipindi cha Sports Extra siku zote alikua kama mualikwa kwa ajili ya kutoa visa vya vya wachezaji wa zamani ambavyo hakina aliviishi. anakumbukumbu navyo na anakipaji kikubwa sana cha kuviwasilisha katika lugha ya kuchekesha na kuburudisha
Tukumbuke kua jamaa huyu katuletea misamiati mingi kwenye soka. Kampa kampa tena, udambwi dambwi, figisufigisu, mbavu ya kulia na kushoto, kiungo muongo muongo, na mengine mengi ni maneno yanayotumika hadi sasa na kayaibua Mbwiga
Kipaji chake cha kuongea na urafiki wake na Jose ulimpa fursa(na sio ajira kamili) ya kujulikana katika ulimwengu wa soka hapa nchini huku akipata posho kwa kuonyesha kipaji chake na hata kusafiri sana ndani na nje ya nchi bila kujali anakiwango gani cha elimu
Nadhani ni vema marafiki zake wanaomtakia mema wamshauri huko alipoenda kwamba ajikite kwenye majukumu yake aliyopewa hapo na aachane kabisa na kuponda kule alipotoka bila kujali sababu yoyote ile iwayo iliyomfanya atoke Clouds hata kama anahisi alionewa, maana kuna leo na kesho