Kama ambavyo tweet inavyoonesha hapo juu, Mbwana Ali Samatta amerudi nchini Ubeligiji, na safari hii akijiunga na klabu kongwe nchini humo, yaani Royal Antwerp! Kwa wafuatiliaji, bila shaka wanafahamu Samatta hakuwa akipata nafasi ya kutosha pale Fenerbahce. Jambo lililonishangaza, inaonekana mashabiki wa Fenerbahce bado walikuwa na imani zaidi na Samatta, lakini Benchi laUfundi likamuona hatoshi!
Kwa mujibu wa Gazeti la Hurriyet la nchini Uturuki, Samatta ameenda Royal Antwerp kwa mkopo wa mwaka mmoja, huku kukiwa na kipengele cha kukiwa na option ya kumnunua kwa $4.72 Million, takribani Sh 11 Bilion za Tanzania.
Ukiangalia kwenye msimamo wa ligi ya Ubelgiji, Royal Antwerp haijafanya vizuri kwenye mechi zake 5 ilizocheza, na matokeo yake timu hiyo ipo nafasi ya 3 kutoka chini. Sio hivyo tu, ingawaje timu hii ina support kubwa sana kutokana na ukongwe wake, lakini mara ya mwisho timu hii kuchukua kombe "kuu" ni wakati mama yangu mzazi akiwa na umri wa mwaka mmoja, na sia ajabu wakati Mzee Samatta enzi hizo akiwa Shule ya Vidudu.
Pamoja na hayo, kwangu naona hii ni fursa kwa Samatta kuonesha uwezo wake. Akifanya yale aliyokuwa amefanya Genk, na Royal Antwerp kufanikiwa kuchukua ubingwa, basi mademu wote wa Antwerp watakuwa wake. Mwamba ataimbwa kila kona, hadi ManU ambao ni marafiki wakubwa wa Royal Antwerp watafahamu uwepo wa Mbongo huyo!!
Mafanikio makubwa ya Royal Antwerp ni wakati Mbwana Samatta akiwa na umri wa mwaka 1, ambapo mwaka huo, yaani 1993 Royal Antwerp walifanikiwa kufika Fainali ya UEFA Cup Winners' Cup, ambapo timu ya Parma kutoka Italia ndie alichukua ubingwa mbele ya Royal Antwerp.
Je, safari ya Samatta kurudi Bongo inakaribia?