Mbuzi wamekata kamba

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,896
3,206
Leo nimejikuta nakumbuka haya maneno "mbuzi zimekata kamba".

Wakati niko mdogo nilipewa kazi ya kuchunga mbuzi wa mzee wangu.

Kwa sababu hakukuwa na mbuzi wengi kivile, nilikuwa nawapeleka asubuhi sehemu yenye majani na kuwafunga ili wasije kwenda kuharibu mazao ya watu.

Kwa bahati mbaya, wakati mwingine mbuzi wangu walikuwa wanakata kamba na hivyo kujikuta matatani pale wahanga walipokuwa wanaleta mashtaka nyumbani!

Nasikia kuna sehemu viongozi waliambiwa wajitahidi kula kwa urefu wa kamba zao, lakini baadhi ni kana kwamba wameshakata kamba tayari na sasa wanaharibu mazao ya watu.

Ee, Mungu tusaidie ili hawa waliokata kamba zao, basi wakamatwe na kuwekewa kamba mpya na imara ili wasiendelee kuharibu mazao yetu.

Amin.
 
Tatizo mbuzi akikata kamba anaenda kufungwa kwenye majani mengine badala ya kuchinjwa na kuliwa supu 😆
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom