mbuzi wa maziwa

mbuzi wa maziwa

Mutensa

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2009
Posts
421
Reaction score
92
Wadau. Bila shaka wenye maoifisi mnamalizia viporo vya weekend. Mimi niko shambani nakagua mimea na mazao huku nikiwa na kofia kubwa kichwani maana jua kali. Katika zunguka yangu nimeona kuwa nahitaji mbuzi wa maziwa.
Jamani kama kuna mtu ana hao mbuzi ani-pm au anitumie email kwenye mutensa@live.co.uk.
Kiufupi natafuta mbuzi jike wa maziwa...
Nisidieni.
 
Check na jamaa wa Sokoine University of Agriculture, Department of Animal Science and Production (DASP) watakusaidia!

dasp@sua.ac.tz

Mas
 
hawa ndio weekend farmers bana, utamkuta uko shambani yuko na sendozi na heineken mkono wa kulia na simu mkono wa kushoto. halafu wakitoka uko shamba wanapita bar wanapata ile kitu yenye mafua mpaka saa tatu usiku. Bongo ukiwa na ankara unatanua sana

Duh! Nilisahau topic ya msingi ya mtoa mada, Mkuu kama alivyokwambia Masanilo hapo juu wacheki hao jamaa watakusaidia mhe (weekendfarmer)
 
hawa ndio weekend farmers bana, utamkuta uko shambani yuko na sendozi na heineken mkono wa kulia na simu mkono wa kushoto. halafu wakitoka uko shamba wanapita bar wanapata ile kitu yenye mafua mpaka saa tatu usiku

Umesahau kitu, pembeni anakuwa amepaki mkoko wa kifisadi na mara nyingi shambani anakuwa amekwenda na nyumba ndogo! Mkewe anaambiwa leo mwende shopping mimi nitakuwa shamba! Bongo hiyoooo
 
Point ya msingi sana hiyo nilihisahu mkuu
 
Wakuu bado sijapata msaada katika hili. Tafadhari nisaidie kwa mnaoweza.
 
Kama uko dar na uko serious nitakuelekeza mbuzi walipo,na unapewa mbuzi mwenye mimba tayari. Ni-pm nikupe jibu la haja yako.
 
Niko seriously looking mkuu. Nimeku-pm contact details zangu.
 
tayari nimekujibu,naamini ukiwa serious mpaka jumamosi hii utakuwa umewaona mbuzi wenyewe huko. Suala la kununua si langu. Kazi kwako mkuu.
 
Wadau. Bila shaka wenye maoifisi mnamalizia viporo vya weekend. Mimi niko shambani nakagua mimea na mazao huku nikiwa na kofia kubwa kichwani maana jua kali. Katika zunguka yangu nimeona kuwa nahitaji mbuzi wa maziwa.
Jamani kama kuna mtu ana hao mbuzi ani-pm au anitumie email kwenye mutensa@live.co.uk.
Kiufupi natafuta mbuzi jike wa maziwa...
Nisidieni.

... na LapTop ukituma thread kwenye JF!!! :rofl:
 
Mkuu niliwapata,
bado natafuta fungu kuwanunua. Mmoja 150,000 Tsh.
bahitaji kama sita hivi...

Ni kweli kabisa,nilionana na yule mzee akaniambia kuwa ulimpigia mkaongea,sasa naomba nikupe tahadhali,ukichelewa mpaka mwisho wa mwaka huu mimi nitawalamba wote pale kwa yule mzee na jirani yake. Vipi kanyagio upo hapo?
 
Malila na Mutensa vipi hao mbuzi wa maziwa mlishawalamba? sometimes huwa narudia kusoma threads za nyuma kuona wapi tumefikia kwa vitendo baada ya kuandika kwenye JF.. najua kuna watu wapo serious sana... mbarikiwe wote mlio serious!!
 
Mungu yupo,kama huamini juu yako. Mwezi jana nimepata mbuzi mmoja jike na mwanae kwa bei ya kutupa kabisa kule kiluvya karibu na PM mstaafu. Nimelamba kwa buku arobaini. Nimekwenda kwa yule mzee,bado wapo wale mbuzi na wamenenepa vizuri. August hii nakwenda kumshawishi yule mzee nilambe mbuzi wote na nitamlipa cash.:A S-heart-2::rapture:
 
Malila, naomba unipatie contacts za huyo mzee.
Mi' mwenyewe nataka kama mbuzi watano, 4 majike na mmoja dume.
nataka niwalete Mtwar a.ka Ntwara.
 
Mungu yupo,kama huamini juu yako. Mwezi jana nimepata mbuzi mmoja jike na mwanae kwa bei ya kutupa kabisa kule kiluvya karibu na PM mstaafu. Nimelamba kwa buku arobaini. Nimekwenda kwa yule mzee,bado wapo wale mbuzi na wamenenepa vizuri. August hii nakwenda kumshawishi yule mzee nilambe mbuzi wote na nitamlipa cash.:A S-heart-2::rapture:

mzee nimekupata.... ngoja na mimi nianze utengenezaji banda then mradi uanze!!!!
 
Malila naomba uni pm contact za huyo mzee nataka nichukue mbuzi wawili wenye mimba kwa kuanzia.

Back
Top Bottom