Mbunge Zubeida Khamis Shaib Bega kwa Bega Utekelezaji

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MBUNGE ZUBEIDA SHAIB BEGA KWA BEGA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI JIMBO LA MFENESINI

Mhe. Zubeida Khamis Shaib, Mbunge wa Jimbo la Mfenesini akiongoza Viongozi wa Kamati ya Siasa ya Jimbo la Mfenesini katika zoezi la kukabidhi Vifaa vya Usambazaji wa Maji Safi na Salama pamoja na Mashine itakayowasaidia Wananchi na Wajasiriamali Wanaoanika Madagaa katika Shehia ya Kama Mkwajuni Jimbo la Mfenesini

Mhe. Zubeida Shaib alipata nafasi ya kuwahutubia Wananchi na Viongozi mbalimbali waliohudhuria na kuwasikiliza Wananchi maoni, ushauri, kero na changamoto zinazowasibu ikiwa ni utaratibu wake kuwasikiliza Wananchi anaowaongoza

Aidha, katika hotuba yake, Mhe. Zubeida Shaib amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Hassan Mwinyi kwa Kusimamia vilivyo maendeleo ya Taifa.

Kwa upande wao, Viongozi na Wananchi wa Jimbo la Mfenesini walimshukuru sana Mhe. Zubeida Shaib kwa kufanya ziara jimboni huku wakimpatia zawadi mbalimbali ikiwemo Kuku kama ishara ya kuonyesha kumpa ushirikiano

Mwisho, Mhe. Zubeida Shaib amewashukuru Viongozi na Wananchi kwa ushirikiano wanaompa na kuendelea kuwasisitiza kuwa na Umoja, kufanya kazi kwa bidii na Kusimamia vizuri utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwani ndiyo mkataba wa CCM na Wananchi waliowaamini.

WhatsApp Image 2023-09-05 at 17.28.45.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-05 at 17.28.46(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-05 at 17.28.48.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-05 at 17.28.49.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-05 at 17.28.50.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-05 at 17.28.48(2).jpeg
 
Back
Top Bottom