Mbunge Zimbabwe avunja rekodi ya busu Afrika

Primier

Member
Dec 16, 2015
86
14
160215135223_zimbabwe_kissing_record_624x351_bbc_nocredit.jpg

Image caption Mbunge Joseph Chinotimba Zimbabwe
Mbunge mmoja nchini Zimbabwe Joseph Chinotimba ameingia katika kumbukumbu za Afrika baada ya kumbusu mke wake Vimbai kwa muda mrefu zaidi kuwahi kunakiliwa barani Afrika.


Mbunge huyo na mkewe walizoa tuzo hilo baada ya kupigana busu kwa dakika 10 na sekunde 17.

Rekodi hiyo iliwekwa katika hafla moja iliyopigiwa upatu na kunadiwa kuwa ''Mashindano ya busu refu zaidi kuwahi barani Afrika''


160215135432_zimbabwe_kissing_record_624x351_bbc_nocredit.jpg

Image caption Bwana Chinotimba na mkewe Vimbai
Hafla hiyo ilipangwa na kuandaliwa kwa ushirikiano na waandalizi wa Daftari la rekodi barani Afrika.

Hafla hiyo iliandaliwa katika mji mkuu wa Harare kama sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanao iliyoadhimishwa jumapili.
 
Badala ya kuweka rekodi za kufanya mabadiliko yanayo impact wananchi (kama Magufuli anavyofanya) wenyewe wanajivunia kuvunja rekodi ya mabusu
 
Mbna waziri kama ana pengo ivi usije ukakuta ulimi wa wife ulinasa akashindwa kuchomoka hizo dakika kumi..
 
Huu ujinga nani amewafundisha wanzimbabwe mbona walikua hawana tabia kama hizo.
 
Hilo jina lake lenyewe CHINOTIMBA ,ukirudisha herufi I nyuma ya T na herufi O ukapeleka mbele ya T ,Hushangai kabisa yeye kupewa hizo tuzo
 
Back
Top Bottom