Mbunge yule Kijana aliyeniomba Ushauri...!

Mbunge yule Kijana aliyeniomba Ushauri...!

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,250
Ndugu zangu,

Kuna simulizi ya kwenye Biblia. Enzi za Mfalme Suleiman kuna watu waliolalamika sana, kuwa wanaishi kwenye manyanyasiko mno.

Kukawa na vijana waliokuwa na kiu ya kutaka mabadiliko ya uongozi wa mfalme. Walitaka watawaliwe na mfalme kijana.

Wazee walipoombwa ushauri wakatamka; kuwa vijana mara nyingi hupungukiwa na busara. Hivyo, si lazima mfalme awe kijana.

Vijana wale wakakaidi ushauri wa wazee. Wakampata Mfalme kijana. Naye alipokuwa madarakani, alitenda mara mbili ya dhambi alizotenda mtawala aliyetangulia.

Mfano, kama mtawala aliyepita alitoa adhabu ya kuchapa kwa mjeledi, basi, mfalme kijana yeye alitaka atumie rungu. Hakukuwa na nafuu walioitarajia.

Ndugu zangu,

Juma la kwanza tu baada ya Bunge kuanza mwaka 2010, nikiwa njiani kutoka Singida nilisimama Dodoma. Hapo nilipata bahati ya kukutana na mmoja wa Wabunge vijana kutoka kambi ya upinzani.

Tulikaa na kunywa chai pamoja. Alinitaka pia ushauri katika kazi yake. Hakika, niliingiwa na matumaini makubwa juu ya fikra zake za kimaendeleo pale alipoanza mazungumzo. Mathalan, kati ya dhambi kadhaa zinazofanywa na wabunge alizoziona, akaniambia juu ya kustaajabishwa kwake na tabia ya Wabunge kufoji risiti za safari zao ili wapate fedha zaidi.

“Yaani kaka Maggid, sikujua kuwa Wabunge hawa wanafanya mambo kama watoto wa shule. Yaani Mbunge anahangaika kufoji risiti za mafuta na kudai kuwa ametokea mahali fulani kuja hapa Dodoma wakati sio!” Aliniambia kwa uchungu mbunge yule kijana.

Lakini, mashaka yakanijia pale nilipomwuliza;

“Sasa ukitoka hapa Dodoma umejiandaa na kipi cha kwenda kuwaambia wapiga kura wako kwenye mkutano wako wa kwanza wa hadhara baada ya kikao chako cha kwanza Bungeni?”

Mbunge yule kijana aliniangalia na kuniambia; “ Naenda kwanza Dar kuhangaikia gari yangu mpya!”

Nikawa nimekatishwa tamaa na Mbunge yule kijana. Kwamba katika juma la kwanza tu la kukaa Bungeni, tayari ameanza kufikiria kuhangaikia masuala yake binafsi, na si masuala ya wananchi waliompigia kura!

Naambiwa, naye siku hizi anapomaliza vikao vya kuongea hata na jamaa zake tu, haraka sana hukimbilia kutoa ‘ bahasha za nauli’.

Siku hizi mbunge yule kijana ana gari zaidi ya ile aliyokwenda kuichukua Dar. Amekuwa mbunge-mfanyabiashara.

Sifikirii tena kwenda kumpa ushauri mbunge yule kijana, maana, naweza kuambulia kudhalilishwa kwa kupewa ‘bahasha ya nauli’ ya kurudia nyumbani kwangu.

Naam, ni heri ya ndugu yangu John Komba, hata akisemwa kuwa anasinzia Bungeni, bado ana mchango kwa jamii; kwa nyimbo zake zenye kuburudisha na kuelimisha.

Ndio, nchi hii inahitaji mabadiliko ya kimsingi, lakini, ni vizuri kutambua, kuwa wengine tunaofikiri kuwa wanaweza kutusaidia katika kuyafikia mabadiliko hayo, hawana tofauti kabisa na baadhi ya tunaofikiria hawatufai.

Na hutokea, kuwa dhambi wafanyayo, na watakayoifanya, yumkini yaweza kuwa ni mara mbili ya inayofanywa na baadhi ya waliopo sasa.

Ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
 
Kwa hiyo katika madhira/mauzi yote ya wabunge, lililokuudhi ni hilo tu? ?

Hujayaona mengine ya magamba wenzio!??
 
Naam, ni heri ya ndugu yangu John Komba, hata akisemwa kuwa anasinzia Bungeni, bado ana mchango kwa jamii; kwa nyimbo zake zenye kuburudisha na kuelimisha.

Ndio, nchi hii inahitaji mabadiliko ya kimsingi, lakini, ni vizuri kutambua, kuwa wengine tunaofikiri kuwa wanaweza kutusaidia katika kuyafikia mabadiliko hayo, hawana tofauti kabisa na baadhi ya tunaofikiria hawatufai.

Na hutokea, kuwa dhambi wafanyayo, na watakayoifanya, yumkini yaweza kuwa ni mara mbili ya inayofanywa na baadhi ya waliopo sasa.

Ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa.

Aisee kumbe Komba ana nafuu kwako Maggid kuliko mbunge wa upinzani aliyekuudhi kwa kutamka anaenda kununua gari? Plastic ideas you got there
 
Wewe kweli wa ajabu sana!
Yani mtu anaye sinzia bungeni unamuona wa maaa!
Na wanao forg risit kupata pesa kwako ni wa maana kuliko mtu anaye kwambia anaenda kutengeneza gari lake?

Hapa kuna unafiki mwingi kuliko uchungu wa nchi!
 
Akili ndogo ndogo zipo kazini,na watajaribu kila liwezekanalo kujinadi,ila waelewe tu kwamba,mabadiliko ni lazima,wananchi wamechoka,maana akili zao ndogo ndogo haziwezi kupambanua wala kutafakari issues.
 
Jibu: Tupo safarini tumepigwa torch ya speed na kusimamishwa kwa muda. Baada ya konda kuzunguka nyuma ya bus akiwa na Traffic ghafla tunaruhusiwa! Hii ndo Tanzania.
 
Anataka kusema wabunge wa upinzani hawana tofauti na wa CCM,wote wachumia tumbo tu.!
 
Akili ndogo ndogo zipo kazini,na watajaribu kila liwezekanalo kujinadi,ila waelewe tu kwamba,mabadiliko ni lazima,wananchi wamechoka,maana akili zao ndogo ndogo haziwezi kupambanua wala kutafakari issues.

Ni zamu ya wengine nao kula, kwani ni lazima iwe CCM tu, wakati wa watanzania wengine nao wapewe nafasi wakila sawa tu maana hata waliopo nao wanakula tu! Hatukatishwi tamaa kwa namna yoyote ile!
 
mbunge kijana wa upinzani amechoka na kikao cha wiki mbili bungeni dodoma anawahi kushughurikia gari yake dar.wapinzani ni zaidi ya ujuavyo. majid
 
Vipi,umekwenda jimboni kwake kuona nin amefanya mpaka sasa au umekalia majungu ya umiliki wa magari?
 
hahahahaa PR manager wa kapteni Komba..hadithi yake inatufundisha Kepteeeeni aendeleee kulala...yeera, sponsored by magodoro dodoma:A S shade:
 
Mnafiki angekuwa nguo tungemtambua kwa rangi!

Kama kweli wewe una uchungu na nchi , acha unafiki na umtaje kabisa jina huyo Mbunge na chama chake ili wananchi tumtambue.
Wacha kumficha muovu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ha ha ha haaa.....Maggid. Naona kama mbunge yule alikuwa muongo juu ya risiti za mafuta. Kwani bunge linajua kila mbunge ametoka wapi, na wala hawanaga sababu ya kupeleka risiti. Ni wana chati ya umbali, wanaangalia umbali na bei ya mafuta ya sokoni, na kuingiza pesa kwenye akaunti.

Nakushangaa kwa mbunge kutoa bahasha ya nauli ni tatizo kwako. na nakushangaa pia kushangaa mbunge huyu kuhangaikia gari lake, sijui angefikaje kwa wananchi.
Mbona wee kutwa wafanya kazi zako na gari lako,mtena muda wowote wasafiri.
Leta mambo ya msingi Maggid.
 
Back
Top Bottom