Mbunge wangu Lema mkomboe kijana Ismaili Bakari

Mbunge wangu Lema mkomboe kijana Ismaili Bakari

mzalendokweli

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2012
Posts
579
Reaction score
138
Huyu kijana ni mhanga wa uliloahidi kwenye kampen kuliondoa, yaan ubambikizaji wa kesi unaofanywa na Polisi Arusha. Kuotkana na mama yake ambaye ni mwkiti wa Mtaa kona Esso dogo katupiwa kesi zisizo na msingi. Tupia jicho Murder. No 276 iko Arusha/Arumeru District court ambayo anaedaiwa kuuwawa hata hajajulikana wazi mpaka sasa, na Robery No 422 nayo Arusha/Arumeru District Court,hii hata leo ukimfuata mlalamikaji atakwambia Ismaili sio mwizi wake kwan anamfahamu vizur. Hii ya Robbery enzake ilifutwa siku chache zilizopita kwan mlalamikaji alikataa katakata kumfahamu huyu kijana. Dogo anateseka kuanzia june 2012 kisa mamaake mwenyekiti mtaa kwa magamba na anasumbua Kona Esso. Huyu mama anastahili kuunganishwa na makamanda kwan ana msimamo na ni mpigania maendeleo ndio mana diwani wa kata yake ambae ni Gamba anampiga vita mbaya. Kuna mengi yamejificha nyuma ya pazia. Kuna mambo kama ya wizi wa sukari kwe magodown Esso nk. Hili ni dokezo tu lakin mkifuatilia mtachimbua uozo mwingi na kamtandao ka uhalif ikiwa ni pamoja na wizi wa sim kuanzia Summit Center mpaka soko mjinga. Hili ni dokezo tu mengine utayaibua kama utaamua kufuatilia.
 
Pole sana kwake, waziri Nchimbi afike pia huko kama alivyofanya kule Mbeya na Kagera.
 
Ina uma sana kama ni kweli, hopefully Lema ataifanyia kazi hoja yako.
 
naiona hoja hapo ingawa mwandiko umenipa shida kidogo,wasiliana naye kamanda GL
 
Kabla hamjafikia uamuzi inabidi mfanye uchunguzi kwanza,
Je, huyu mtu ana historia ipi?
Sio kila jambo ni kuilaumu polisi na tusije kufikia hatua eti kila mtu kabambikiwa kesi mwisho hakuna mhalifu atakamatwa kwa sababu kila mtu atadai kabambikiwa
Nikuulize swali
ULIISHA WAHI FIKA MAHAKAMANI UKASIKIA MSHTAKIWA ANASEMA YEYE NI MKOSAJI? aslimia 99 husema wameonewa
Sikatai anaweza kuwa kweli kabambikiwa lakini uchunguzi ufanyike kwanza
 
Pole sana Bwana Ismail Bakari. Ingawa sijaelewa. Mh. Lema amesikia na hakika atafuatilia suala la Bwana Bakari.

Cc Crashwise
 
Last edited by a moderator:
Kabla hamjafikia uamuzi inabidi mfanye uchunguzi kwanza,
Je, huyu mtu ana historia ipi?
Sio kila jambo ni kuilaumu polisi na tusije kufikia hatua eti kila mtu kabambikiwa kesi mwisho hakuna mhalifu atakamatwa

Nina mashaka na uelewa wako kama hatajwi aliyeuawa, mlalamikaji anakana kumfahamu huyo kijana; polisi wamemuweka ndani kwa kigezo gani?

Baada ya mahakama kubaini au kuambiwa hayo kama waliambiwa hatua gani zimechukuliwa? Una haki ya kutetea magamba hata kwa mambo mabaya ila jiulize unaelewekaje na jamii?
 
Kabla hamjafikia uamuzi inabidi mfanye uchunguzi kwanza,
Je, huyu mtu ana historia ipi?
Sio kila jambo ni kuilaumu polisi na tusije kufikia hatua eti kila mtu kabambikiwa kesi mwisho hakuna mhalifu atakamatwa kwa sababu kila mtu atadai kabambikiwa
Nikuulize swali
ULIISHA WAHI FIKA MAHAKAMANI UKASIKIA MSHTAKIWA ANASEMA YEYE NI MKOSAJI? aslimia 99 husema wameonewa
Sikatai anaweza kuwa kweli kabambikiwa lakini uchunguzi ufanyike kwanza

Huwezi kuwashawishi watu wasiiLaumu polisi kutokana na utendaji kazi usiozingatia uadilifu.
Unakumbuka Zombe na sakata la wafanyabiashara wa madini?Umesoma habari za Nchimbi kwenye magazeti ya leo?
Na kama umesoma vizuri Lema ameombwa afuatilie,pia kwa hali kama hii kutetea polisi yataka moyo au uwe mdau wao
 
Hoja zote ni za muhimu,mtoa mada kaelezea anachokijua/kiamini na huyu gamba lukosi naye kaja na kamchango kake ambako kiungwana kabisa kina mantiki,tunaomba wahusika wafuatilie jambo hili,na ushauri wa huyu Xgwanda a.k.a msaliti pia uzingatiwe,unaweza ukampeleka mtuhumiwa wako ukiwa na kila aina ya kielelezo ila mwisho wa siku hoja ya kuonewa/kubambikiwa ika prevail na ukajikuta unatoka mahakamani kichwa chini,si kila anayedai kuonewa huwa ameonewa kweli,wala si kila mfungwa ana hatia.
 
Kabla hamjafikia uamuzi inabidi mfanye uchunguzi kwanza,
Je, huyu mtu ana historia ipi?
Sio kila jambo ni kuilaumu polisi na tusije kufikia hatua eti kila mtu kabambikiwa kesi mwisho hakuna mhalifu atakamatwa kwa sababu kila mtu atadai kabambikiwa
Nikuulize swali
ULIISHA WAHI FIKA MAHAKAMANI UKASIKIA MSHTAKIWA ANASEMA YEYE NI MKOSAJI? aslimia 99 husema wameonewa
Sikatai anaweza kuwa kweli kabambikiwa lakini uchunguzi ufanyike kwanza

Mbona wakurupuka?kwani wewe unaelewa nini juu ya tupia jicho.Ngoja nikuelimishe kidogo we gamba ni kwamba Kmanda Lema anadokezwa kuwa kuna haja ya kufanya uchunguzi binafsi juu ya kesi ya mtajwa hapo juu.
 
Pole sana kwake, waziri Nchimbi afike pia huko kama alivyofanya kule Mbeya na Kagera.

Tena aje haraka Amulike pale mkoani maana pamegeuka sehemu ya biashara!Kuna kigogo analindwa makao makuu Ili kufanikisha biashara za mirungi!baadhi ya maofisa waliokaa muda mrefu pale arusha wanamtishia hata rpc Ashindwe kufanya kazi zake!Polisi tujulisheni Imefikia wapi ile Ishu ya mjeshi na meno ya tembo!
 
Kabla hamjafikia uamuzi inabidi mfanye uchunguzi kwanza,
Je, huyu mtu ana historia ipi?
Sio kila jambo ni kuilaumu polisi na tusije kufikia hatua eti kila mtu kabambikiwa kesi mwisho hakuna mhalifu atakamatwa kwa sababu kila mtu atadai kabambikiwa
Nikuulize swali
ULIISHA WAHI FIKA MAHAKAMANI UKASIKIA MSHTAKIWA ANASEMA YEYE NI MKOSAJI? aslimia 99 husema wameonewa
Sikatai anaweza kuwa kweli kabambikiwa lakini uchunguzi ufanyike kwanza

Ukiangalia namba ya kesi ni ya 200+ inamaana kuna 200 zingine ambazo hazijatajwa hapa.
 
Mbona wakurupuka?kwani wewe unaelewa nini juu ya tupia jicho.Ngoja nikuelimishe kidogo we gamba ni kwamba Kmanda Lema anadokezwa kuwa kuna haja ya kufanya uchunguzi binafsi juu ya kesi ya mtajwa hapo juu.

Nashukuru sana GT. Hawa wengine sjui wanakujaje humu.
 
Ni kweli inauma kwa stori ya upande wa mlalamikaji,
Lakini je? umesikiliza upande wa mashitaka?

Bwana Chris hapa sijaleta siasa. Ni serious issue kijana anateseka nimefuatilia hili swala kwa undani inasikitisha sana. Nimefanikiwa hata kuona barua alioandika aliedaiwa kua mlalamikaji kwe kesi iliofutwa akiieleza mahakama kua huyo wanaedai kua jambazi aliemuibia katika bar yake yeye hamtambui kwan anakumbuka vizur sura za waliompora lakin polisi waliendelea kung'ang'aniza hiyo kesi na kumbembeleza mlalamikaji akatoe ushahidi mlalamikaji akakataa na akawa anashirikiana na familia ya mshtakiwa polisi walipoona hivyo wakambambika Robbery ingine ambayo nayo mlalamikaji wake anadai waliompora walivaa mask so haez kutambua kama mshtakiwa ndie. Hata hvyo polis wanakomaa kua ndie. Kifupi kuna harufu inayoashiria kuna vitu haviko sawa ndio mana nikamwomba mbunge wetu "afuatilie".
Mnisamehe kama mwandiko unatoka vibaya kasim kangu sio smart.
 
poleni sana,ila naelewa wazi kuwa,arusha mmepata kiongozi lema mmempata msimwache pekee atakiwa kuungwa mkono.
 
Back
Top Bottom