Mbunge wangu Godbless Lema, umebaki mpweke gerezani, majuto ni mjukuu


Kada wa CHADEMA

Kada wa CHADEMA

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2016
Messages
290
Likes
616
Points
180
Kada wa CHADEMA

Kada wa CHADEMA

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2016
290 616 180
Siku zote majuto ni mjukuu. Majuto huja baada ya kufanya kosa kubwa ambalo haliwezi kurekebishwa kwa namna yoyote ile.

Ninakuona Mbunge wangu Godbless Lema jinsi ulivyojikunyata kwenye Selo usijue nini hatma ya maisha yako. Jukwaa lilikudanganya kuwa ukiwa mbunge, unaweza kusema lolote hata kama kusema lolote juu ya mamlaka kuu ya nchi. Hii yote ni kutokana na kibri cha madaraka, malezi mabaya ya utotoni pamoja na athari ya shughuli zako kabla hujawa mbunge.

Inaniuma sana kuona sasa wana Arusha wakiachwa bila kuwa na mbunge kwa sababu ya ujinga wa mtu mmoja tu na kutochunga kauli zake. Inaniuma sana. Kila nikifikiria jinsi wana Arusha walivyokupigia kura nyingi sana kwa matarajio utawawakilisha vema, sikutegemea kama leo hii utawaacha yatima. Walikutuma uende Bungeni ukawasemee kero zao na kuwasaidia kutatua matatizo yao. Hawakutuma umtukane Rais wala kuwasemea juu ya ndoto ulizoota kuwa Rais atakufa kabla ya 2020.

Mbunge wangu Lema, nayajua maisha ya Selo kwa vile niliwahi kupitia huko kuanzia usiku wa Oktoba 26, 2015 tulipokamatwa pale King D Sinza tukimsaidia Mzee aibuke mshindi. Nayajua maisha ya Selo tangu siku hiyo na sina hamu tena ya kurejea huko. Ukimuona mtu anatamani kurejea Selo basi unapaswa kumtafakari mara mbili mbili kwani kuna wengine wanafurahia maisha ya kule hasa nyakati za usiku.

Mbunge wangu Lema, nikikumbuka yaliyonipata usiku nikiwa Selo nikihamishia kwa mbunge wangu Lema hakika napatwa na huzuni kubwa sana. Kama yale ambayo mimi nilifanyiwa na wale niliowakuta anafanyiwa mbunge wangu basi kwa hakika ni fadhaha kubwa sana. Sehemu ya kulala inakuwa ni ndogo, watu wanakuwa na harufu za aina tofauti, mbu wanatung'ata kila kona, nafasi hata ya kunyoosha miguu hakuna, msosi unakuwa ni wa manati, hakuna nafasi ya kuongea na mwenzi wako kwa vile hayupo huko. Hakika ni tabu na mateso makuu.

Mbunge wangu Lema, wale waliokuwa wanakushangilia na kusema "Na Iwe Hivyo" wakati unamuombea mabaya Rais wa nchi leo hii hawapo pamoja nawe. Umebaki mpweke usipate hata wa kukushauri. Kosa umelitenda na limetendeka.

Mbunge wangu Lema, chama kimeshakupa kisogo. Hii ina maanisha kuwa hawaungi mkono kile ulichotamka na kwa hiyo kosa hilo ulilotenda limekosa baraka ya chama. Si Mbowe wala Mashinji wala Lowasa ambao wamediriki hata kuja Arusha kukuona na kukujulia hali. Wapo busy na kujenga chama. Jifunze kitu. Hata wale mawakili Nguli, Peter Kibatala, John Mallya na Tundu Lissu wameshindwa kabisa kukuokoa ili usiendelee kusota Selo. Ngoma imekuwa ngumu kwao.

Mbunge wangu Lema, ona jinsi Mkeo anavyogalagala kitandani usiku wa manane huku akijaribu kupapasa huku na huku pande zote za kitanda akitaraji kukugusa. Wapi! Lema hayupo tena chumbani bali yupo Selo ambako wamelala kwa kubanana.

Mbunge wangu Lema, watoto umewaachia majonzi makubwa sana. Jana nimemsikia mtoto wako mdogo akisema kwa huzuni kubwa sana! Alisema hivi;" Baba, mbona umekosa mapenzi kwa watoto wako kwa kukaa nje ya familia kwa zaidi ya wiki mbili sasa?". Iliniuma sana kwa sababu mtoto yule hajui nini kinaendelea kwa baba yake. Umemkwaza sana na unamtesa mno.

Mbunge wangu Lema. Nakuhurumia sana
 
M

mwasu

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2011
Messages
8,553
Likes
6,660
Points
280
M

mwasu

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2011
8,553 6,660 280
Unafiki ni kitu kibaya sana, acha leo Lema awe mpweke gerezani kwa kuonewa na viongozi wa ccm, ila atakuwa shujaa uraiani na atavikwa taji la ushindi mbinguni, ole wake aoneaye mtu kwa kuwa ana madaraka, dhambi hii itamtafuna yeye nauzao wake na mwisho ni jehanamu ya milele.
 
balimar

balimar

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Messages
3,718
Likes
4,722
Points
280
balimar

balimar

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2015
3,718 4,722 280
Ajikaze mtoto wa kiume jela si jeraha.
Asimamie anachokiamini siku moja tutamwelewa au ataeleweka. Jela hata wewe ulieandika huo uzi unaweza tokea ukaa tu walikaa mawaziri hata marais wanakaa these days sioni la ajabu
 
J

jembe afrika

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Messages
7,222
Likes
1,303
Points
280
J

jembe afrika

JF-Expert Member
Joined Jan 15, 2014
7,222 1,303 280
Mkuu unamhurumia mwenzio wakati wewe ndo mhanga namba moja Wa kuisoma namba
 
D

Duterte

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2016
Messages
1,066
Likes
1,106
Points
280
D

Duterte

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2016
1,066 1,106 280
Inasikitisha sana. Haswa kwa hao watoto aliowaacha bila mapenzi na ulinzi wa Baba. Mkewe anaweza kuwa na wa kumliwaza uraiani. La sivyo angemshauri na kumsihi Mumewe mapema kutokana na mienendo yake na Utovu wa Nidhamu kama kiongozi.
 
Bome-e

Bome-e

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Messages
9,652
Likes
7,198
Points
280
Bome-e

Bome-e

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2014
9,652 7,198 280
Pale serikali inapotumia nguvu kubwa kupambana na harmless people,its a shame.Sioni msingi wa kesi zaidi ya kukomoana na ubabe.Muandishi ni unafiki tu umekupelekea kuandika hayo,we know your true identity,wageni jukwaa hili ndio wanaweza kuwa fooled.
 
MR MAJANGA

MR MAJANGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2014
Messages
2,292
Likes
3,522
Points
280
MR MAJANGA

MR MAJANGA

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2014
2,292 3,522 280
Kwa serikali ya ccm hayo anayopitia Lema Ni madogo, kama serikali ya ccm waliweza kuwauwa wale wafanyabiashara wa madini na kuwaita majambazi itakuwa Lema?
 
API Gravity

API Gravity

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2016
Messages
658
Likes
763
Points
180
API Gravity

API Gravity

JF-Expert Member
Joined Mar 15, 2016
658 763 180
Unafiki ni kitu kibaya sana, acha leo Lema awe mpweke gerezani kwa kuonewa na viongozi wa ccm, ila atakuwa shujaa uraiani na atavikwa taji la ushindi mbinguni, ole wake aoneaye mtu kwa kuwa ana madaraka, dhambi hii itamtafuna yeye nauzao wake na mwisho ni jehanamu ya milele.
Haipo jamii inayofurahia utovu wa nidhamu na mdomo mchafu wa Lema. Mwambieni akubali kubadilika jana siyo leo, anaweza kuonekana shujaa kwa wachache wenye akili kama zake lakini kwa wengi anaonekana kituko.
 
Y

YAHERI MUNGU

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2016
Messages
321
Likes
214
Points
60
Y

YAHERI MUNGU

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2016
321 214 60
Unafiki ni kitu kibaya sana, acha leo Lema awe mpweke gerezani kwa kuonewa na viongozi wa ccm, ila atakuwa shujaa uraiani na atavikwa taji la ushindi mbinguni, ole wake aoneaye mtu kwa kuwa ana madaraka, dhambi hii itamtafuna yeye nauzao wake na mwisho ni jehanamu ya milele.
Nyinyi endeleeni tu kujifariji na kumfariji mbunge wenu Lema kwa ujeuri wake na utovu wa nidhamu.Anavuna anachokipanda. Katika AMRI kumi za Mungu, moja inasema kuwa "Mheshimu mzazi wako upate kuishi muda mrefu", hapa mzazi ni pamoja na mkubwa. Vilevile Biblia inasema kuwa "Heshimuni mamlaka iliyopo", mamlaka ni pamoja na Mamlaka ya Rais wa nchi. Sasa huyo Lema hilo taji la ushindi huko mbinguni atapewa na nani ikiwa hata Mungu mwenyewe hapendi watovu wa nidhamu kama Lema?
 
M

mwasu

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2011
Messages
8,553
Likes
6,660
Points
280
M

mwasu

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2011
8,553 6,660 280
Haipo jamii inayofurahia utovu wa nidhamu na mdomo mchafu wa Lema. Mwambieni akubali kubadilika jana siyo leo, anaweza kuonekana shujaa kwa wachache wenye akili kama zake lakini kwa wengi anaonekana kituko.
Lema hajawahi kuwa na mdomo mchafu bali wenye midomo michafu wana mnenea machafu, kusema kuwa kaota ndoto ya kuhusu kifo cha mkuu ni tusi? Acha kujitoa ufahamu Lema ni shujaa kwa kuwa anasema kweli aionayo kuliko kuwa na dhambi za kufunga watu midomo, haya next shingongo maana nae kasema kweli, ccm lazima wajitafakari.
 
K

Kichakoro

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2008
Messages
1,998
Likes
2,201
Points
280
K

Kichakoro

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2008
1,998 2,201 280
Siku zote mtumwa hupaswa kunyenyekea kwa slavemaster ila ukiona mtumwa amekuwa na nguvu kuliko boss wake na boss kakaa kimya basi jua kuna shida kubwa sana
 
M

mwasu

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2011
Messages
8,553
Likes
6,660
Points
280
M

mwasu

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2011
8,553 6,660 280
Nyinyi endeleeni tu kujifariji na kumfariji mbunge wenu Lema kwa ujeuri wake na utovu wa nidhamu.Anavuna anachokipanda. Katika AMRI kumi za Mungu, moja inasema kuwa "Mheshimu mzazi wako upate kuishi muda mrefu", hapa mzazi ni pamoja na mkubwa. Vilevile Biblia inasema kuwa "Heshimuni mamlaka iliyopo", mamlaka ni pamoja na Mamlaka ya Rais wa nchi. Sasa huyo Lema hilo taji la ushindi huko mbinguni atapewa na nani ikiwa hata Mungu mwenyewe hapendi watovu wa nidhamu kama Lema?
Usikariri maandiko vibaya wewe, sio kila mamlaka inatoka kwa Mungu, na si kila asemalo mtoto kuhusu mzazi wake ni kumkosea heshima, kuna wazazi walevi, wazinzi na wezi mtoto anaweza kuusema ubaya wa mzazi na hapo hata kuwa kamkosea heshima, hata Mungu ameonya yeye auaye kwa upanga nae ata uawa kwa upanga, hakuna kitu kibaya kama kutumia malaka kuangamiza wenye haki.
 

Forum statistics

Threads 1,274,107
Members 490,586
Posts 30,501,243