Mbunge wa zamani CCM ajiunga na CHADEMA

Mbunge wa zamani CCM ajiunga na CHADEMA

Hata vitani ikitoakea wapinzani mmewashambulia na kuwasukuma nyuma huku wakiwa wameacha silaha zao, silaha hizo huwa haziachwi, ndio maana tunaisambaratisha CCM huku tukichukua wanachama wake ambao tunaona wazi kabisa kwamba watasaidia mapambano, chama bila wanachama na si ufisadi na ulaji rushwa. Big up sana CHADEMA.
 
...ni heri yake amewahi kabla milango ya Safina haijafugwa...hao wenye akili za samaki waliong'ang'a niwa na magamba ndo watakao lia midomo juu siku(2015) ikifika...
 
...ni heri yake amewahi kabla milango ya Safina haijafugwa...hao wenye akili za samaki waliong'ang'a -niwa na magamba ndo watakao lia midomo juu siku(2015) ikifika...
 
Ni hatari kuwapokea hawa jamaa.Mbele ya safari watakua wengi na watakivuruga chama
 
kwa kweli si kila kitokacho ccm cha kuchukua wanaweza wakahamia huku CDM na uozo na akili za kiccm wakaua chama CDM.
nakubaliana na ww, kila watu 1000 wa ccm mmoja tu ndo anaweza akawa msafi.
 
Mbunge wa zamani CCM katika majimbo ya Mpwapwa na Kongwa Gideon Senyagwa amekihama chama hicho na kujiunga na chama cha CHADEMA.Mbunge huyo alipewa kadi Na. AO CDM 0101716.

Mbunge huyo wa zamani alihamia CDM Novemba 9 pamoja na makada wengine wa CCM wakiwemo Mkiti wa Tawi la Ngh'umbi Boazi Madukani na Katibu wa Tawi hilo Mbagilwa Festo.Pia CHADEMA imezoa wanachama 260 katika jimbo hilo kama ishara ya kuunga mkono uamuzi wa mbunge huyo wa zamani.


Akihutubia maelfu ya watu katika mkutano uliofanyika Kibaigwa Senyagwa alisema kuwa hafurahishwi na vitendo vinavyofanywa na CCM ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili kutoka kwa baadhi ya viongozi huku wakipuuza kero za wananchi.

Aliwataka wananchi kote nchini kuunganisha nguvu na CHADEMA kuiondoa CCM madarakani.Amesema CCM inapaswa kujua mwisho wake umekaribia kama hata mtu kama yeye ameamua kukiacha chama hicho.

Source: Tanzania Daima.
Mfa Maji huyo anatapatapa
 
...ni heri yake amewahi kabla milango ya Safina haijafugwa...hao wenye akili za samaki waliong'ang'a niwa na magamba ndo watakao lia midomo juu siku(2015) ikifika...

Safina ipi ya Nuhu Au Noah ya kuelea Au ya chadema ya kuzama.
 
Tunashukuru kwa kuja na wanachama wapya maana ndio lengo kuu la CHADEMA kutafuta wanachama kwa kadri iwezekanavyo.!
 
Naipa big up M4C inazidi kukusanya wanawapotevu na kuwarudisha kundini congs CDM ndondo si chululu alafu haba na haba hujaza kibaba collect more energy for2015 with peoples supports tutakuwa na CDM-Demoract elect of TZ kwani Republican - CCM now ruling failed to bring signicant change only slogans of maisha bora kwa kila mtanzania which failed!
 
Chadema mekuwa desperate sana mimi nilijua chama chenu mnataka kujenga na damu changa na watu wenye mawazo mapya kumbe ni recycle bin!
Chadema kama chama kinapokea wale wanaoiamini itakadi yake. Kusema tunachukua makombo au wazee inashangaza!
 
Hivi inakuaje mwnachama akiwa chama kingine anakua fisadi lakini akija cdm ndiyo mpiganaji?nikigezo gani mnakitumia hapo mkuu?
 
Hivi inakuaje mwnachama akiwa chama kingine anakua fisadi lakini akija cdm ndiyo mpiganaji?nikigezo gani mnakitumia hapo mkuu?

Kwa sababu anatubu madhambi yake na kuomba msamaha.
 
Back
Top Bottom