Mbunge wa zamani CCM ajiunga na CHADEMA

Mbunge wa zamani CCM ajiunga na CHADEMA

Lakini mbona juzi alihudhuria mkutano mkuu wa Kizota! au na yeye aliiwakilisha Chadema? Hongera Cdm kwa kupokea makombo ya CCM! huyu mbunge uliemtaja wala hana umaarufu wowote! Jee, sumae nae ameshapewa Kadi?
Kama hana Umaarufu, kutoka kwake amezoa wanachama wa Magamba 260, kama angekuwa na umaarufu sijui angezoa wangapi? Magamba yakikosa hoja bwana!
 
Hivi gazeti la uhuru na mzalendo yanasomwa wapi, mbona kwenye mbao za kuuza magazeti siyaoni?
Umeonaee!mie huwa nayatafuta sana hasa ninapokuwa nimechoka ili nione wenye mawazo mgando wanafikiri vipi lakini siyaoni,mara ya mwisho niliyaona kwenye luninga pale wajumbe wa CCM walipokuwa wanayasoma kwa unafiki!
 
kwa kweli si kila kitokacho ccm cha kuchukua wanaweza wakahamia huku CDM na uozo na akili za kiccm wakaua chama CDM.
 
Hongera kwa chadema, hakuna kitu kizuri kama kupata watu wenye ushawishi kwenye maeneo yenye ngome ya mpinzani wako.
dodoma, singida na tabora ni mikoa inayowatesa sana wapinzani kama hali imeanza kuwa hivi ni sawa na mwanaume aliyekuwa akipokea matusi kwa mwanamke anayemtokea af taratibu anaanza kupokea meseji na kuulizwa, ''umeamkaje.?''
 
kwa hiyo wajameni mtu akitaka kujiunga cdm watumie vigezo gani kumkubali au kumkataa? Hata leo akihama kikwete si mtasema makombo?
 
Lakini mbona juzi alihudhuria mkutano mkuu wa Kizota! au na yeye aliiwakilisha Chadema? Hongera Cdm kwa kupokea makombo ya CCM! huyu mbunge uliemtaja wala hana umaarufu wowote! Jee, sumae nae ameshapewa Kadi?

umaarufu upi unaoutaja au kama ana account uswis
 
Nina mashaka makubwa na hawa wadau wa magamba wanao hamia CDM!
Wengi wao wanakuja huku aidha kusaka vyeo au kusaliti.
Chadema kuweni makini.
 
Ok huyu Senyagwa namjua sana aliwahi kua Mgombea wa Jimbo la Kongwa ambapo Job Ndugai ndie aliemnyang'anya hilo jimbo na kimsingi hakuwahi au alikua akiwadharau sana wapiga kura na hivi niongeavyo mpaka sasa anatembea kwa miguu,lakn zaidi namkaribisha CDM saaana
 
kwa kweli si kila kitokacho ccm cha kuchukua wanaweza wakahamia huku CDM na uozo na akili za kiccm wakaua chama CDM.

Kwahiyo mnashauri akina nani ndo waruhusiwe kujiunga chadema? Wanyarwanda? Viongozi wengi wa upinzani waliopo leo wametokea ccm ina maana nao hawaaminiki! Acheni yeyote anayetaka ajiunge cdm kama ni fisadi atatakaswa atakuwa safi muhimu wapewe muda wa kukomaa na kufundishwa uzalendo kwa chama chao kipya kabla ya kupewa uongozi
 
Sisi hatuchukui watu kwa ajili ya status yao kama CCM kwamba lazima uwe maarufu, lazima uwe na mshiko no matter umeupataje, CDM ni chama cha wote, uwe nacho usiwenacho
Lakini mbona juzi alihudhuria mkutano mkuu wa Kizota! au na yeye aliiwakilisha Chadema? Hongera Cdm kwa kupokea makombo ya CCM! huyu mbunge uliemtaja wala hana umaarufu wowote! Jee, sumae nae ameshapewa Kadi?
 
Lakini mbona juzi alihudhuria mkutano mkuu wa Kizota! au na yeye aliiwakilisha Chadema? Hongera Cdm kwa kupokea makombo ya CCM! huyu mbunge uliemtaja wala hana umaarufu wowote! Jee, sumae nae ameshapewa Kadi?

Cha msingi si umaarufu wake, maana kwa kauli hiyo ungetaka sasa CDM wajiunge watu maarufu tu! Lakini ujumbe uko wazi, hata waliowahi kubebwa na CCM mpaka kuingia kwenye bunge kwa tiketi yake, WANAKIHAMA!
 
Lakini mbona juzi alihudhuria mkutano mkuu wa Kizota! au na yeye aliiwakilisha Chadema? Hongera Cdm kwa kupokea makombo ya CCM! huyu mbunge uliemtaja wala hana umaarufu wowote! Jee, sumae nae ameshapewa Kadi?

Inamaana CCM imetutekeleza wananchi kwa sababu sisi sio maarufu au sio?
 
Kwahiyo mnashauri akina nani ndo waruhusiwe kujiunga chadema? Wanyarwanda? Viongozi wengi wa upinzani waliopo leo wametokea ccm ina maana nao hawaaminiki! Acheni yeyote anayetaka ajiunge cdm kama ni fisadi atatakaswa atakuwa safi muhimu wapewe muda wa kukomaa na kufundishwa uzalendo kwa chama chao kipya kabla ya kupewa uongozi

mh sasa watafundishika ? watabadilika? huu ndio wasiwasi wangu.
 
Angeacha ubunge wake wa CCM akajiunga na CDM ningemuona shujaa kweli kweli lakini ameona jina limeshasahaulika amechuja ndio anakimbilia huko kufufua jina lake.
Hata Mangula alikua amechuja lakini karudishwa damu changa bila hekima na mbinu za wazee kama hawa ni vigumu kupenya Dodoma inahitaji wakongwe wenye kuweza kukaa na wapiga kura na kuongea nao taratibu kwani wao hawaelewi haraka na ndio maana bado wapo nyuma kidogo.
 
Chadema mekuwa desperate sana mimi nilijua chama chenu mnataka kujenga na damu changa na watu wenye mawazo mapya kumbe ni recycle bin!

Mtazamo wako sio sahihi hata wazee wanahitajika.......muhimu ni kuwa amejiunga kama mwanachama wa kawaida na hakuna cheo kinatafutwa
 
Back
Top Bottom