Mbunge wa Tunduma(CHADEMA), Frank Mwakajoka amekamatwa kwa tuhuma za kumpiga mtu mwaka 2018

Kuna mambo yanaudhi sana. Kweli kamanda kafanya press kwa hilo!?
 
Tunaomba afikishwe mahakamani maana huko ndiyo kwenye welevu wa sheria
Mbunge wa Tunduma (CHADEMA), Frank Mwakajoka amekamatwa na polisi ikielezwa kuwa atafikishwa mahakamani muda wowote kujibu tuhuma za kumpiga mtu mwaka 2018.

Akizungumza leo Alhamisi Julai 11, 2019 kamanda wa polisi Mkoa wa Songwe, George Kyando amesema mbunge huyo amekamatwa leo na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Amebainisha kuwa Mwakajoka anadaiwa kumpiga mwananchi ambaye hajamtaja jina, kwamba kesi hiyo ni ya muda mrefu
"Kuhusu jina la mtu aliyepigwa hapa sina labda unipe muda ili nilitafute,” amesema kamanda huyo.

Katibu wa Baraza la Vijana la CHADEMA(BAVICHA) Mkoa wa Songwe, Ayub Sikagonamo amedai Mwakajoka amekamatwa kwa madai ya kumpiga ofisa mtendaji wa mtaa, Deus Mwampashe.

Mbunge huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.
 
Hivi yule jamaa aliyepigwa na spika alipona kweli maana alitandikwa bonge la fito
Hahaha labda na Spika Ndugai atakamatwa siku moja kwa makosa kama haya, ngoja waweke precedent.
Rudisheni kumbukumbu zenu, hata kama uluwahi kupigwa ukiwa primary, unaweza shitaki sasa.
 
Mwakajoka Sikukosea Kukupa Kura,moja Kati Ya Kura Ninayo Jivunia Baada Ya Ile Ya Sirinde, Nakuamini Kamanda Na Utashinda Najuwa Ni Hila Ila Kwauwezo Wake Utashinda
 
Mbunge wa CHADEMA akamatwa kwa tuhuma za kumpiga mtu mwaka 2018

Mbunge wa Tunduma (CHADEMA), Frank Mwakajoka amekamatwa na polisi ikielezwa kuwa atafikishwa mahakamani muda wowote kujibu tuhuma za kumpiga mtu mwaka 2018.

Akizungumza Alhamisi Julai 11, 2019 kamanda wa polisi Mkoa wa Songwe, George Kyando amesema mbunge huyo amekamatwa leo na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Amebainisha kuwa Mwakajoka anadaiwa kumpiga mwananchi ambaye hajamtaja jina, kwamba kesi hiyo ni ya muda mrefu
"Kuhusu jina la mtu aliyepigwa hapa sina labda unipe muda ili nilitafute,” amesema kamanda huyo.
 
Kama polisi wanaweza kutunza kumbukumbu na sisi ni zaidi ya kumbukumbu muiteni Ndugai naye alipiga 2015
 
Back
Top Bottom