Mbunge wa Tabora athibitisha udini wa serikali ya CCM

Mbunge wa Tabora athibitisha udini wa serikali ya CCM

Sio kwamba udini haukuwepo ila Marais waliopita hawakuupa nafasi...
Unaweza kufuatilia moja ya thred ambayo ipo katika threds zilizohifadhiwa katika jukwaa hili ya
Mohammed Said na Yericko Nyerere!

Nakubaliana na wewe kuwa "udini" ulikuwepo na kwa taarifa yako udini ni vision ya muda mrefu sana kuhakikisha watu wa dini fulani wanahodhi njia zote za uchumi!

Kuna hoja niliwahi kuileta kwanini watu wa sensa hawataki kuweka kipengele cha dini ukipata nafasi pitia hapa https://www.jamiiforums.com/great-t...ngo-vinavyohusika-na-takwimu.html#post4508300
 
Sibishani na "qwertyuiop" btn ukisoma nilichokiandika utakuwa umeelewa ukigoma kuelewa siwezi kukulazimisha kuelewa. Ila ni upumbavu kujifanya huelewi kitu ambacho kipo wazi.
mfuasi wa ccm anachoweza kukuambia cha kweli ni jina lake tu?
 
yeye alijuaje hao anaodhani ni wakristo ni wakristo kweli! hakumsikia makamba anasema "hakuna anayejua idadi yao maana hakuna anayejiangaisha kujua kuna wakristo au waislam wangapi"

kwa hoja ya rage ni kwamba wapo wengi wanaotengeneza takimwu za kuwapendelea ndo maana hataki kugusa idadi ya waislam walioajiriwa NSSF, kamati ya katiba, igp wakuu wa polis dar na hao wamepaishwa madqraka kipindi jipi[/QUOT watu wenye udini utawaona tu km ww,yaan kwakua NSSF inaongozwa na muislam basi nyooote roho zinawauma,mbona taasisi nyingine nyeti km BOT,TRA hamzizungumzii au kwakua zimeshikiliwa na wakristo??yaan muislam kuongoza kitaasisi kimoja tu cha nssf roho zinawauma mnataman kupasuka!
 
je unakumbuka kuwa raisi alishawahi kuwaita mashehe pale kwake ili kuwashukuru kwa kazi nzuri ya kupiga kampeni misikitini?
nilitegemea majibu rahisi yenye mrengo wa kiimani kuliko wa kitaifa... bullshiiiiiiiiit. jiondoeni katika utumwa wa kiroho nyie wapumbavu
 
kwa nini apendelee ukristo huoni kama yaweza pelekea machafuko zaidi na kuwafanya waislamu waelewe kuwa hii serikali ni ya mfumo kristo kama walivyokuwa wakidai tangu awali?

Mheshimiwa Kapya, hali ilikua mbaya zaidi ya hivyo. Hapo JK yupo katika harakati za kubalance tu ndio kelele zote hizo.
 
Mheshimiwa Kapya, hali ilikua mbaya zaidi ya hivyo. Hapo JK yupo katika harakati za kubalance tu ndio kelele zote hizo.
mzimu mi nafikiri viongozi wa serikali wawe makini na matamko ya kidini?
 
yeye alijuaje hao anaodhani ni wakristo ni wakristo kweli! hakumsikia makamba anasema "hakuna anayejua idadi yao maana hakuna anayejiangaisha kujua kuna wakristo au waislam wangapi"

kwa hoja ya rage ni kwamba wapo wengi wanaotengeneza takimwu za kuwapendelea ndo maana hataki kugusa idadi ya waislam walioajiriwa NSSF, kamati ya katiba, igp wakuu wa polis dar na hao wamepaishwa madqraka kipindi jipi

dr dau wa nssf hakuteuliwa na kikwete bali aliteuliwa kipindi cha mkapa,kuhusu nssf kua na waislam wengi mbona hujahoj TRA kua na wakristo wengi tena wachaga???

Kuhusu kuwapandisha vyeo kina said mwema na kova ambao ndio huwaumiza roho zenu mbona hujahoji kuwateau wakristo wengi zaidi ya 70 % kua makatibu wakuu,mawaziri na manaibu wao pamaoja na wakuuu wa mikoa?
 
I see, nyie watu sio kama mnafanya mambo haya kwa bahati mbaya! mnasukumwa na dhamira za ajabu sana ndani ya mioyo yenu. Kumbukeni kuwa mtoto haimbiwi nyimbo mbaya, jaribuni kutumia akili zenu kutafakari yanayosemwa. Tatizo lenu nyie Chadema hata kama mnanajua ukweli wa kitu, hamkubali kushindwa, hilo tu ndilo linanichukiza, mtu anajua kabisa "udini" maana yake nini lkn atang`ang`aniazia kitu alimradi onekane yuko sawa.

Kuna malalamiko mengi sana yametolewa kuhusu chadema sote mashahidi. Kuna waliosema ni chama cha kikanda zikaletwa hoja kuonyesha huo ni upotofu!
Zikaja hoja za kuwa ni chama cha kikabila zikajibiwa kwa hoja walioleta hoya wakashindwa!
Zikaja hoja kuwa cdm ni chama cha "kidini" wanachadema na wasio kuwa wanachadema wakachangia vizuri na kupambanua kuwa kuna watu kama kina Zitto Kabwe ni waislam wapo cdm na Zitto ni naibu katibu mkuu! Sijasikia hoja zako za mbona na fulani yeye ni mpagani! Kwa hoja yako inaonyesha basi hata hao unaowatetea na wao ni wadini kwasababu wameshindwa kuwachukua na wapagani kuwapa nafasi kwenye chama!

Jamani ifike mahali tuseme basi kwenye hizi habari za kidini, hivi mleta mada hujapata kusoma na ambao ni dini tofauti na wengine wakawa kama n dugu zako? Huna majirani ambao ni dini tofauti na wewe? Kwenye familia yenu hakuna muingiliano wa dini tofauti na uliyonayo? je mwanao na watoto wa ndugu zako wanasoma shule za dini moja? KAtika maisha yako yote hujapata kusaidiwa na mtu asie kuwa wa dini yako?

Wapi tunakwenda?

Kwa hiyo SERIKALI ya CCM inasubiri nini KUIFUTA CHADEMA?!Kwa sababu haifutwi,basi CCM ni wadini ndiyo maana wanahangaika kujua idadi ya Wakristo na Waislamu katika nyanja mbalimbali nchini!Itaenda hadi kwenye timu ya taifa,
na huk sijui itakuwaje maana wachezaji lazima wawe 11-nani atakubai kupunjwa?!UDINI siyo IDADI ya watu kwenye sekta fulani...UDINI ni kuwa na fikra kwamba huyu anastahili/hastahii kitu kwa sababu ya dini yake!Itakuwaje kwenye shule za serikali ambazo hakuna walimu wa dini fulani,hospitali ambako hakuna wataalamu wa dini fulani,au vyombo vya usafiri visivyomilikiwa na watu fulani?!Je,KUNA HAJA YA TAASISI KUFANYA AFFIRMATIVE ACTIONS eti kwa ajili ya kuepuka kudhaniwa udini?!TUPE UDINI WA CHADEMA ndg yetu!
 
asante kaka na walikemea sana lakini now..............
Sio kwamba udini haukuwepo ila Marais waliopita hawakuupa nafasi...
Unaweza kufuatilia moja ya thred ambayo ipo katika threds zilizohifadhiwa katika jukwaa hili ya
Mohammed Said na Yericko Nyerere!
 
Unajua watu wengi wana.define udini kwa namna isiyo ya ukweli. Mmojawapo ni huyu Rage. Yeye anafikiri kwa rais muisilamu kuteua wakristu wengi ndio ishara ya kutokuwapo udini. Mimi nasema, kama kweli JK aliwateua wakristu ili aonekane hajapendelea waisilamu (kama alivyoashiria Rage), basi huo ndio udini. Mwalimu Nyerere aliongea vizuri sana kuhusu udini. Alisema "Hatutamchagua mtu kwa sababu ya dini yake, wala hatutamkataa mtu kwa sababu ya dini yake". Bila ya kujali ni wa dini yako au asiye wa dini yako, kama unazingatia dini ya mtu katika kumchagua au kumteua, huo ndio udini. Kwa hiyo, kama JK aliwateua mawaziri kwa kuangalia huyu ni dini gani, hata kama aliowateua sio wa dini yake, huo ni udini

Excellent contribution! Udini ni religious favoritism regardless of the religious affiliation of either party. Ila sitegemei kama Mh. Rais wetu anateuwa watendaji kwa kigezo hicho. Ni mawenge tu ya Rage akidhani anamtetea Rais na CCM kumbe anazidi kuwaharibia.
 
Unajua watu wengi wana.define udini kwa namna isiyo ya ukweli. Mmojawapo ni huyu Rage. Yeye anafikiri kwa rais muisilamu kuteua wakristu wengi ndio ishara ya kutokuwapo udini. Mimi nasema, kama kweli JK aliwateua wakristu ili aonekane hajapendelea waisilamu (kama alivyoashiria Rage), basi huo ndio udini. Mwalimu Nyerere aliongea vizuri sana kuhusu udini. Alisema "Hatutamchagua mtu kwa sababu ya dini yake, wala hatutamkataa mtu kwa sababu ya dini yake". Bila ya kujali ni wa dini yako au asiye wa dini yako, kama unazingatia dini ya mtu katika kumchagua au kumteua, huo ndio udini. Kwa hiyo, kama JK aliwateua mawaziri kwa kuangalia huyu ni dini gani, hata kama aliowateua sio wa dini yake, huo ni udini

Wote mmechemsha!!!!!! Hakuna dini tatu Tanzania. Kuna dini nyingi sana siyo ukristo, upagani ama uislamu tu.......Hapo na ninyi mmekuwa wabaguzi..........Mnabagua uhindi, ubohora, ubudha na nyinginezo nyingi tu....
 
dr dau wa nssf hakuteuliwa na kikwete bali aliteuliwa kipindi cha mkapa,kuhusu nssf kua na waislam wengi mbona hujahoj TRA kua na wakristo wengi tena wachaga???

Kuhusu kuwapandisha vyeo kina said mwema na kova ambao ndio huwaumiza roho zenu mbona hujahoji kuwateau wakristo wengi zaidi ya 70 % kua makatibu wakuu,mawaziri na manaibu wao pamaoja na wakuuu wa mikoa?

Very good mkuu!!!!
 
Hivi juni unapata faida gani kueneza chuki za kidini? kwenye ile thread yako ambayo uliandika maneno ya uongo kutimiza matakwa yako nilijaribu kukuweka sawa kuwa uliyoyasema hayakuwa ya kweli na ulipindisha ukweli kwa faida yako na ya waliokutuma.

Nina amini unafanya hivi sio kwa bahati mbaya kuna watu nyuma wanachochea haya mambo na "pengine" kuna malipo makubwa mnayapata au kuyategemea kwa kazi hii ovu!

Unasema NSSF hivi wewe unajua miaka ya mwanzo ya uhuru mji huu watumishi wote wa ngazi ya chini "madereva na wahudumu/messengers" walikuwa ni wenyeji wa pwani na dar es salaam? ambao majority walikuwa ni waislam! Umefanya takwimu sahihi ukaona kuna Wachagga wangapi TRA?kabla ya kuigusa NSSF? Hivi unadhani watu wakikaa kimya hawajui kinachoendelea? Acheni chuki za kijinga ambazo hazina maana yoyote kwa taifa hili. Jipangeni vizuri kwa hoja zenye tija kwa taifa sio hoja za kufarakana!

Aliyoyasema Rage yana ukweli kabisa kuwa kumepita awamu nne hakukuwa na maneno ya "udini" naanza kumwamini kuwa "udini" umeletwa na waliongia kwenye siasa hivi karibuni kwa maana nakumbuka marafiki zangu wengi niliosoma nao walikuwa dini tofouti na mimi na mpaka sasa nawaona kama family members wangu hatujawahi kubaguana kwa sababu wao wana dini tofauti na mimi.

Hii kitu ipo kwenye peak kuna mwandishi wenu mmoja wa habari ni mdini kupindukia naisubiri makala yake kwa hamu na tamu.

Badala ya kujadili mambo ya utaifa mnajadili m maswala ya dini ama kweli tuna safari ndefu sana.

Mohamed, mimi siliangalii suala la udini kwenye appointments japo ukiangaliwa kwa makini unaweza ukaona msukumo wa dini. Nashauri kuwe na vetting kwenye appointment za raisi kama inavyofanyika Kenya, ili tuone kuwa meritocracy inatawala kwenye appointment. Sio kupeana vyeo kwa sababu ya udini au urafiki au ukabila. Unajua Kenya wana tatizo la ukabila sana, ila hawana tatizo la udini. Ukiwa na uwezo wa kufanya mambo, unachaguliwa. Ndio mana Muhamed Dida hakupata kura nyingi hata maeneo yenye waislamu wengi kama vile Grasisa na Mombasa. Vilevile, kuna mbonge wa ODM kutoka Kisumu ambaye ana asili ya Kisomali na ni muislamu. Ila suala kubwa linalohatarisha usalama wa nchi lilianza kwenye kampeni za uraisi mwaka 2005 na 2010, ndio mana serekali hii inahusishwa na uasisi wa udini nchini. Kwa sababu tuliona kipindi Prof. Lipumba akiwa na nguvu, CUF ikihusishwa na udini, na Dr. Slaa alipogombea uraisi CHADEMA kikahusishwa na dini. Kwenye hotuba ya Dr. Slaa akiwa nadhani Mbulu, alitoa mfano wa kumteua mwalimu wa Kiislamu katika shule ya dini ya kikatoliki. Lakini pia Dr. Slaa amekuwa mbunge na wakati huo hakuitwa kwa kazi yake aliyokuwa anafanya mwanzo.
Lisiposhughulikiwa kwa dhati, tunaweza kuingia kwenye machafuko. Kuuawa kwa Padri kule Zanzibar, na vitisho dhidi ya wakristo Zanzibar sio ishara nzuri. Suala la kumwagiwa tindikali kwa mmoja wa viongozi wa kiislamu kule Zanzibar nadhani linahusisha watu wa jumuia za kiislamu. Mimi naishi Zanzibar, vijana wengi hawana kazi, wanaangalia CD za kutukana ukristo na CHADEMA kuanzia asubuhi mpaka jioni. Nimeangalia CD hizi nyingi sio kuwa zimerekodiwa ndani ya msikiti, nyingi ni kwenye mihadhara, na serekali inajua hilo. Nadhani imekaa kimya kwa sababu kwanza katika kampeni iliwaahidi waislamu mambo ambayo isingeweza kuyatimiza kwa haraka. Ndnio maana baada ya uchaguzi, miaka ya 2011-2012 tulisikia mengi kuhusu mfumo Kristo. Huu umekuwa msamiati kwangu na kwa watu wengi, lakini mpaka mwaka jana Dr. Slaa alipouonyesha huo mkataba kati ya jumuia ya maaskofu na serekali na watu kuona kuwa hakuna flow of money kutoka serekalini kwenda kwenye jumuia hiyo, ndipo wakakaa kimya. Yalikuwa yanahubiriwa mambo kuwa jumuia ya kikristo inapate pesa nyingi kutoka serekalini, serekali haikutoa hata tamko la kupinga au kukubali, which means walitaka maneno hayo yaendelee kusambazwa. Serekali inajua vitisho vya taasisi za kiislamu dhidi ya viongozi wa kikristo Zanzibar, lakini hata tamko tu serekali haijawahi kutoa.
Namuunga mkono Zito Kabwe anapotoa tahadhari ya kuwa makini kwenye kushughulikia matatizo ya kidini kwa sababu imani wakati mwingine inaweza ikawa kubwa mpaka mtu akaiweka akili yake na ubinadamu wake pembeni. Ndio maana kila leo huko Iraq na Pakistani wanauana, tena hawa ni waislamu kwa waislamu, tofauti ni dhehebu Shia na Suni. Huko Nigeria watu karibia 1000 kwa miaka mitatu tu wameuawa kwa sababu za kidini tu. Kwa hiyo, kuna haja ya kulishughulikia hili. Nashauri, suala la kidini lisiongelewe bungeni bali kie alichokipendekeza waziri mkuu ndicho kifanyiwe kazi. Bunge letu limegawanyika, hata wapinzani wakitoa pointi ya maana bado ccm itaibeza, na hata serekali itatoa pendekezo la maana, wapinzani wataibeza. Na hili ni tatizo lililoanzishwa na spika wa kupendelea na kuruhusu vijembe bungeni. Kwa hiyo kuruhusu suala la dini liongelewe bungeni kunaweza kukafanya hatred kati ya dini moja na nyingine iwe kubwa.
 
wana jf
Katika kuchangia na kujibu hoja za chama pinzani bungeni, mbunge wa Tabora Mjini bw. Aden Rage,alijikuta akitumbukia kwenye uthibitisho wa udini huku akiashiria kupinga ilihali kimsingi anatoa ushahidi unaoonesha upendeleo wa udini.

Hali hiyo ilikuja baada ya kutoa takwimu za mtiririko wa watendaji wakuu wa serikali kama vile wakuu wa mikoa,wakurugenzi na kuonesha kuwa rais aliteua viongozi katika dini mbili tu yaani ukristu na uislamu huku akisahau dini ya upagani wakati kila siku serikali inahubiri kuwa nchi haina dini ila inatambua uwepo wa dini za aina 3 (ukristu,uislam na pagani).

Swali ni je Rage haoni kama anamfunga mwajiri wake kwa kutoa takwimu zinazoonesha wakristu kuwa wengi katika serikali hii na kuwasahau wapagani,achilia mbali kuwa alitoa takwimu za uongo?

Hivi upagani ni dini??
 
Hoja za udini hazijengi nchi wakuu, hebu tufikire taifa lina matatizo gani ya msingi ambayo yanahitaji mawazo yetu sisi ili kupata majawabu, Tuwaze juu ya elimu yetu amabayo hata mpaka sasa hata wanafunzi wa kijiunga na A-level bado ni kitendawili yaani hakuna wenye sifa za kutosha, Tuwaze juu ya tatizo sugu la ufisadi nchini etc, Hivi kweli leo hii udini ndio umekuwa kipaumbele chetu?

Mimi ni mkristo ninayetokea ktk jamii yenye dini tofauti lakin sipendezwi na badhi ya michango ya wakristo na waislamu humu JF yaani tumepigwa upofu na Shetani na sasa tumeacha agenda kuu yani tumegeukiana sisi kawa sisi. Dah......!

Nchi yangu eeeh.......!
 
CCM ni waasisi wa udini, CHADEMA wanaumwagilia maji na kuuwekea rutuba ili unawiri.
 
Homeboy Kapya,

Shossi ni Mbishi sana na pia ni Mweupe mno kichwani. Soma PM.
 
Back
Top Bottom