Mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM) avuliwa ubunge na mahakama!

Sheria zetu sio kali ki hivyo, alitakiwa avuliwe kila kitu (nguo included) sasa wao sheria inakoma kwenye ubunge tu.

Pia lazima angepewa kifungo kwa kosa la rushwa. Lema walidai alitukana na pia haikuthibitishwa beyond reasonable doubts kuwa alitenda kosa hilo.

Lakini huyu jamaa ushahidi wa rushwa uko nje nje so kwa nini hakufunguliwa kesi ya papo kwa papo na akapata adhabu fasta?

Hon. Judge I'm not entirely happy with your verdict.
 
kama mahakama imedhibitisha kuwa amepokea rushwa nitashangaa tena kama hatafunguliwa kesi nyingine ya kosa la kutoa rushwa. Pccb haihitaji kuumiza kichwa tena hapo, kwani ushahidi upo. Kazi ni kufungua tu file la kosa la rushwa.
 
Hatimaye kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo la sumbawanga mjini imetolewa na kuonekana kuwa ushindi wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia ccm haukuwa huru na haki.Hii ni kutokana na ushahidi kuthibitisha pasi na shaka kuwa mgombea wa chama cha mapinduzi alitumia rushwa katika kushawishi wananchi kumpigia kura.Lakini pia kulikuwa na tetesi kuwa hata utangazaji wa matokeo uligubikwa na utata mkubwa na unaonekana uliingiliwa na watu wenye mamlaka za juu kitaifa. Mahakama ya hapa mjini imetoa maamuzi kuwa aeshy Hilary siyo mbuge halali na hivyo uchaguzi urudiwe upya. Je maamuzi haya yaweza kuwa ndio usahihi wa maamuzi ya mahakma zetu nchi tanzania?
 
Hata hivyo mheshimiwa huyo ana kashafa nyingi machoni pa watanzania ikiwemo ya kupenda mabinti wadogo.Pia anadaiwa shule ilimshinda form 2 baada ya kufukuzwa shule na mwl Yamsebo (mgombea wa CHADEMA).Kwa hali hii angeongoza vipi Sumbawanga?
 
Wakuu leo ndiyo kunatolew hukumu ya kupinga matokeo ya ubunge wa sumbawanga mjini wa Aeshy Hilaly Halphany CCM dhidi ya mwalimu Norbet Joseph Yamsebo wa Chadema ambaye anadai kuchakachuliwa katika uchaguzi huo.

Madai miongoni ni pamoja na kutoa rushwa kwa makundi mbalimbali na watu wengi walijitokeza kutoa ushahidi huo na kukiri kuwa ni kweli walipokea vitu mbalimbali ikiwemo fedha, baskeli, pikipiki, vinywaji, kinanda kwa kanisa katoliki, nk kwa sharti la kumpigia kura mbaya zaidi ni kwa mkurugenzi mwanamama kutoa ushahidi wa kupinga ushindi wa mbunge huyo, mkurugenzi huyo alihamishwa muda mfupi mara baada ya matokeo ya uchaguzi kutolewa na kupelekwa wilaya ya Ileje.

Moja ya kituko katika kesi hii mara baada ya mbunge huyo kuulizwa kama anaamini na kusema hajui kama alishinda ila mkurugenzi ndiye anayejua ushindi huo, kimsingi ulinzi umeimalishwa kwani yaweza kuwa mbaya endapo Aeshy atatangazwa mshindi, askali wapo wa kutosha, washawasha na mabomu, lakini kesi hii ilikosa umaarufu kwa kuwa waandishi njaa wote walikuwa upande wa Aeshy mpaka ripota wa ITV Joshua joel update tutawaletea mara kesi itakapoanza....

Kamanda Doma.

UPDATES:
Umati umejitokeza kwa wingi sana na watu wamejaa ndani hivyo imebidi spika zifungwe nje lakini gari la polisi limekuwa likizunguka kuonya juu ya uvunjifu wowote wa amani.

Muda mfupi ujao jaji ataingia ila naona makamanda wengi sana kutoka sehemu mbalimbali wakiwa ndani ya magwanda

Jaji ameingia na kuanza kusoma kesi kwa lugha ya kiingereza na kesi nzima ina takribani kurasa 68

Mawakili wanaendelea kutoa utetezi wao wa mwisho lakini umati uliopo unatisha na Licha yakuonekana wafuasi wengi ni wa Chadema lakini Askari wameondolewa na kuashiria uwezekano wa chadema kushinda kesi.

Hoja za mwisho zinaweza kuwabana Magamba lakini naona Polisi wameanza kumwagika
UPDATES
mashabikina wafuasi wa Chadema wanashangilia nje ya mahakama kwa mbwembwe japo jaji bado hajatoa tamko
UPDATES
HATIMAYE CHADEMA WAIBUKA NA USHINDI NA UCHAGUZI KUTANGAZWA KURUDIWA UPYA BAADA YA BWANA AESHY KUKUTA NA KOSA LA KUTOA RUSHWA KATIKA UCHAGUZI HUO. Chademaaaaaaaaaaaaaaaaa vemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Chadema

Hatimaye kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo la sumbawanga mjini imetolewa na kuonekana kuwa ushindi wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia ccm haukuwa huru na haki.Hii ni kutokana na ushahidi kuthibitisha pasi na shaka kuwa mgombea wa chama cha mapinduzi alitumia rushwa katika kushawishi wananchi kumpigia kura.Lakini pia kulikuwa na tetesi kuwa hata utangazaji wa matokeo uligubikwa na utata mkubwa na unaonekana uliingiliwa na watu wenye mamlaka za juu kitaifa. Mahakama ya hapa mjini imetoa maamuzi kuwa aeshy Hilary siyo mbuge halali na hivyo uchaguzi urudiwe upya. Je maamuzi haya yaweza kuwa ndio usahihi wa maamuzi ya mahakma zetu nchi tanzania?

Jibu lake ni ndiyo maana mahakama imejiridhirisha pasipo na mashaka kuwa mbunge aliyekuwepo madarakani aliingiia kwa rushwa, ghilba n.k

Viongozi wa namna hiyo siyo machaguo ya wananchi, hawatufai.
 
Hiyo ni Ishara kuwa haki siku zote ina nguvu kuliko madaraka na pesa. hakuna awezaye kushindana na nguvu ya umma
 
kama mahakama imedhibitisha kuwa amepokea rushwa nitashangaa tena kama hatafunguliwa kesi nyingine ya kosa la kutoa rushwa. Pccb haihitaji kuumiza kichwa tena hapo, kwani ushahidi upo. Kazi ni kufungua tu file la kosa la rushwa.

Wananchi wengi ni watumwa wa kukoseshwa haki zao ili ukombozi na uhuru wa kweli hauko mbali....Mungu asante kwa kuonesha uovu ulikojificha.NA BADO TENA BADO SANA .Hii ni cha mtoto ,nasema bado wapo wengi wa style hii ya sumbawanga mjini..
 
Naipongeza Idara ya Mahakama kwa kusoma alama za nyakati. Bado ile Tume inayotangaza kile ambacho Mgombea hakuvuna.
 
Wanasema Chungu lakini Dawa.....katika maisha ya Binadamu katika nyakati ngumu kuliko zote ni kukubali matokeo.Bottom line.....kila ngoma ina mdundo wake!
Go CDM, Mahanga here we come.....Presha Inapanda Presha Inashuka!
 
kama mahakama imedhibitisha kuwa amepokea rushwa nitashangaa tena kama hatafunguliwa kesi nyingine ya kosa la kutoa rushwa. Pccb haihitaji kuumiza kichwa tena hapo, kwani ushahidi upo. Kazi ni kufungua tu file la kosa la rushwa.

Kama mawaziri(ndani ya Serikali ya ccm)wameachwa mpaka sasa hivi wanatanua kwa raha zao,vipi kwa mbunge wa ccm mkuu?Sahau kuhusu hilo
 
Sijajua vigezo lakini nasikia ni pale Ribosome alipolalamika eti Molemo kamuita FF
binafsi ritz keshanisababishia ban tatu, ya mwisho ya miezi mitatu ndiyo imeisha juzi juzi...ritz and co wanafanya kamchezo ka ku provoke watu na uki retaliate kwa lugha kali kidogo ujue unapigwa dude.. nadhani wana mod/s wao ambaye yuko standby kwa shughuli hiyo...wacha watupige ban kwa sasa lakini ipo siku tutapata vyanzo vingine vya habari za kuaminika zaidi ya jf...!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom