Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ajivua Ubunge; ajitoa CCM na kuomba kujiunga CHADEMA

Chama na nchi vimekabidhiwa kwa mwendawazimu ambaye ameleta hofu na taharuki nchi nzima ikiwemo ndani ya chama. Kama asipokabiliwa mapema huyu basi ataleta athari kubwa sana nchini kwa maamuzi yaliyojaa chuki kubwa, undumilakuwili, ukurupukaji, kudharau sheria za nchi, katiba na Bunge.
Ujumbe wako unaheshimika,lakini nikuombe utumie lugha au maneno malaini kufikisha ujumbe wako.
 
NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017.

HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.

AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA.

VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndio chimbuko la Uongozi Bora wa nchi, na kuonesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yatokana na wananchi wenyewe, na kwamba Serikali ni ya Watu kwajili ya Watu.

MIMI Naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA, kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali. AIDHA, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.

HIVYOBASI, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya KIKATIBA, natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM leo hii, na nitaomba IKIWAPENDEZA wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, basi waniruhusu kuingia MALANGONI mwao, niwe mwanachama, ili kuungana na CHADEMA na watanzania wote wanaopenda kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini kwa kupitia mfumo wa ki demokrasia na uhuru wa mawazo.

VILEVILE, nimemua kujiuzulu KITI Cha Ubunge, Jimbo la Singida Kaskazini kuruhusu kufanyika kwa UCHAGUZI mwingine ili wananchi wapate fursa ya kuchagua ITIKADI wanayoona inawafaa kwa majira na nyakati hizi zenye changamoto lukuki nchini Tanzania. Ni imani yangu, kamwe hayatakuwa ya bure maneno haya, wala uamuzi huu niufanyao mbele ya Watanzania leo ili kwamba, SOTE kama TAIFA tuingie kwenye mjadala wa kuijenga upya misingi ya nchi yetu. Ni maombi yangu kwa MUNGU kuwa Haki itamalaki Tanzania. Upendo, amani na mshikamano wa watu wa imani zote za dini, mitazamo yote ya kiitikadi za Kisiasa, na makabila yote nchini uimarike. Tushindane ki sera na kuruhusu tofauti za mawazo, lakini tubaki kama ndugu, na TAIFA lililo imara na nchi yenye ADILI.

[HASHTAG]#MunguIbarikiTanzania[/HASHTAG].
Lazaro S. Nyalandu.
 
65c2a434f978ec2ea8adfe3fa6e64af0.jpg

5f1599dbb7adbbe34505726511b2a0d8.jpg
 
Ngoja nisikilize muziki wa Vieux Papa Simaro "Masiya" Lutumba kwani leo mapovu yatatoka kila upande. Bakizeni maneno lakini ili mhifadhi ujiniasi wenu-kuna leo na kesho kila upande utafakari pamoja na wale wenzangu mie wasiokuwa na chama. Nyalandu uwe tayari kupigwa mawe-huko unakotoka na huko uendako pia kwani utagusa matarajio ya watu wa kila upande.
 
CCM wamenunua madiwani wangapi vile ila CHADEMA wamewakomesha wao wanaondoka na wabunge haaaa sipati picha polepole atakavyokuwa anakwenda kasi leo mpaka tutamwita kasikasi.Sasa itabidi Nyalandu Nissan nyeupe inakuhusu kaka na kuanza kufuatiliwa mali zako.CHADEMA walishazoea jamani
 
Imetoka mbunge Lazaro nyalandu kujiuzulu sasa inabidi kabla ya kupokelewa chadema tujiulize maswali haya:

1. Kahama kwa moyo wote?

2. Je sababu aliyosema ya kuacha ubunge na kutaka kujiunga na wengine walioko CCM wanaona sio sababu ya msingine?

3. kwa nini aende chadema na sio chama kingine?

4. Je, nguvu itaongezeka CHADEMA kiasi gani?

5. kuna viongozi wanasema uchumi wa nchi unakua vizuri wakati wapinzani wanasema uchumi umeyumba na watu hawana hela, Je wanasema kulinda nafasi zao tu au.

6. Kama nyalandu kaweza kuacha ubunge na kuomba kujiunga na chadema, Je hakuna viongozi wa serikali wengine wanatamani kujiunga na Upinzani?

Hii ni video ikionyesha Lazaro nyalandu alipokuwa akitangaza kujiuzulu ubunge na kuomba kujiunga na Chadema



Tuongezee swali hapo chini kama unalo.
 
Nashangaa ooo nashangaa mimi nashangaa?hapana,hata yule wa maliasili na utalii anaelekea hukohuko jalalani.Kitu kikishaoza lazima kiende jalalani,sio kiwandani.Anasifa gani?Maliasili na utalii ilikuwaje alipokuwa yeye?kwa nini maunga alihama?aligundua mapungufu ya ccm?mbona wamechelewa kugundua?au mrija ukishakatwa unajitambua?Mbona wanapotoka kama huyu maunga hasemi siri za ndani za huku ccm?au anakuwa amekuja kuchafua huku kusiwe na msimamo?Sielewi na sema sielewi!kwa nn akitoka asiende ACT?au kwa vile mgombea uraisi wa kule ni mpenda dezo na dili wanakimbilia kule ili watuuze ikitokea miujiza wakishika Dola?
na mwigulu akiondoka siku hio usisahau kuja kuhorojoa..wanyaturu sio wajinga kama nyie
 
Chadema walivyo vilaza watampa nafasi yakugombea urais2020
Vipi mkapa akihama?? Mtakumbushia Yale makoleo ya dhahabu ??? Ila sahivi fresh hana noma huko alipo kwenu???
Kaa ijitafakari kat yenu na chadema kilaza ni nani??

Pia VIP kuhusu Jk ,akihama utasema aliuza nchi kwa shi ji mping na riz kuachiwa??
Ila sahiv fresh hawana kosa mkuu kwasababu hawajahama!!!!

Mwinyi vipi?? Akihama mtasema aliuza mbuga ya wanyama kwa waarabu miaka 99 .Hivyo mnamshughulikia na mnatengeneza chama kipya!!!

Sasa ndo ujue kumtafuta msafi ccm,ni sawa na kuipata bikra leba.....

Akili zenu ccm zimejaa maviii..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom