Mbunge wa Mtwara mjini asema Serikali kama ilipeleka Vifaru Mtwara ili gesi itoke, basi ipeleke Vifaru hivyo Ngorongoro kuwaondoa Wamasai!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,957
141,944
Mbunge wa Mtwara mjini amesema wamasai 110,000 wanaoishi Ngorongoro waondolewe na kulipwa fidia ili kulinda hifadhi kwa sababu Ngorongoro siyo mali ya Wamasai pekee bali ni ya taifa zima kama ilivyo gesi ya Mtwara.

Mbunge huyo amesema ng'ombe walioko Ngorongoro ni mali ya matajiri wanaoishi Arusha wala siyo wanavijiji wa Ngorongoro.

Kama gesi ilitoka ikapelekwa Kinyerezi Dar es salaam basi na Wamasai ni lazima waondoke Ngorongoro amesema mbunge huyo.

Source: TBC
 
Daahh sema mamb mengine ni vzr kushauri hasa kwa kutotumia mihemko ya kisiasa na kujipendekeza! Kutumia nguvu sio uongoz bora. Ni vyema itumike busara na kutoa elimu kwa wahusika!!
Nadhani wamekuwa wanashauriwa kwa busara sana sasa wamejiona wao ndio was maana it's time to act now or never.

Ni zaidi ya miaka 10 wanabembelezwa tu yaani wao akina Nani nchi hii ya wote bana .
 
TBC ndiyo wametoa habari hii? Hivi wanaelewa wanachokifanya? Hii habari ukiiangalia kqa jicho la tatu inahatarisha mstakabali wa umoja wa kitaifa!!! Huuo mbunge adhibiti kauli zake na TBC wachuje cha kutulisha watazamaji!

Isiwe kama Channel ten inayorusha miziki mchana kweupe ya wakati mwingine kufunika uso ukiwa karibu na watu wa kupewa heshima
 
Daahh sema mamb mengine ni vzr kushauri hasa kwa kutotumia mihemko ya kisiasa na kujipendekeza! Kutumia nguvu sio uongoz bora. Ni vyema itumike busara na kutoa elimu kwa wahusika!!
Kwahy mtwara ilipopelekewa vikosi vya jwtz na vifaru,sakata la gesi ilikuwa busara,au wakati wa kununua korosho walizolima wa nguvu zao nayo ilikuwa busara?
 
TBC ndiyo wametoa habari hii? Hivi wanaelewa wanachokifanya? Hii habari ukiiangalia kqa jicho la tatu inahatarisha mstakabali wa umoja wa kitaifa!!! Huuo mbunge adhibiti kauli zake na TBC wachuje cha kutulisha watazamaji!

Isiwe kama Channel ten inayorusha miziki mchana kweupe ya wakati mwingine kufunika uso ukiwa karibu na watu wa kupewa heshima
Huyu mbunge anatoka ccm ?
 
Back
Top Bottom