Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (CHADEMA) kuhamia NCCR-Mageuzi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,703
218,237
Mbunge wa Moshi Vijijini Kupitia Chama  Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), A ( 347 X 640 ).jpg

Mbunge wa Moshi Vijijini (CHADEMA) Anthony Komu amesema kipindi chake kitakapomalizika, ataondoka katika Chama hicho na kugombea Ubunge kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi

Mbunge huyo amesema CHADEMA imejaa tuhuma za ndani ya Chama na imepoteza mwelekeo wa kuwapigania Wananchi

Amesisitiza kuwa bado hajaondoka CHADEMA ataendelea kuwatumikia Wananchi wa Moshi Vijijini kwasababu walimpa heshima ya kuwaongoza

Komu amesema atajiunga NCCR-Mageuzi Uchaguzi Mkuu 2020 utakapofika. Ameahidi kuwa hatogombea tena Ubunge katika Jimbo hilo


My Take;
Kumekuwa na tetesi za muda mrefu kwamba Wanaohamia NCCR ni kama wameweka kituo cha muda mfupi kabla ya kwenda CCM ambaye ndiye mlipaji mkuu

Tunamtakia kila la heri kwenye maisha yake mapya huko aendako

...............................

Ombi : Chadema isimfukuze uanachama ndugu Komu , imuache ajikaange kwa mafuta yake mwenyewe .

=====

Zaidi...


Dar es Salaam. Mbunge wa Moshi Vijijini(Chadema), Anthony Komu ametangaza rasmi kujivua uanachama kwa sababu ya kukatishwa tamaa na tuhuma za usaliti zinazomkabili kwa muda mrefu.

Hata hivyo, amesena ataondoka rasmi baada ya kumaliza muda wake wa ubunge kwa kuwa bado atahitaji ushirikiano wa chama hicho jimboni kabla ya kumaliza muda wake.
Akizungumza na wanahabari leo Machi 29,2020 jijini Dar es salaam, Komu amesema amechukua uamuzi huo baada ya kusikitishwa na uongozi wa chama hicho kutosahihisha au kufafanua tuhuma za usaliti zilizosababisha mbengu ya chuki kukomaa ndani ya chama.

"Nimeomba kukutana nanyi(wanahabari) ili kuweka bayana mwelekeo wangu wa kisiasa, kwa sababu ya mijadala ya muda mrefu juu ya mwelekeo wangu wa baadaye," amesema Komu.

Komu anakuwa mbunge wa tisa kati ya 35 waliojivua uanachama kwa madai mbalimbali ya kukosekana kwa demokrasia ndani ya chama au kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli.

Licha ya kukiri kutofautiana na viongozi wenzake, lakini tofauti za kimitazamo zimemfanya aonekane muasi.
"Hatua hiyo ilisababisha kutoaminika hata pale ambapo ningeweza kutoa mchango wangu katika ujenzi wa chama chetu," amesema Komu aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Fedha wa Chadema.

Komu ametaja baadhi ya visa na tuhuma za usaliti alizokutana nazo licha ya kuwa mstari wa mbele katika hatua na matukio mbalimbali yaliyokijenga chama hicho hadi sasa.
Baadhi ya madai aliyoshambuliwa na wanachama wenzake ni pamoja na kupanga njama za kumuua Tundu Lissu, kwa kushirikiana na mtanzania aliyempokea Ubelgiji kwa matibabu.

Katika hotuba yake iliyotanguliwa na tahadhali za maambukizi ya virusi vya corona(COVID 19) nchini, Komu ameeleza namna alivyoshiriki kujenga mfumo wa siasa za vyama vingi nchini, akiimarisha upinzani kupitia NCCR Mageuzi kabla ya kuhamia Chadema.

"Msimamo huu naomba upokelewe kwa mtazamo chanya Chadema, utasaidia kuondoa majungu yanayoendelea, eti nataka nihakikishiwe kurudi nafasi ya ukurugenzi wa fedha, kurudi jimboni, eti kupindua nafasi ya mwenyekiti wetu," amesema Komu.
 
Erythrocyte, Amesha chota zile Mbatia alizo ahidiwa ili kusimamisha wagombea nchi nzima. Katoa mlolongo wa historia yake ambayo sijaona hata impact yake kwa jamii. Huyu ndie atabaki kuwa historia.

Hawa wana siasa sijui kama huwa wana fikiria vyema. Wanadhani kuhama chama wamehama na wale walio mpa kura. Kumbe kahama yeye na mke wake maana hata watoto wana uhuru wao wanaweza wasihame nae.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aamua kujistaafisha ubunge , na kwamba hatogombea tena uchaguzi ujao .

Kumekuwa na tetesi za muda mrefu kwamba Wanaohamia NCCR ni kama wameweka kituo cha muda mfupi kabla ya kwenda ccm ambaye ndiye mlipaji mkuu .

Tunamtakia kila la heri kwenye maisha yake mapya huko aendako
Na wewe utahama lini au unasubiri hadi saccos ifirisike?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom