Mbunge wa Kyela, Dr. Harison Mwakyembe aifunga radio ya jamii ya mpinzani wake kisiasa

Mkuu wangu,
Kyela FM ni redio ya jamii na imelipa malipo yote TCRA. Kwahiyo maelezo yako hapa chini hayatuhusu.

Pitia sheria za TCRA ili kujiridhisha.
Mkuu unejitengenezea mwenyewe safari ya kwenda kushitakiwa mahakamani!
Nijuavyo mimi kila kituo chenye leseni na kinafanya biashara na matangazo hulipia $3,070 kila mwaka TCRA.
Sasa sijui huko Mbeya vipi, lakini kwa kiaka saba utadaiwa $21,490.
Uhuru FM nao wanadaiwa zaidi ya $50,000 kulingana na vyombo vya habari.

Ujinga si kinga.
 
Mbunge Harrison G. Mwakyembe ana chuki binafsi yule mzee ila yote watu wa kyela wanayajua jamaa ana influence sana kwenye utawala sasa udikteta wake anauleta mpaka kwenye jamii yake badala ya kuisaidia ana poka mamlaka ya kutangaza habari. hivi mwkyembe tukuweke kundi gani? huu ni usengerema sijaukubali hata kidog nchi haiendeshwi kwa namna ya chuki binafskama unavyofanya kyela yenyewe hujaifanyia kitu bado chukki juu we mtu wa aina gani? WASHAURI WAKO WANAKUPONZA
 
Acha mapovu kijana, unaobishana nao wengine ni wamiliki wa hizo FM.
Sasa wewe mpiga domo vijiweni umepewa somo hapa lakini unabisha kama lumpen.

Kuwa mbishi just for its sake si U-great thinker.

Kumiliki FM hakukuondoi ujinga na hasa kama kuna mapungufu ya kuzaliwa nayo. Jieleze sasa, TCRA wana mamlaka ya kufungia redio iliyosajiliwa kisheria? Hiyo sheria umewahi kuisoma? Ulikuwa ukifahamu kwamba ipo au nimekustua?

Nabisha kama lumpen? What? kwani lumpen ni mbishi? au ana mtindo wake wa ubishi? Hilo neno ulilisikia wapi? kwa mjomba aliyemaliza la nane la zamani? :A S shade:

Here is the dictionary definition;
Oforrelatingtodispossessed,often displaced peoplewho havebeen cutofffromthesocioeconomicclasswithwhich they would ordinarily be identified:
 
Hii ni kutoka facebook ambako mjadala pia unaendelea, (Copied)

Nimetoka mamlaka husika muda huu kuulizia suala hili la kufungiwa Kyela FM. Nimepewa majibu yafuatayo:-

1. Kuna onyo Kyela Fm walipewa kwa mdomo siku ya tarehe 25 waligoma hawakutekeleza. Waliambiwa waache kurusha vipindi isipokuwa wapige mziki wakagoma.
2. Kyela fm wanakiburi kwa kukaidi hilo agizo. Kukataa kupokea barua ya serikali ni kosa lingine walijiongezea jana. ni kosa la jinai limeongezwa kwenye kesi tayari.
3. kyelafm haina leseni ya kurushia matangazo.
4. Mmiliki wa radio kuitumia radio yake kujinadi kisiasa linaleta mgongano wa maslahi.
5. uendeshaji wake ni wa kibiashara tofauti kama ilivyoradio. Kyela fm hawana leseni inayoonyesha wamesajiliwa kama radio jamii. kwenye orodha niliyokuta tcra radio jamii ukanda wetu huku ni CHAI Fm tu ya Rungwe na wamiliki ni wakulima wa Chai.
'
Hapo kwenye red font hakuna uhusiano wowote na TCRA. Suala la kujinadi kwa kutumia radio yako ni suala la tume ya uchaguzi. Magufuri anapopata wide coverage UKAWA hawalalamiki TCRA, wanalalamika kwa tume ya Uchaguzi.

Mbona hamuachani na TCRA??? kuna nini? au simu za mkononi ndo mawasiliano tuuuuu!
 
Nyinyi bana naona mumefirisika kimawazo, majibu yenu kila siku ni kudhani waelewa wa kila kitu. Ni much know sana kuliko TCRA kama sio watanzania wote. Hoja hazijengwi juu ya udhaifu wa mwingine kuhalalisha kufanya kosa. Ni bora ukakaa kimya, sio lazima ujibu kila kitu. Nenda TCRA kawaambie hizo hoja zako. Hivi kuachana na TCRA ni lazima? Unaweza kuamua kuachana nao wewe lakini usilazimishe wote tufikiri kama unavyofikiri. TCRA ndo walioifungia na hizo ndo sababu zao hutaki TCRA milango iko wazi.


'
Hapo kwenye red font hakuna uhusiano wowote na TCRA. Suala la kujinadi kwa kutumia radio yako ni suala la tume ya uchaguzi. Magufuri anapopata wide coverage UKAWA hawalalamiki TCRA, wanalalamika kwa tume ya Uchaguzi.

Mbona hamuachani na TCRA??? kuna nini? au simu za mkononi ndo mawasiliano tuuuuu!
 
Tuliomjua tulisikitika alipoteuliwa mwenyekiti wa kamati ya bunge on Richmond.visasi na. undumilakuwili vimemtawala.
 
Mkuu Wangu,
Usidanganywe na hizo propaganda hizo.

Mimi binafsi namfahamu engineer Mwangoka na kwenye hili yeye hahusiki na kabebwa tu na watu toka makao makuu.

Redio za jamii nyingi zinaendelea kutumia CP kwasababu moja tu. Hazina uwezo wa kuweka transmitters zao mbali na vituo. Hiyo ni sheria ya TCRA ambayo imepitwa na wakati kwasababu transmitters za sasa hasa hizi ndogo hazina madhara kabisa na hazina tofauti na TV. Kwa kulielewa hilo TCRA imekuwa ikivivumilia vituo vyote ili viendelee kutumia CP.

Lakini bahati nzuri mwaka jana redio za jamii ziliingia mkataba na Airtel kwa msaada wa UNESCO ili zitumie minara ya Airtel kuweka kurushia matangazo yake. Kyela FM ni moja ya redio zilizofaidika na makubaliano hayo.

Sio kweli kabisa kwamba eti vituo vinatoa rushwa ili viendelee kutangaza. Kwa case ya Kyela FM huyu huyu mama Mwangoka ndiye alikuja kufanya uchunguzi mwaka jana na akaandika recommendation TCRA kwamba sasa tumetimiza masharti yote na tupewe leseni kamili.
Mkuu nakubaliana huyo mama wa TCRA ni tu mmoja mweledi sana na anafanya kazi yake ipasavyo na Mungu ampe ujasiri.
Tatizo ni wale mainjinia waliokupo kabla yake kuja kusafisha maovu.

TCRA tunawaongeza sana kwa kumpeleka huyo mama Mbeya maana hata madudu kama ya Kyela FM yasingejulikana.
 
'
Hapo kwenye red font hakuna uhusiano wowote na TCRA. Suala la kujinadi kwa kutumia radio yako ni suala la tume ya uchaguzi. Magufuri anapopata wide coverage UKAWA hawalalamiki TCRA, wanalalamika kwa tume ya Uchaguzi.

Mbona hamuachani na TCRA??? kuna nini? au simu za mkononi ndo mawasiliano tuuuuu!
Aiseee!!!!
We Nunda umeshindikana!!!
 
'
Hapo kwenye red font hakuna uhusiano wowote na TCRA. Suala la kujinadi kwa kutumia radio yako ni suala la tume ya uchaguzi. Magufuri anapopata wide coverage UKAWA hawalalamiki TCRA, wanalalamika kwa tume ya Uchaguzi.

Mbona hamuachani na TCRA??? kuna nini? au simu za mkononi ndo mawasiliano tuuuuu!
Huya mama wa TCRA ni mchapa kazi na mkweli.
Kama Kyela FM wamefungiwa basi ni kwa sababu ya ukanjanja.
 
hayo mengine, unajua wewe, ila ukweli utabaki pale pale tu kuwa mbunge hana ubavu wa kukifungia kituo cha radio, japo kuna uhuni mwingi wa kisiasa lakini kwa Tz, hatujafikia huko, hayo mambo ya azimio la Bagamoyo unalijua wewe, lakini mwaka huu rais atatoka huko!!
 
Pamoja na udhaifu wa Mwakyembe, lakini jamaa baado ni mtu anaweza kuwasaidia zaidi. Mwakalinga hana vision kabisa.
 
Kama kweli Mwakyembe ameshiriki kukifungia kituo cha Kyela FM kwa kutumia nafasi yake, basi huo ni udikteta na ni hatari.

Pia huo ni ukandamizaji wa demokrasia kwa kutotaka kusikiliza sauti na maoni ya wengi.

Mwisho kabisa ni kwamba Mwakyembe sasa muda wake wa ubunge Kyela umetosha na apishe wengine wenye uwezo wafanye kazi waje na mambo mapya.
 
Mbona mnalia lia kwani ninyi mlijipangaje?????? Ndoroooboooo nyie. Na nasema waifunge tu maana hakuna namna nyingine.
 
Radio husika Kyela FM haijapewa leseni bado kwani hawajakamilisha mchakato wa kupatiwa leseni. Walipewa Construction Permit - kibali cha kujenga na kufanya majaribio kwa mwaka moja- ambapo mamlaka ingekagua masuala ya kiufundi na kiutendaji ili wapewe leseni.

Hawakuweza kukamilisha matakwa ya leseni na pia wamefanya makosa kuanza matangazo bila leseni na kufanya kazi Kama tayari wana leseni. Wamefanya vipindi vinavyokiuka hata masharti Kama wangekuwa na leseni! Kuvunja kanuni za utangazaji, na sheria ya EPOCA pamoja na Kanuni za Utangazaji wakati wa uchaguzi ambazo hawakuwa wamepewa hadi wapate leseni.

Aidha yapo matatizo ya kiufundi ambayo hatuwezi kuweka hapa kwa sababu ya utaratibu na sheria za kuwalinda wateja wetu na washindani wao.

TCRA inapofanya maamuzi hutumia sheria, kanuni na masharti ama ya leseni au kibali cha kujenga kituo na kufanya majaribio!

Endapo hawaridhiki na maamuzi ya TCRA wanaweza kukata rufaa Fair Competition Trubunal.
 
Nyinyi muwe wakweli, mimi hua ninawaonya sana vijana pale redioni ila wanajifanya wajuaji. Hawachukui tahadhari yoyote juu ya habari wanazotangaza husani kipindi hiki cha uchaguzi. Kuna kipindi walirusha kipindi wanahoji watu eti watu wanamtaka mkurugenzi wa redio awe mbunge. Niliwaambia hio sio fair kabisa kwani kuna mgongano wa kimasilahi lakini hawaelewi. Mimi mwenyewe binafsi niliwataarifu TCRA juu ya jinsi ya redio yenu anavyotangaza mambo hayo, yanaweza kuhatarisha amani na mshikamano wa jamii hasa kipindi hiki. Ushabiki wa kisiasa bila maadili kuna siku nilifikiria watu wanaweza kuchoma moto pale redio yenu. Fateni sheria, kanuni na taratibu za vyombo vya habari msikimbie kulaumu na kuhusisha hili tukio na mambo yenu ya kisiasa.

Wanachi wengi wanalaamika kua redio yenu imekua na strength kubwa sna kiasi cha kusababisha redio zote kyela kushika redio yenu tu. Wananchi wakiwaambia kua hilo ni tatizo mnaanza kusema kua TCRA ndo waaulizwe. Mimi binafsi sio mwakyembe lakini nimewahi kuwasilisha malalamiko yote haya nayoyaandika hapa TCRA. Maana tukiwaambia pale redioni mnajifanya hamuelewi. Hii nchi inasheria sisi wanakyela tunahaki ya kupata habari sio kutoka redio yenu tu, wengine tunataka tusikie mambo ya kitaifa sio ya kijiji kama yenu.

Msifanye siasa, fanyeni kazi kwa weledi. Mnasema mkawaambie TCRA tumewaambia sasa mnamsingizia Mwakyembe. Hayo mumeyataka wenyewe na mkurugenzi wenu, mnajifanya wajuaji sana na kudharau sheria mkifikiri mna nchi yenu hapa kyela. Huo ndo mkondo wa sheria. Wananchi wengi tu wanalalamika sana juu ya redio yenu.

Acheni siasa

Miongoni mwa waliopelekea redio yenu hiyo kufungwa mmojawapo huyu hapa kajitokeza hivyo mwacheni mwakembe ,muhusika huyu hapa.
 
Ripoti ya Ukaguzi wa kituo ni Siri yetu na mteja! Wala Ukaguzi ukifanyika mwenye kituo hapewi ripoti hadi imepelekwa menejiment pamoja na bodi ambayo kisheria humshauri Waziri wa Habari kuwa Redio Fulani imekamilisha masharti na Mamlaka inakusudia kumpa leseni.

Waziri hudhiria au hukutaa lakini kwa mujibu wa sheria anawajibika kutoa sababu za kukataa. Kwa maana hiyo Meneja wa Kanda, Menejimenti au Bodi inaweza kutoa kauli ya mdomo kwa mmiliki kama inavyoelezewa hapa.

Tunafanya kazi yetu kwa weledi na kwa kufuata utaratibu, sheria na kanuni za utangazaji! TCRA ingependa kuwakumbusha wadau wetu wenye CP hawaruhusiwi kufanya shughuli za utangazaji hadi wapewe leseni kamili ambayo huandamana na Masharti ya leseni, Sheria ya Mawasiliano ya kielektroniki na Posta pamoja na Kanuni za Utangazaji! Hivi ndio vitendea kazi ambavyo hukabidhiwa mmiliki na kutakiwa kumpa mhariri na Meneja muendeshaji.
 
Ninavyofahamu ni kuwa hiyo ni Radio ya Jamii na hapa ikiwa na maana ni Wanakyela kwa msaada wa UNESCO ndiyo wamejenga hiyo Radio hadi ikafika hapo. Je kuna utaratibu wowote wa Serikali kusaidia hizo Radio au ndiyo yaleyale ya yule Daktari wa Mioyo ambaye Serikali ilihakikisha inamfilisi ili baadaye kabisa waje wanunue Mashine za Mchina.

Tawi lisilozaa hukatwa ila mkono mchafu haukatwi bali unaoshwa. Sijui nyinyi wenzetu mmelalia wapi, kukata au kuosha.

Anyway, nategemea mwezi wa November mambo yatabadilika kwa kutenganisha mchele na pumba.

Kuna haja kwelikweli ya UKAWA kushika hatamu ili Wababe fulani nchi hii waondoke.

Kuli Rashid huko Zanzibar alishasema siku nyingi akiwa kwao Zenji: YANAMWISHO.

Radio husika Kyela FM haijapewa leseni bado kwani hawajakamilisha mchakato wa kupatiwa leseni. Walipewa Construction Permit - kibali cha kujenga na kufanya majaribio kwa mwaka moja- ambapo mamlaka ingekagua masuala ya kiufundi na kiutendaji ili wapewe leseni.

Hawakuweza kukamilisha matakwa ya leseni na pia wamefanya makosa kuanza matangazo bila leseni na kufanya kazi Kama tayari wana leseni. Wamefanya vipindi vinavyokiuka hata masharti Kama wangekuwa na leseni! Kuvunja kanuni za utangazaji, na sheria ya EPOCA pamoja na Kanuni za Utangazaji wakati wa uchaguzi ambazo hawakuwa wamepewa hadi wapate leseni.

Aidha yapo matatizo ya kiufundi ambayo hatuwezi kuweka hapa kwa sababu ya utaratibu na sheria za kuwalinda wateja wetu na washindani wao.

TCRA inapofanya maamuzi hutumia sheria, kanuni na masharti ama ya leseni au kibali cha kujenga kituo na kufanya majaribio!

Endapo hawaridhiki na maamuzi ya TCRA wanaweza kukata rufaa Fair Competition Trubunal.
 
Mamlaka kwa muda mrefu imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wa Kyela na hata vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na baadhi ya vyombo vya habari katika maeneo inakosikika kwa majaribio.

Tunawasihi wadau wetu kufuata taratibu na kuacha kueneza habari zisizo na ukweli.
 
Katika hali ya kushangaza Ndugu Dr. Mwakyembe kaifungia radio ya muhasimu wake kisiasa(George Mwakalinga) ijulikanayo Kyela Fm.

Kitendo hiki wananchi wa Kyela wanakilaani kwani ni ukiukaji wa haki ya habari kwa jamii ya wanakyela na matumizi mabovu ya madaraka .

Tangia Lini Dr. Mwakyembe Amekuwa Mkurugenzi Mkuu Wa TCRA? Ila Naomba Kuuliza Hivi Hili Jina Lenu La Mbeya Limetokana Na Tukio Gani?
 
Back
Top Bottom