Mbunge wa Kishapu(CCM), Suleiman Nchambi aliyekutwa na silaha 16 aburuzwa mahakamani, asomewa mashitaka 12

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,947
95,237
Mbunge wa Kishapu, Suleiman Masoud Nchambi ameshitakiwa kwa makosa 12 ya Uhujumu Uchumi katika Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga ambapo kesi hiyo imetaja kusikiliza tena siku ya Jumatatu Mei 11, 2020 na mtuhumiwa amerudishwa rumande.

Nchambi alikutwa na silaha 16, risasi 536 pamoja na nyama za Wanyamapori mnamo Mei 6.

Soma: Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi (CCM) mbaroni kwa kukutwa na Silaha 16 na risasi 536 - JamiiForums

A91E3D65-4AF2-402E-9F1A-62BFC82B5CC8.jpeg


In God we Trust
 
Halafu Jangili sugu kama hili baada ya siku chache tu, utaambiwa limekaa meza moja na DPP na kukubaliana kuilipa serikali milioni kadhaa halafu linarudi tena mtaani kuuendeleza ujangili wake!

Sijui kama kuna mwana ccm wa kizazi hiki cha sasa ambaye siyo mwizi, mchawi, fisadi, mroho wa madaraka na mali, nk. Labda wale wa enzi za Mwalimu.
 
Km wale wazee wa madini ambao rais aliwataja kwa mbwembwe na kujipatia utukufu akawaachia huyu kijani halisi ataachiwa tu........
Ukitaka mambo yako maovu yasitiriwe jiunge ccm basi
 
Km wale wazee wa madini ambao rais aliwataja kwa mbwembwe na kujipatia utukufu akawaachia huyu kijani halisi ataachiwa tu........
Ukitaka mambo yako maovu yasitiriwe jiunge ccm basi
Lugola kapiga karibu 1T lakini yupo nje kuna watu 17M wapo ndani
 
Back
Top Bottom