Mbunge wa Kigamboni Faustine Ndungulile:Sipingi Ujenzi wa Mji Mpya Kigamboni


R.B

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Messages
6,294
Likes
1,261
Points
280
R.B

R.B

JF-Expert Member
Joined May 10, 2012
6,294 1,261 280
DSCN1199.JPG
galleryicon.png
Mheshimiwa Faustine Ndugulile na Fina Mango baada ya kipindi cha Makutano, Magic FM
DSCN1196.JPG
galleryicon.png
Mheshimiwa Ndugulile akisikiliza swali toka kwa Muendeshaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango
DSCN1197.JPG
galleryicon.png
Mbunge wa Kigamboni akijibu moja ya maswali aliyoulizwa na wasikilizaji wa Kipindi cha Makutano.Picha na Makutano Show-
-
Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Faustine Ndungulile amesema kamwe hajawahi kupinga ujenzi wa mji wa Kigamboni bali alitaka serikali imhakikishie kuwa wananchi wanashirikishwa katika hatua ya maamuzi juu ya mradi wao. Mheshimiwa Ndugulile ameyasema hayo wakati akijibu swali kuhusu msimamo wake juu ya mradi huo katika kipindi cha Makutano, Magic FM.

Mradi huo ambao sasa ni miaka minne tangu uanze kuongelewa umezua mjadala mkubwa kwa wakazi wa Kigamboni, huku Mhe Ndugulile akitolewa kwenye moja ya vikao vya bunge la Jamhuri ya Muungano kutokana na msimamo wake juu ya mradi huo. Alisema tatizo la serikali imekuwa haitaki kufuata sheria inayotaka ushirikishwaji wa wananchi kila hatua katika sera ya mipango miji. Pia aliongezea kusema wananchi wanataka majibu kuhusu lini mradi utaanza, wapi utaanzia, nini hatma yao hasa kuhusu fidia. Alipoulizwa swali na mmoja wa wanakigamboni kuhusu mgogoro uliojitokeza baina yake na madiwani wa jimbo lake uliosababishwa na wao kutembelea moja vikao vya bunge kwa mualiko wa waziri wa ardhi na makazi Mhe Anna Tibaijuka, Ndugulile alijibu kuwa kwa sasa umeisha na kila mmoja ameshajua kosa lake.
 
bornagain

bornagain

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Messages
3,387
Likes
30
Points
145
bornagain

bornagain

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2012
3,387 30 145
Mtasema sana lakini mMarekan keshauziwa na muda wowote anaanza ujenzi
 
Kennedy

Kennedy

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2011
Messages
14,326
Likes
5,353
Points
280
Kennedy

Kennedy

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2011
14,326 5,353 280
Dr Faustine Ni Member Ila Wanaigia Jf Kwa Hofu Sana
 

Forum statistics

Threads 1,237,186
Members 475,465
Posts 29,280,614