Mbunge wa Jimbo la Siha, Godwin Aloyce Mollel(CHADEMA) ajivua wadhifa huo na kuhamia CCM

Mwana Kwetu

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
652
500
Iukiona mtu ananunulika kwa hela ambazo baada ya muda zinaisha hasa Mbunge ni indicator kuwa lengo la kugombea ubunge ni biashara na siyo kutumikia wananchi.
 

LebronWade

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,615
2,000
"CHADEMA wekeni STRATEGIES (mikakati) MPYA ili kuwa-ATTRACT WANACHAMA (waliopo na wapya)" ..... Kaushauri muafaka ... but sidhani kama katapewa uzito katika nyakati hizi za SINGO MPYA inayo-hit isemayo KUNUNULIWA WAPINZANI ... ninapita nitarudi baadae

Ni rahisi kuongea hivyo mkuu than done.....hawa mabwana ndio wapo uwanjani wanacheza,shida wanazopata Mungu anazijua...hamna mtu anaingia uwanjani kwa nia ya kushindwa.....I can feel deeply for the opposition players...ni one of the toughest people and brightest minds we have hands down...dola ndio inataka kuharibu hii nchi...unaua opposition kwa gharama ipi?We will pay dearly as a society..soon than later.
 

busy bees

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
2,250
2,000
Hili tumeling'amua: Wote wanakimbia kumuunga mkona Magu baada ya kutishwa sana! Wengine wana biashara zisizo halali wanafuatiliwa na system wanaambiwa pona yao ni kurudi ccm. Angalia Albert Msando, Wema Sepetu na wengineo. Mwishoni itakuwa wote wale wachafu lazima warudi kwenye jalala la uchafu. Kwa sababu mwenye jalala ni ndiye aliyeiba kura akawepo juu!
CHADEMA msifadhaika hii inaitwa ubatizo wa moto!! dhahabu itabaki safi na ikishatakaswa kwa moto hakuna yeyote atakayeiweza! trust me watakuja wale wasafi waliokuwa jalalani bahati mbaya!! Nguvu ya umma itakuwa kubwa ajabu SUBIRINI!!! leteni operation MAGUFSADI- Kukomesha wizi wa kodi zetu kwa ajili ya kurudisha uchafu jalalani!!
Hao ndo MAKAMANDA wenyewe ... Cream safi .... mie sina neno nafunga mdomo
c9ae9446a0b015ae8e8914a0c71b2d8f.jpg
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
13,548
2,000
Hivi katika hao WAHAMAJI si Nyalandu pia yumo ama mie niko nyuma ya PAZIA ... na mbona nae haitwi MSALITI kwa walompigia kula kule jimboni kwake? au kwa kuwa kavaa GWANDA ....

Yaani KUNYA ANYE KUKU AKINYA BATA KAHALISHA ....

sidhani kama umenielewa,na sijiskii kufafanua any further..........
 

busy bees

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
2,250
2,000
Haiingii akilini eti naunga mkono kutetea rasilimali zetu kwa kujivua ubunge. Huu ndio ufala tunaoambiwa siku zote na Mkapa. Yaani unarudi kwenye kundi letu , huku kusiko na na mahali pa kutunga sheria za kulinda rasilimali, ukakae kijiweni kulinda rasilimali? Only fool can comprehend that. Yaani unatoka huko kwenye kulinda rasilimali unajiunga na sisi tuliokutuma kwa sababu hatuwezi kwenda huko wote unatudanganya eti sasa ndio unallinda are you serious? Yaani mlinzi wa nyumba kupewa master bedroom alale ni jambo linaingia kichwani kwamba ndo anafanya kazi ya ulinzi? Is i it a joke or what?

Ukenge kama huu haipo mahali popote dunani zaidi ya TZ. Hivi mbona hao wa CCM wasiachie nyadhifa zao kuunnga mkono kwa kulinda rasilimali?

Hayo ndio mafanikio yako binafsi au ya chama chako au CCM? Je yale mengine tulikutuma ukayasemee tayari? Tuko maskini, je hili utatoka tena CCM uende CHAUMA au NASA? Kweli Moleli huna akili hata chembe, ulitudanganya wewe ni Dokta kumbe kumbe afadhali mimi wa darasa la saba.

Basi tambua kwamba huko uendako wanamwuliza ziko wapi bambadier zetu, iko wapi meli ya samaki wetu wa Kichina, iko wapi meli yetu ya Bagamoyo? Hizi sii rasilimali?
Maji yamefika shingoni
 

mangikule

JF-Expert Member
Jun 11, 2012
4,580
2,000
Hao ndo MAKAMANDA wenyewe ... Cream safi .... mie sina neno nafunga mdomo
c9ae9446a0b015ae8e8914a0c71b2d8f.jpg
Wote wamebatizwa kwa moto tayari ni wasafi kama dhahabu! tafuteni makinikia muchukue kama kawaida yenu kuepuka dhahabu na kukimbilia uchafu wa dhahabu!!
 

Mbamjo

Member
Mar 30, 2013
82
125
WASIOKUWA NA AJIRA WAPUNGUA: Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS imesema idadi ya watu wasiokuwa na ajira hapa nchini inapungua mwaka hadi mwaka huku ukuaji wa uchumi ukibakia kukua kwa asilimia saba kwa kipindi kirefu.

NBS imeeleza hayo jijini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari wakati wa warsha iliyoandaliwa na ofisi hiyo pamoja na tume ya mipango iliyokutanisha wadau mbalimbali wanaozalisha na kutumia Takwimu kubwa ili kujadili namna ya kupata takwimu bora katika kutathimini mpango wa maendeleo wa Taifa wa muda wa miaka mitano.
Naomba msaada wadau wametumia vigezo vipi kwenye huo utafiti wao?na sampling wamechukua watu wa aina gani?wasomi,waliojiari au vibarua wanaofanya kaz bila mikataba?
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
88,372
2,000
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu , naomba yeyote mwenye kujua chochote kuhusu jinsi CHADEMA ilivyonufaika na uwepo wa Godwin Molel ndani ya chama atueleze , binafsi sijaziona.

Kwa kweli zaidi ya aibu na fedheha ambayo chama kimepata kwa kumpigania BINADAMU AMBAYE AMEWEZA KUJIUZA mithili ya nyanya masalo , sijaona hasara nyingine iliyotokea kwa chadema.

Nachukua nafasi hii kuwaomba radhi wananchi wa jimbo la Siha kwa aibu iliyotokea .
 

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
24,812
2,000
Hilo swali limekuwa la kawaida sasa maskioni mwetu toka upande wenu baada ya kupata pigo la kukimbiwa na mpendwa wenu. Poleni.
 

KALEBE

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
773
500
Kama hawa ndo aina ya wabunge tulionao, ni dhahiri shahiri ya kwamba safari yetu bado ndefu sana katika kufikia demokrasia ya kweli, swali dogo tu la kujiuliza ni je? Mbunge huyu hawezi kutekeleza au kuunga jitihada za magufuli akiwa ndani ya chama chake? Je kuna chama ambacho itikadi yake inakataza kuunga jitihada za dhati zinazofanywa na chama kingine kwa lengo la kuleta maendeleo kwa watu wake, kama jibu ni hapana, huyu mbunge aliyeachia nyadhifa zake hii leo ana lengo gani hasa? Kama hawa ndo wasomi, ambao tunaamini wana uwezo wa kufikiria na kutoa mwelekeo kwa wengine ambao kisomo chao ni cha chini, kwa maamuzi kama haya tuamini kitu gani? na je ikitokea ya kwamba, rais ajaye akashindwa kufanya kama ambavyo huyu jamaa anatarajia, atarudi tena chadema? Nafikiri huyu baba achunguzwe kwa ukaribu yawezekana ni miongoni mwa watu wenye vyeti feki, udaktari wake waweza kuwa na walakini
 

Mnyakatari

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,882
2,000
Kujiuzuru ubunge kwa kigezo cha kuunga mkono juhudi za kulinda rasilimali za taifa huku ukisababisha matumizi makubwa ya rasilimali fedha kwenye uchaguzi wa nafasi unayoiacha wazi ni ukichaa first class....

Fedha zinazopotea kwa ajili ya uchaguzi unaosababishwa na uamuzi wako ni rasilimali inayopotea bure kwa sababu yako wewe mpambanaji wa kulinda rasilimali.

Sasa unajipambanua vipi kuwa wewe unaunga mkono ulinzi wa rasilimali huku hapohapo ukiruhusu matumizi yasiyo ya lazima ya walipa kodi maskiini wa taifa lako.

Wote waliojiuzuru nafasi zao na kusababisha chaguzi kwenye nafasi walizokuwa nazo kwa kigezo cha kuunga mkono kazi inayoitwa "iliyotukuka" au kuunga mkono kupambana na ufisadi na/au rushwa na kulinda rasolimali za nchi ni vichaa....Ni kama vile mtu anayechimba shimo ili apate udongo wa kufukia shimo lingine kwa sababu ya kutuambia yeye hapendi mashimo.Si uchizi??
 

busy bees

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
2,250
2,000
Kujiuzuru ubunge kwa kigezo cha kuunga mkono juhudi za kulinda rasilimali za taifa huku ukisababisha matumizi makubwa ya rasilimali fedha kwenye uchaguzi wa nafasi unayoiacha wazi ni ukichaa first class....

Fedha zinazopotea kwa ajili ya uchaguzi unaosababishwa na uamuzi wako ni rasilimali inayopotea bure kwa sababu yako wewe mpambanaji wa kulinda rasilimali.

Sasa unajipambanua vipi kuwa wewe unaunga mkono ulinzi wa rasilimali huku hapohapo ukiruhusu matumizi yasiyo ya lazima ya walipa kodi maskiini wa taifa lako.

Wote waliojiuzuru nafasi zao na kusababisha chaguzi kwenye nafasi walizokuwa nazo kwa kigezo cha kuunga mkono kazi inayoitwa "iliyotukuka" au kuunga mkono kupambana na ufisadi na/au rushwa na kulinda rasolimali za nchi ni vichaa....Ni kama vile mtu anayechimba shimo ili apate udongo wa kufukia shimo lingine kwa sababu ya kutuambia yeye hapendi mashimo.Si uchizi??
Naanza kwa ku-declare: SIUNGI MKONO GHARAMA ZITUMIKAZO KATIKA CHAGUZI ZA MARUDIO though sipingani na KATIBA ....

Jambo la kushangaza nguvu kubwa sana yatumika kuwashambulia hao waloyaachia majimbo yao kwa sababu ya kumuunga mkono Rais katika jitihada zake za kusimamia RASILIMALI za TAIFA .... sababu kubwa itolewayo ni UHARIBIFU WA PESA za wananchi kwa ajili ya UCHAGUZI wa MARUDIO ...

Swali Fikirishi: ... Hivi pesa itakayotumika kwa uchaguzi wa marudio jimbo aloliachia Mh. Nyalandu si PESA YA WANANCHI? ... mbona hatukuona POVU JINGI akikemewa Mh. Nyalandu kwa uamuzi wake huo? sana sana twaona akipongezwa kwa uamuzi huo na kuonekana shujaa ....

Akiachia mbunge toka SIDE A kwenda SIDE B twapiga VIGELEGELE na kuliza MAVUVUZELA huku tukimkaribisha kwa shangwe pasi na kutaja HASARA itakayolipata taifa kwa uchaguzi wa marudio ... but

Akiachia mbunge toka SIDE B kwenda SIDE A ni LAANA zamiminika mwanzo mwisho, avuliwa nguo na kufanywa kama HAYAWANI huku akitwishwa zigo zito la MSALITI na tukimlaani kwa kuliingiza taifa katika gharama za uchaguzi mwingine ....

THIS IS DOUBLE STANDARD and HYPOCRISY nothing else ... hebu tuwe WATANZANIA WAZALENDO
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom