Mbunge wa Jimbo la Siha, Godwin Aloyce Mollel(CHADEMA) ajivua wadhifa huo na kuhamia CCM

Wa kumlaumu Nyalandu yeye ndie alianza mchezo wa kujivua ubunge na kwenda chama kingine na alipofanya hivyo hatukusikia kelele zote hizo bali alionekana shujaa,ila wengine wakitumia haki yao wale wavuka mto Mara huja na kejeli na matusi kibao,basi hata Nyalandu atakuwa amerogwa
Na si kulogwa tu bali pia na yeye KANUNULIWA na wenye chama
 
nyie mliohama wote ni wasaliti,

Kama CCM inavutia,ndio mlitakiwa mpigane ndani ya chama chenu, muweke strategies mpya kuwaatract wanachama wapya,sio kuhama,

Nawashangaa sana,mnataka turudi kwenye serikali ya chama kimoja,sidhani kama lipo duniani?????????????!!!!!!!!!!,

Tanzania haitawasamehe kwa hili,

wapinzani wapo kucreate balance,at least serikali inawork within boundaries,sasa mkicreate chama kimoja huoni kama mnmapa Rais afanye anavyotaka?????? akifanya lolote la hovyo mtakua na audacity ya kumkosoa ???demokresia ndio bye bye kulinda matumbo yenu!
"CHADEMA wekeni STRATEGIES (mikakati) MPYA ili kuwa-ATTRACT WANACHAMA (waliopo na wapya)" ..... Kaushauri muafaka ... but sidhani kama katapewa uzito katika nyakati hizi za SINGO MPYA inayo-hit isemayo KUNUNULIWA WAPINZANI ... ninapita nitarudi baadae
 
Ila Nyarandu namuaminia ana maakili akipewa nafasi na wengine yeye pamoja na Lowasa,Tundu lisu akipona,wakikaa pamoja na kuweka mkakati wa chama chao,watafanikiwa tu,......wasipanick
Hivi katika hao WAHAMAJI si Nyalandu pia yumo ama mie niko nyuma ya PAZIA ... na mbona nae haitwi MSALITI kwa walompigia kula kule jimboni kwake? au kwa kuwa kavaa GWANDA ....

Yaani KUNYA ANYE KUKU AKINYA BATA KAHALISHA ....
 
Hivi mtu hawezi kuwa kuunga mkono jitihada za serikali kuleta maendeleo akiwa upinzani ? Kiazi
Inawezekana kabisa kufanya hivyo (kupongeza juhudi) ... tatizo ni pale ambapo yule aisifuye serikali anaposhambuliwa kama mpira wa kona na kuanza kuitwa MSALITI na kukaliwa na vikao ... rejea sakata la Mh. Nasari aliposhambuliwa na kusakamwa humu SOCIAL MEDIA kisa kaipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya JPM
 
Mbunge wa Jimbo la Siha kwa tiketi ya CHADEMA, Godwin Ole Mollel ajiuzulu nafasi hiyo pamoja na uanachama wa CHADEMA kuanzia leo Disemba 14, 2017.

Mwanasiasa huyo amesema kuwa ameshindwa kuukataa ukweli huu kuwa hivi sasa uongozi wa nchi yetu chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM) umedhihirisha wazi kupigania rasilimali za nchi na kwa kuwa niliomba ridhaa ya Ubunge kwa ahadi ya kupigania rasilimali za nchi nimejikuta sina namna nyingine zaidi ya kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiuzulu Ubunge wangu ili niungane na CCM katika jukumu hili muhimu kwa Taifa.

Nimefanikiwa kuipata barua yake ya kujiuzulu na kujivua uanachama wa CHADEMA;

Video





Kama kuna kosa linawatafuna CHADEMA ni Jimbo la Siha, hadi leo linaendelea kuwatafuna. Mbunge wake alikuwa ni Mwanri (sasa ni Mkuu wa Mkono Shinyanga) enzi hizo akiwa Waziri wa kikwete wa TAMISEMI. Ni mtu mwema, makini, anaheshimika TANZANIA nzima. Wakati huo alikuwa Boss wake Majaliwa Kassim ambaye sasa ni Waziri Mkuu. Ni nani asiyemjua Mwanri, yule jamaa sauti nene ya kufoka, jeusi tii, nywele kipilipili, Mtanzania orijino. Tulitegemea angechaguliwa kuwa Waziri Mkuu, lakini akatumiwa ujumbe na Lowassa ajiunge na Chadema kama anataka ubunge. Mwanri alipokataa si ndiyo wakamfitinisha na wananchi (ni eneo la Waarusha wakulima na Wamasai wafugaji, Mwanri ni Mchagga). Pia inaaminika kura zake zilichakachuliwa. Watashinda jimbo, wakadhani wameshinda, kumbe mambo yenyewe ndiyo haya. Sasa tusubiri video ya Nassari tumuone huyu Mbunge kahongwa na Mnyeti.
 
Hili tumeling'amua: Wote wanakimbia kumuunga mkona Magu baada ya kutishwa sana! Wengine wana biashara zisizo halali wanafuatiliwa na system wanaambiwa pona yao ni kurudi ccm. Angalia Albert Msando, Wema Sepetu na wengineo. Mwishoni itakuwa wote wale wachafu lazima warudi kwenye jalala la uchafu. Kwa sababu mwenye jalala ni ndiye aliyeiba kura akawepo juu!
CHADEMA msifadhaika hii inaitwa ubatizo wa moto!! dhahabu itabaki safi na ikishatakaswa kwa moto hakuna yeyote atakayeiweza! trust me watakuja wale wasafi waliokuwa jalalani bahati mbaya!! Nguvu ya umma itakuwa kubwa ajabu SUBIRINI!!! leteni operation MAGUFSADI- Kukomesha wizi wa kodi zetu kwa ajili ya kurudisha uchafu jalalani!!
 
Tatizo la vijana wa CDM wamejaa kebehi, matusi na dharau. Jaribuni kutumia akili zenu japo kidogo.
Nyie mnasema hawa wananunuliwa, sawa kabisa! Soko lipo wapi? Huko sokoni wanaenda fisiemu tu? Nyie hamhitaji hizi bidhaa? Nanyi kanunueni km mlivyofanya kwa Nyala.
Cdm ilipoteza uelekeo toka ilipo wanunua kina luwasa na zero. Walikiuka misingi na agenda zao zilizokuwa zinawapa nguvu. Walitaka starehe ya muda mfupi wakasahau magonjwa. Wale jamaa ni magonjwa waliokuja kuua upinzani tulio upenda.
Matusi, kejeli na dharau hazitatusaidia. Tujibu hoja kwa hoja.
 
Kama ilivyo katika mapenzi, kuwa si kila mmoja huwa ni mpenzi bali wengine huwa ni wapenzi watazamaji!!!
Mniwie radhi kwa kauli hii kuwa nchi yetu bado haijatunukiwa wanasiasa wakomavu na wenye kusimamia nia njema ya chama chao, wengi wapo ku struggle ili wapate chochote. Mtu anapoacha ubunge kwa kigezo cha kumuunga mkono rais huyo ni muongo kwasababu kufanya uchaguzi ni gharama kuliko hata kumuunga mkono rais!!!
Watu wa namna hii nashauri hata utendaji wa kata wasipewe, maana ni wanafiki wanadhani wanakisaliti chama na wakati wanawasaliti wananchi walio wachagua.
Nyerere na wapigania uhuru wetu wangekuwa na fikra mbovu Kama hizi za kutamani tamani nadhani mpaka Leo tungekuwa colony la mwingereza, wazee wetu hawa hawakuikimbia TANU kwenda kumuunga mkono gavana Richard Turnbull. Walisimamia Nia yao moja na wakaridhika na kidogo walichokuwa nacho hatimaye tukafanikiwa kupeperusha bendera yetu na kutambulika kama Taifa.
*ANGALIZO KWA CCM*
Kuweni makini sana na wanademokrasia uchwara kama hawa.
Chama kisijivune kurusha vyavu katika dimbwi kubwa la samaki. Kumbukeni si vyote vinavyokuja ni samaki, kuna vyura na kenge pia.
Watu hawa wasio na misimamo wala uchungu na Taifa maskini kama hili, wanaoacha majimbo yao ili hela ambayo ingefanya shughuli zingine za maendeleo ikafanye uchaguzi wa marudio ktk majimbo yao ni wa kuogopa kama ukoma!!
Nashauri CDM wasikatishwe tamaa na hawa wanaharakati hewa.
*Ni maoni tu wapendwa *
Huu mchezo hauhitaji hasira. Mbona hukutoa povu walivyohama nyala? Hukuona hasara kwa taifa wala ccm? Ccm hawakukatishwa tamaa? Kwanini hutaki kuongea ukweli? Kwanini unakuwa kipofu na kiziwi kiasi unajitoa ufahamu? Tunafanya makosa kuwaona hawa wanaohamia ccm ni wasaliti na wanaohamia cdm ni makamanda. Cdm ni kuwambia ukweli tu, viongozi wetu wajitathmini, na wawe na mikakati vitendo hivi visijirudie. Sio kuwapa moyo wa kijinga kabisa. Ila nakupongeza kuwa tahadharisha hao ccm.
Hv, sera na agenda yetu kubwa nini sisi kama chama kikuu cha upinzani?
 
Sasa kama mwenyekiti alisema chama ni watu, na hao wanaoondoka ni watu, nani atabaki sasa.
 
Hahaahaaa...muasisi was kampeni hii anajulikana mkuu ni Lazaro Nyalandu, alidhani wengine watamfuata huko alikokimbilia bahati mbaya upepo umegeuka. Muwe wapole ndo makali ya msumeno yalivyo
Huyo aliamua kuachana na wajinga wasioweza kujibu hoja kwa hoja badala yake kutumia maguvu na vitisho
 
Haiingii akilini eti naunga mkono kutetea rasilimali zetu kwa kujivua ubunge. Huu ndio ufala tunaoambiwa siku zote na Mkapa. Yaani unarudi kwenye kundi letu , huku kusiko na na mahali pa kutunga sheria za kulinda rasilimali, ukakae kijiweni kulinda rasilimali? Only fool can comprehend that. Yaani unatoka huko kwenye kulinda rasilimali unajiunga na sisi tuliokutuma kwa sababu hatuwezi kwenda huko wote unatudanganya eti sasa ndio unallinda are you serious? Yaani mlinzi wa nyumba kupewa master bedroom alale ni jambo linaingia kichwani kwamba ndo anafanya kazi ya ulinzi? Is i it a joke or what?

Ukenge kama huu haipo mahali popote dunani zaidi ya TZ. Hivi mbona hao wa CCM wasiachie nyadhifa zao kuunnga mkono kwa kulinda rasilimali?

Hayo ndio mafanikio yako binafsi au ya chama chako au CCM? Je yale mengine tulikutuma ukayasemee tayari? Tuko maskini, je hili utatoka tena CCM uende CHAUMA au NASA? Kweli Moleli huna akili hata chembe, ulitudanganya wewe ni Dokta kumbe kumbe afadhali mimi wa darasa la saba.

Basi tambua kwamba huko uendako wanamwuliza ziko wapi bambadier zetu, iko wapi meli ya samaki wetu wa Kichina, iko wapi meli yetu ya Bagamoyo? Hizi sii rasilimali?
 
Back
Top Bottom