Malafyale
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 13,813
- 11,126
Wajumbe wanne wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF), na maofisa wengine saba wa chama hicho akiwemo Mbunge wa Viti Maalum (Tabora), ambaye pia ni Katibu wa Wabunge wa CUF, Magdalena Sakaya, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Urambo mkoani Tabora kwa shtaka la kufanya mkutano bila kibali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Liberatus Barlow, aliliambia NIPASHE jana kuwa walifikishwa mahakamani hapo jana asubuhi chini ya ulinzi mkali wa polisi na kusomewa mashtaka ya kumshambulia mpelelezi, kutojitambulisha kwa makusudi kwa askari polisi na kwenda kuchukua mifugo ambayo inashikiliwa na polisi.
Kamanda Barlow alisema walifikishwa mbele ya Hakimu Oscar Burugu wa mahakama hiyo, baada ya kusomewa mashtaka walinyimwa dhamana.
Alisema mahakama hiyo ilikataa dhamana yao kwa kuhofia kuvunjika kwa amani kwani wangeweza kwenda kuhamasisha wananchi kwenda kuchukua mifugo ambayo bado inashikiliwa na polisi.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alisema mahakama hiyo imewanyima dhamana ikidai kuwa iwapo wataachiwa amani inaweza kuvurugika.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 6, mwaka huu na washtakiwa wote walirudishwa rumande.
Wajumbe hao wa Baraza Kuu waliofikishwa mahakamani na kunyimwa dhamana pamoja na mbunge huyo, ni Doyo Hassan, Yassin Mrotwa, Zainabu Nyumba na Masoud Omar.
Wengine ni Ofisa Haki za Binadamu na Sheria Makao Makuu ya CUF, Hashim Bakari na aliyekuwa mgombea ubunge kupitia chama hicho Jimbo la Urambo Magharibi, Kirungi Kirungi.
MY NOTE:Niliwahi kumsikia Mwenyekiti wa CUF Prof Lipumba akisema kuwa CHADEMA kukamatwa kwao Arusha ilikuwa halali maana ni CHADEMA ni chama cha vurugu na kutotii sheria za nchi;sasa kwa kukamatwa kwa Mbunge wao na watendaji wa ngazi za juu wa CUF bado Lipumba atazidi kusema kuwa CHADEMA hawafuati sheria au sasa atajirudi na kugundua kuwa serikali ya CCM imeshindwa kutawala na sasa inadumu kwa nguvu za dola tu?