Huyu jamaa kazi yake kuuza sura tu mjini atawapa chadema wakati mgumu sana hapo badae!
Mimi kama Kiongozi wa CHADEMA Mkoa wa Iringa nataka kuweka wazi kwamba ni mapema mno kumpima Msigwa utendaji kazi wake kwa kipindi cha miezi kumi na moja tu.
Kwanza yeye alipoingia madarakani alikuta Mbunge aliyemtangulia kachukua mafaili yote ya Ofisi na kuondoka nayo nyumbani kwake.Ikumbukwe kwamba mbunge huyo, Monika Mbega (CCM) alikuwa ni Mbunge wa Iringa mjini tangu mwaka 2000 hadi 2010. Kwa maana nyingine ni kwamba Mbega ameondoka na taarifa rasmi za Ofisi ya mbunge wa Iringa Mjini za kipindi cha miaka 10.
Hivi Msigwa anaweza kujua ni miradi mingapi ilikuwa inasimamiwa na Ofisi ya Mbunge kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita bila ya kuwa na kumbukumbu za kiofisi ambazo Monica Mbega ameondoka nazo? Kwa mfano ni vikundi vingapi vya uzalishaji mali vilifadhiliwa na ofisi ya mbunge na vilifadhiliwa kwa kiasi gani cha fedha.
Watoto na watu wengine walio kwenye mazingira magumu wamesaidiwaje na Mbunge aliyepita na wako kwenye hatua ipi. Mbega aliwasiliana na ofisi ngapi kwa niaba ya watu wa Iringa na aliwasiliana na ofisi hizo kwa lengo lipi. Hoja yangu hapa ni kwamba kabla ya kumbebesha mzigo mkubwa Msigwa ni lazima kwanza tumsaidie kupata nyaraka hizo muhimu za kiofisi ili aweze kuchapa kazi kiufanisi.
Ni kweli kwamba Msigwa ni mwenyekiti wa Iringa Mjini, lakini swala la Uchaguzi wa kata hizi za Gangilonga na Kitanzini ambazo tulipoteza tulifanya mkosa ya kiufundi kwenye kuchagua wagombea na jinsi tulivyoendesha kampeni zetu. Hakuna wa kumlaumu katika hili, kwani wote kwa pamoja tuliipoanza kampeni tuliamini kwamba tutashinda lakini hali ya mambo baadaye haikuwa upande wetu.
kushindwa kwetu kulitokana na makosa ya kiufundi ambayo hatudhani kama huko tuendako tutayarudia tena. Kitu pekee ninachokiona ni kwamba watu wengi wanafikiri kwa kupambana na Msigwa itakuwa ni rahisi kwao kuwa wagombea wa CHADEMA kwenye nafasi ya Ubunge hapa Iringa Mjini mwaka 2015.
Ushauri wangu kwao badala ya kuanzisha kampeni za kupakana matope na kujifagilia basi tumsaidie Msigwa ili ikifika mwaka 2015 wana Iringa Mjini waone tofauti kati ya mbunge wa CCM na wa CHADEMA. Tunaye diwani mmoja Bwana Nyalusi yeye naye aonyeshe kwenye kata yake ya Mvinjeni jinsi ya kuendesha utawala bora ili mwaka 2015 tuwe na cha kuwaonyesha wananchi.