Mbunge wa CHADEMA (Msigwa) atalipoteza jimbo kwa mwendo huu

Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,045
Katika sehem ambayo inanipa mashaka sana kwa kuwepo na kuendelea kuwepo uongozi wa CHADEMA ni manispaa ya Iringa.
Pamoja na kufanyika uchaguzi mdogo wa madiwani kata ya Kitanzini na Gangilonga CDM hawakupata ushindi ingawa alikuja Mbowe na Joseph Sugu na wakati wa uchaguzi Msigwa alikuwepo lakini bado CDM ilitoka kapa.
Mtazamo wangu ni kwamba CDM inaweza kupoteza jimbo by 2015 kama hali itabaki hivi.
 
Msigwa hana uwezo wa kuvuta hisia za vijana ,katika uchaguzi wa 2010 mchungaji alipita kutokana na vita ya wenyewe ndani ya CCm baada ya Mwakalebela kuenguliwa. Lakini Bi Chiku Abwao akijipanga uzuri jimbo litabaki ndani ya CDM kama Msigwa asipoleta makundi. Kauli za msigwa mara nyingi zinajikanganya sana.
 
Anastahili kushauriwa na aenende katika mstari wa wenzake,lakini pia kuna haja ya kuangalia tatizo ni nini kisha kujipanga namna ya kuli-address tatizo.tukikubali kuliachia hilo jimbo ina maana tunakubali tuendelee na Magamba ya sisiemu
 
But kaz yake nzuri bungeni tunaweza kuipima then ndo ........................, naona ni mwenye ujasiri sana na mpambanaji mzuri
 
Unachosema au ulichoandika una uhakika nacho au unakurupuka tu,umetumwa na magamba fikra finyu hizo za MAGAMBA wewe K.I.L.A.ZA nenda shule kwanza uje uweke upupu hapa.
 
kati ya watu wanaonivutia ktk uchangiaji wa hoja ubengeni huyu msigwa huwa namkubali sijui tatizo liko wapi.
 
gangilonga ni maeneo ya watajiri(mafisadi)wengi wao ni magamba hawana shida hao!kitanzini siwezi kujua sababu ya chadema kushindwa.
 
Jamani uchaguzi ulikuwa kata za gangilonga kama sikosei, huko ndio wenye neema wana kaa wataitisa ccm kweli?
 
Hizi propaganda hizi kila siku kila mtu anaibuka na lake.

Msigwa ana miaka minne zaidi ya kukamilisha kazi aliyotumwa na wananchi, sasa chini ya mwaka mmoja tayari mmeshaanza mizengwe.
 
Katika sehem ambayo inanipa mashaka sana kwa kuwepo na kuendelea kuwepo uongozi wa CHADEMA ni manispaa ya Iringa.
Pamoja na kufanyika uchaguzi mdogo wa madiwani kata ya Kitanzini na Gangilonga CDM hawakupata ushindi ingawa alikuja Mbowe na Joseph Sugu na wakati wa uchaguzi Msigwa alikuwepo lakini bado CDM ilitoka kapa.
Mtazamo wangu ni kwamba CDM inaweza kupoteza jimbo by 2015 kama hali itabaki hivi.
Tuacheni Iringa na Msigwa wetu, kwa muda mchache toka aiingie bungeni amekwisha tuhakikishia kuwa hatukufanya makosa kumchagua; kafanya mambo mengi ambayo magamba hawakuyafanya. Kwa kifupi sisi ndio tunaomjua mbunge wetu na CDM yetu. Kukosa udiwani isiwe issue, in short tunakijua tunachokifanya na tunampango Msigwa awe mbunge wetu wa maisha ni kifo tu kitatutenga naye. Mwakalebela ni mnafiki tulishamsoma kitambo hata arudi vipi ataambulia manyoya, anaanzisha ligi ya mpira wa miguu kuwarubuni vijana, but mpira tutacheza na zawadi tuachukua, but CHADEMA ndio baba ndio mama.
 
Ni vema ukiwa mmoja wa wadau ukaainisha maeneo yenye upungufu na solution kuliko kulalamika, kwani malalamiko hayasaidi.
 
Tuacheni Iringa na Msigwa wetu, kwa muda mchache toka aiingie bungeni amekwisha tuhakikishia kuwa hatukufanya makosa kumchagua; kafanya mambo mengi ambayo magamba hawakuyafanya. Kwa kifupi sisi ndio tunaomjua mbunge wetu na CDM yetu. Kukosa udiwani isiwe issue, in short tunakijua tunachokifanya na tunampango Msigwa awe mbunge wetu wa maisha ni kifo tu kitatutenga naye. Mwakalebela ni mnafiki tulishamsoma kitambo hata arudi vipi ataambulia manyoya, anaanzisha ligi ya mpira wa miguu kuwarubuni vijana, but mpira tutacheza na zawadi tuachukua, but CHADEMA ndio baba ndio mama.
Aiseee huyu jamaa mimi najua ni mpambanaji sasa nashangaa mnaposema amekalia kuti kavu! Mimi kwa mbali nahisi Mr Two aka Sugu afanye mambo yanayoeleweka vinginevyo watu wa Mbeya wanaweza kumwaga vinginevyo kura zipigwe kishabiki.
 
Huyu jamaa kazi yake kuuza sura tu mjini atawapa chadema wakati mgumu sana hapo badae!
Mimi kama Kiongozi wa CHADEMA Mkoa wa Iringa nataka kuweka wazi kwamba ni mapema mno kumpima Msigwa utendaji kazi wake kwa kipindi cha miezi kumi na moja tu.

Kwanza yeye alipoingia madarakani alikuta Mbunge aliyemtangulia kachukua mafaili yote ya Ofisi na kuondoka nayo nyumbani kwake.Ikumbukwe kwamba mbunge huyo, Monika Mbega (CCM) alikuwa ni Mbunge wa Iringa mjini tangu mwaka 2000 hadi 2010. Kwa maana nyingine ni kwamba Mbega ameondoka na taarifa rasmi za Ofisi ya mbunge wa Iringa Mjini za kipindi cha miaka 10.

Hivi Msigwa anaweza kujua ni miradi mingapi ilikuwa inasimamiwa na Ofisi ya Mbunge kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita bila ya kuwa na kumbukumbu za kiofisi ambazo Monica Mbega ameondoka nazo? Kwa mfano ni vikundi vingapi vya uzalishaji mali vilifadhiliwa na ofisi ya mbunge na vilifadhiliwa kwa kiasi gani cha fedha.

Watoto na watu wengine walio kwenye mazingira magumu wamesaidiwaje na Mbunge aliyepita na wako kwenye hatua ipi. Mbega aliwasiliana na ofisi ngapi kwa niaba ya watu wa Iringa na aliwasiliana na ofisi hizo kwa lengo lipi. Hoja yangu hapa ni kwamba kabla ya kumbebesha mzigo mkubwa Msigwa ni lazima kwanza tumsaidie kupata nyaraka hizo muhimu za kiofisi ili aweze kuchapa kazi kiufanisi.

Ni kweli kwamba Msigwa ni mwenyekiti wa Iringa Mjini, lakini swala la Uchaguzi wa kata hizi za Gangilonga na Kitanzini ambazo tulipoteza tulifanya mkosa ya kiufundi kwenye kuchagua wagombea na jinsi tulivyoendesha kampeni zetu. Hakuna wa kumlaumu katika hili, kwani wote kwa pamoja tuliipoanza kampeni tuliamini kwamba tutashinda lakini hali ya mambo baadaye haikuwa upande wetu.

kushindwa kwetu kulitokana na makosa ya kiufundi ambayo hatudhani kama huko tuendako tutayarudia tena. Kitu pekee ninachokiona ni kwamba watu wengi wanafikiri kwa kupambana na Msigwa itakuwa ni rahisi kwao kuwa wagombea wa CHADEMA kwenye nafasi ya Ubunge hapa Iringa Mjini mwaka 2015.

Ushauri wangu kwao badala ya kuanzisha kampeni za kupakana matope na kujifagilia basi tumsaidie Msigwa ili ikifika mwaka 2015 wana Iringa Mjini waone tofauti kati ya mbunge wa CCM na wa CHADEMA. Tunaye diwani mmoja Bwana Nyalusi yeye naye aonyeshe kwenye kata yake ya Mvinjeni jinsi ya kuendesha utawala bora ili mwaka 2015 tuwe na cha kuwaonyesha wananchi.
 
Msigwa ni kiongozi jasiri na mwenye hekima sana na mpambanaji...kama anaudhaifu huo basi aufanyie kazi..tofaut na hapo ni mzuri bado.
 
gangilonga ni maeneo ya watajiri(mafisadi)wengi wao ni magamba hawana shida hao!kitanzini siwezi kujua sababu ya chadema kushindwa.
mkuu kitanzini wamejaa waswahili na wengi wao shule hakuna kidoogo maeneo ya miyomboni sokoni na stendi wanajitambua kifikra na ndo kula nyingi za CDM zilitoka hapo,ila maeneo ya Kitanzini walinunuliwa na el 2000 kila siku nyumba hadi nyumba
 
. Lakini Bi Chiku Abwao akijipanga uzuri jimbo litabaki ndani ya CDM kama Msigwa asipoleta makundi. Kauli za msigwa mara nyingi zinajikanganya sana.
sijui kwa nini umejiita Ipogolo. Lakini ni nini kimekutuma uanze kuzungumzia uchaguzi ambao uko mbele kwa miaka minne kuanzia sasa. Chiku ana haki ya kugombea kama atakuwa hai na bado mwanachama wa CHADEMA. Kuna kitu kinaitwa SWOT kwenye kila uchambuzi anaoufanya mtu. Yaani Strength, Weakness, Opportunity na Threat. Zitumie hizo ili uweze kutuambia Udhaifu, Uimara, Fursa na Hatari za hao wote wawili kwenye kugombea ubunge mwaka 2015.

kwa nini unaamini kwamba Chiku ndiye "akijipanga" vizuri atakibakiza kiti cha Ubunge mikononi mwa CHADEMA na siyo Msigwa? Hebu tufanye kazi za kuwatumikia wananchi kuliko kushabikia watu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom