Mbunge wa CHADEMA ataka wananchi waiamini CCM!!

Hakuna haja ya kubishana na mtu -------- kama shibuda...
 
Huyu Shibuda tumemvumilia sana. Amalize tu hiki kipindi

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Mkuu kaa pembeni na uzi huu. Ukiingia pale Mirembe ukakuta wagonjwa wanasakata dansi la wimbo uupendao nawe utacheza? Sii utawaacha waendelee kuselebuka? Sasa hili ndio hilo dansi,twende kwenye mengine hao waache wacheze.
 
Niliposoma tu mwanzzoni nikawa nimeisha jua atakuwa shibuda, mwanamme asiye jua anataka nini, pia ni tatizo, lakiniukimwangalia tu ata tembea yake unapata majibu hivyo hawezi kusumbua akili za mwanamme yeyote
 
...Ila Shibuda ni gangwe, Hapo CHADEMA hakuna wa kumnyanyulia mdomo. Keep it up Shibuda, tunahitaji wabunge wengine mia, majasiri kama wewe!
 
Mara ya mwisho nakumbuka mwenyekiti wa Chadema ndugu Mbowe akimwaga sifa kedekede kwa Mwenyekiti wa CCM, JK, pindi JK alipoenda kule Hai kilimanjaro kufungua mradi wa barabara!. Kwa hiyo tusiwe na double standards, kama mtu ni mchapakazi apewe sifa yake!!. au kama tunamshambulia Shibuda, basi tukumbuke Mbowe ndo alitoa sifa zaidi kwa kiongozi wa CCM!!!
 
Kumbe habari yenyewe kutoka gazeti la chama UHURU na yaliyomo humo yamesemwa na SHIBUDA. Basi sawa......!
 
Na mwandishi Stephen Beligeya Dodoma;

Mbunge wa Maswa Magharibi [CHADEMA] John Magale Shibuda,amemwagia sifa katibu mkuu wa CCM Abdrahaman Kinana,kwa kumuelezea kuwa ni kiongozi mtendaji,makini na mchapa kazi na msikivu ktk kushughulikia kero za wananchi.
Pia alisema kuwa Ccm ni chama sikivu na makini ktk kusikiliza kero za wananchi hivyo kuwataka wananchi kuwa na imani nacho ili matatizo mbalimbali yanayowakabili yaweze kutatuliwa,kauli hii ya Shibuda ambae ni mwana siasa makini na muwazi aliitoa mjini Dodoma.

Alisema inapokuja swala la maendeleo na uzalendo kwa taifa,hapo ndipo inapo dhiirisha namna na jinsi CCM na serikali yake inavyotimiza wajibu ktk kuwatumikia wananchi wake bila kujali itikadi.
Hayo aliyaeleza ktk mkutano wa pamoja kati ya wawakilishi wa wafugaji kutoka wilaya mbalimbali ktk mkoa wa Dodoma,Mbeya na Morogoro ulioandaliwa na Kinana kwa ajili ya kusikiliza kero zonazowakabili.

Shibuda alisema kuwa Kinana amekuwa kiongozi Hodari makini na mchapa kazi,hivyo kuwataka wafugaji hao kuwa na imani nae.

Chanzo: Gazeti la Uhuru!

hapo kwenye RED, kama kweli yuko makini basi alienda CHADEMA kwa malengo ya kuivuruga, sasa ameshindwa kutekeleza lengo lake ndio anaanza kuonesha wazi alichokusudia, vinginevyo hana umakini wowote ndio maana matendo vyake na maneno yake yanatofautiana.
 
Mara ya mwisho nakumbuka mwenyekiti wa Chadema ndugu Mbowe akimwaga sifa kedekede kwa Mwenyekiti wa CCM, JK, pindi JK alipoenda kule Hai kilimanjaro kufungua mradi wa barabara!. Kwa hiyo tusiwe na double standards, kama mtu ni mchapakazi apewe sifa yake!!. au kama tunamshambulia Shibuda, basi tukumbuke Mbowe ndo alitoa sifa zaidi kwa kiongozi wa CCM!!!

Huwezi kumfananisha JK na Kinana
 
Na mwandishi Stephen Beligeya Dodoma;

Mbunge wa Maswa Magharibi [CHADEMA] John Magale Shibuda,amemwagia sifa katibu mkuu wa CCM Abdrahaman Kinana,kwa kumuelezea kuwa ni kiongozi mtendaji,makini na mchapa kazi na msikivu ktk kushughulikia kero za wananchi.
Pia alisema kuwa Ccm ni chama sikivu na makini ktk kusikiliza kero za wananchi hivyo kuwataka wananchi kuwa na imani nacho ili matatizo mbalimbali yanayowakabili yaweze kutatuliwa,kauli hii ya Shibuda ambae ni mwana siasa makini na muwazi aliitoa mjini Dodoma.

Alisema inapokuja swala la maendeleo na uzalendo kwa taifa,hapo ndipo inapo dhiirisha namna na jinsi CCM na serikali yake inavyotimiza wajibu ktk kuwatumikia wananchi wake bila kujali itikadi.
Hayo aliyaeleza ktk mkutano wa pamoja kati ya wawakilishi wa wafugaji kutoka wilaya mbalimbali ktk mkoa wa Dodoma,Mbeya na Morogoro ulioandaliwa na Kinana kwa ajili ya kusikiliza kero zonazowakabili.

Shibuda alisema kuwa Kinana amekuwa kiongozi Hodari makini na mchapa kazi,hivyo kuwataka wafugaji hao kuwa na imani nae.

Chanzo: Gazeti la Uhuru!
looser!!!
 
Viongozi wa CHADEMA wamekomaa kisiasa, wana uwezo wa kuvumilia hata Mbunge wa CCM ndani ya chama. Kwa sasa, je, kuna mbunge wa CCM anaweza kumsifia Mrema kwa utendaji wake wa kipindi kile?
 
Ccm ni chama makini siku zote wakisema lakini kinasonga mbele.

ulitegemea aseme nn? alishapima upepo cdm kuwa alishashitukiwa muda mrefu ameamua kurudi kwa waliomtuma.cdm walishamtema kiaina siku nyingi.
 
Back
Top Bottom