Mbunge wa CCM mbaroni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge wa CCM mbaroni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Oct 9, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Mbunge wa CCM mbaroni
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Friday, 07 October 2011 19:43 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Mwandishi Wetu
  MBUNGE wa Mbarali (CCM), Modestus Kilufi amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumtishia maisha mtendaji wa kata moja katika jimbo lake.Akizungumza kwa simu jana akiwa chini ya ulinzi wa polisi, mbunge huyo alisema alikamatwa akiwa jimboni kwake Mbarali na kusafirishwa hadi Kituo Kikuu cha Polisi Mbeya Mjini.

  “Nimekamatwa na polisi. Wamekuja polisi wengi wakiwa na silaha na gari. Nilikuwa Mbarali na sasa wananipeleka Mbeya Mjini,” alisema Kilufi na kuongeza:

  “Nimewauliza tatizo ni nini wakasema eti nimemtishia Ofisa Mtendaji wa Kata na nilipowauliza kwa nini hawakunipigia simu kwamba nahitajika kituoni hawakutaka kunisikiliza,” alisema.

  Alisema anashangaa polisi hao kutompigia simu na kumweleza kuwa anatafutwa ili afike mwenyewe kwa kuwa yeye ni kiongozi na badala yake kwenda kumkamata Mbarali ili wampeleke Mbeya Mjini.

  “Hayo ndiyo yamenikuta. Huyo mtu wanayesema nimemtishia maisha sijawahi hata kukutana naye tangu nimetoka bungeni, kwa sasa tupo maeneo ya Uyole ndiyo tunaelekea Mbeya Mjini, wako askari kama wanne, watano hivi, ngoja tukasikie kitakachotokea huko,” alisema mbunge huyo jana saa 11.45 jioni kupitia simu yake ya mkononi.

  Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Anaclet Malindisa alithibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo. Hata hivyo, alisema ni mapema kueleza sababu za kukamatwa kwake hadi hapo mawasiliano yatakapofanyika.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  [h=4]Comments [/h]


  0 #10 am Proud Mzanzibari 2011-10-09 02:04 Ndio kwanza nione leo mbunge wa ccm ku[NENO BAYA] mbaroni,au anataka kutengeza jina,ccm kwishaaa huna jambo wewe,sizani kama habari hizi ni za ukweli,
  Quote

  +1 #9 KUDOSI 2011-10-08 22:26 Wanaacha kuwakamata akina Rage, Bulaya na Aeshi wanakamata mtu anayetetea maslahi ya walalahoi. Hivi ni lini Polisi Tanzania watafanya kazi kwa kufuata maadili, sheria na kanuni za jeshi? Kwanini wayumbishwe na Magamba?
  Quote

  +1 #8 KUDOSI 2011-10-08 22:20 Huyo mbunge ni CCM wenyewe wanamwandama kwa sababu ya kuwa upande wa wananchi kudai shamba lao la Mbarali lililochukuliwa na gabachori. Magamba na polisi wako upande wa hilo gabachori.Hakuna kazi nzuri walioifanya polisi, wanatumiwa tu na hilo gabachori na Magamba.
  Quote

  0 #7 Nayungi 2011-10-08 15:57 Polisi fanyeni hivyohivyo na kwa sisiem maana mlizidi kuwaandama wabunge wa upinzani
  Quote

  +1 #6 kidongoi 2011-10-08 10:11 Mchimba kisima hutumbukia mwenyewe! CCM kumbukeni mtoto akimtukana baba yake mzazi anatoa nafasi kwa watoto wengine kumtukania baba yake! Mmeshusha wenyewe hadhi ya ubunge ngoja laana iwarudi! Asante polisi wa Mbeya! Mwanawane bado Rage kwani hamkumuona na pisto hadharani? Polisi Tabora vipi?
  Quote

  0 #5 SYLVIA 2011-10-08 08:08 Quoting mzalendo:
  Kamata kamata ya wabunge ni mradi wa nani? huyu nae spika katoa idhini ya kukamatwa kwake au lah? kazi ipo BORA wa CCM NAE KAKAMATWA ILI AONJE CHUNGU WALIONJA WABUNGE WENZAKE.tena asote ndani kama wiki hivi sio anakaa masaa.tuone kama litakwepo tamko la CCM kulaani udhalilishwaji wa mbunge wao.mwandishi wa habari hii kaacha maswali mengi kwani habari yake haijakamilika afanye uchunguzi kama spika alitaarifiwa kusudio la kumkamata na pia angejumuisha habari kama alietishiwa kasemaje.​
  akiwa bungeni ndo spika anatarifiwa vinginevyo anakamatwa kama wengine akifanya kosa eti apigiwe sim yeye ni nani? kama ni kiongozi kwani hao wa chadema sio viongozi? aache kudhalilisha jeshi tena akome kusema hivyo?
  Quote

  -1 #4 KENGE 2011-10-08 07:55 HONGERA POLISI-MBEYA KWA KAZI NZURIIIIII!
  Quote

  +1 #3 Kasim 2011-10-08 07:47 WAKUPIGIE SIMU WEWE NI NANI MWENYE SIMU YAKO?.... UMESAHAU MBOWE ALIKAMATWA KWA STAILI HIYO HIYO, AU KWA VILE UPO CCM UKADHANI UTAPEWA SPECIAL TREATMENT?.... NENDA HUKO SELO, UTAWALA WA SHERIA UNARUDI TARATIBU POLISI.
  Quote

  -1 #2 joseph Masanja 2011-10-08 01:35 Kamanda wa polisi mbeya safi sana asitoke ndani huyo kufilia humo ndani maana ccm haina maana hata siku moja safi sana unatakiwa kuwa mkuuwa polisi tanzania kuanzia leo
  Quote

  -1 #1 mzalendo 2011-10-08 01:30 Kamata kamata ya wabunge ni mradi wa nani? huyu nae spika katoa idhini ya kukamatwa kwake au lah? kazi ipo BORA wa CCM NAE KAKAMATWA ILI AONJE CHUNGU WALIONJA WABUNGE WENZAKE.tena asote ndani kama wiki hivi sio anakaa masaa.tuone kama litakwepo tamko la CCM kulaani udhalilishwaji wa mbunge wao.mwandishi wa habari hii kaacha maswali mengi kwani habari yake haijakamilika afanye uchunguzi kama spika alitaarifiwa kusudio la kumkamata na pia angejumuisha habari kama alietishiwa kasemaje.
  Quote  Refresh comments list
   
 3. only83

  only83 JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Wamezoea.....na ndio maana kutembea na silaha kwao sio tatizo.
   
 4. tikatika

  tikatika JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,669
  Likes Received: 2,198
  Trophy Points: 280
  Natamani akamatwe Makinda labda ndio watajua wao ni VIP ! Safi Sanaa mlishangilia kukamatwa wabunge wa upinzani nanyi onjeni joto!
   
 5. N

  Njopa Senior Member

  #5
  Oct 9, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Sio polisi hii!!!! Atakuwa amekanyaga maslahi ya wenye chama ccm, ccm ina wenyewe
   
Loading...