Mbunge wa bahi matatani tena kwa kashifa ya rushwa

Mbunge wa bahi matatani tena kwa kashifa ya rushwa

Mlengo wa Kati

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2011
Posts
2,730
Reaction score
492
Ripoti yamhusisha na ufisadi
Mfuko wa Jimbo
Kamati ya Uhakiki wa Fedha za
Mfuko wa Jimbo la Bahi Mkoani
Dodoma iliyoundwa na Baraza la
Madiwani wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bahi, imemtia hatiani na
kumuweka katika wakati mgumu Mbunge wa jimbo hilo, Omary
Badwel, baada ya kubaini
amehusika katika ubadhilifu wa
mamilioni ya fedha za mfuko huo.
Kutokana na hali hiyo, kamati hiyo
imependekeza Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo kumchukulia
hatua Mbunge huyo pamoja na
kutakiwa kurejesha mamilioni ya
fedha anayodaiwa kuhusika
kuzifuja.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Julius Chitojo, jana alisema fedha
anazotakiwa kuzirejesha Mbunge
huyo ni pamoja na Sh. 2,750,000
alizozipokea msaidizi wake Sh.
1,950,000 ambazo zilitokana na
wananchi kuuziwa majembe kwa bei ya juu, Sh. 5,440,000 za
majembe 32 ambayo
hayakuwafikia walengwa na Sh.
milioni 4.3 ambazo hazijapelekwa
kwenye vikundi.
Chitojo ambaye pia ni diwani wa kata ya Zanka, alisema kuwa
kamati hiyo imebaini kuwa
wananchi walidanganywa kwa
kuuziwa majembe hayo kwa madai
kuwa ni aina ya Chapa Zimbabwe
wakati yana Chapa ya Jogoo. Alisema kamati yake ilibaini kuwa
majembe hayo yaliuzwa kwa
wananchi kwa bei ya juu kuliko
ilivyokubaliwa na kamati ya mfuko
wa jimbo.
“Tumebaini kuwa makusanyo ya fedha kutokana na mauzo ya
majembe hayajarudi halmashauri
ili wananchi walio wengi waweze
kunufaika na mfuko huu wa
jimbo...badala yake fedha hizi
zimechukuliwa na Said Kayumbo kwa maelekezo kuwa
anampelekea Mbunge Badwel,”
alisema.
Alisema baadhi ya wananchi
wamepata mgawo wa majembe ya
bure wakati wengine wameuziwa na pia fedha za vikundi ziliingizwa
katika akaunti ya Jumuiya ya
Akiba na Maendeleo Bahi
(Basada) kinyume cha utaratibu na
hadi kufikia Oktoba 30, mwaka
jana fedha za vikundi tisa zilikuwa hazijawafikia walengwa.
Aliongeza kuwa fedha za mchango
wa kusafisha kisima cha maji
katika kijiji cha Chibelela
zilichukuliwa na Mbunge huyo
Januari na Februari, 2013 na hazikurejeshwa.
Alisema Sh. milioni 1.7
zilizochangwa na wananchi wa
kijiji cha Chibelela kwa ajili ya
mradi wa maji wa kijiji hicho
zilichukuliwa na mbunge. Aliongeza kuwa wananchi
walidanganywa kwa kupewa
stakabadhi za ada ya kujiunga na
Basada badala ya kupewa
stakabadhi za ununuzi wa
majembe na kusema kuwa hiyo ina ashiria kuwaibia wananchi na
halmashauri. “Mbunge ndiye aliyewapa kazi
Basada ya kukusanya fedha za
majembe na alikuwa akiongozana
nao kwenye mikutano mbalimbali
ya kukabidhi majembe...pia
wananchi wauziwe majembe kwa nusu bei ya jembe itakayokuwa
sokoni kwa kipindi hicho ambapo
ilikuwa ni Sh. 110,000 kwa jembe
moja wakati yalinunuliwa na
halmashauri kwa Sh. 170,000,
hivyo wananchi walipashwa kutoa Sh. 85,000 na siyo Sh. 110,000,”
alisema diwani huyo.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa
kamati hiyo ilibaini kuwa majembe
yaliyosambazwa ni 85 yenye
thamani ya zaidi ya Sh. milioni 14.4 kati ya 78 yaliyouzwa kwa
Sh. 110,000 ambayo ni sawa na
Sh. milioni 8.5.
Alisema wakati wa uchunguzi wa
suala hilo, kamati ilikumbana na
changamoto mbalimbali katika ukamilishaji wake katika kupata
mawasiliano na baadhi ya
walengwa yalikuwa magumu hali
iliyosababisha kutumia muda
mrefu kuwapata.
Alisema mbunge huyo alipoitwa na kamati kujitetea kuhusiana na
kuhusika katika suala hilo alikataa
kutoa maelezo yake kwa
maandishi.
“Kutokana na uhakiki huu, kamati
imebaini ya kuwa ni kweli matumizi ya fedha za Mfuko wa
Jimbo hayapo sawa sawa, hivyo
kamati hii inatoa maoni kuwa
baraza lichukue hatua stahiki dhidi
ya Mbunge pamoja na kurejesha
fedha Sh. 2,750,000 alizozipokea msaidizi wake Sh. 1,950,000
ambazo ni ziada ya bei
iliyokubaliwa Sh. 4,440,000 za
majembe 32 hayajawafikia
walengwa na Sh. milioni 4.3
hazijapelekwa kwa vikundi,” alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha, kamati hiyo iliitaka Basada
kurejesha fedha za halmashauri
ambazo walizikusanya na
kuzitumia kiasi cha Sh. milioni
4,180,000 pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria
kwa kutoa risiti ambazo hazikuwa
za ununuzi wa majembe na pia
fedha za mfuko wa jimbo zitolewe
kama ruzuku na siyo mkopo.
Katika ripoti hiyo yenye viambatanisho mbalimbali
ambavyo vinadhihirisha fedha hizo
kupokelewa na mbunge pamoja na
msaidizi wake Kayumbo zikiwa
zimesainiwa na kuandikwa kwa
mkono. BADWEL AZUNGUMZA Badwel kwa upande wake alisema
inawezekana kuwa kuna tatizo
katika mfuko huo na kudai kuwa
yaliyopo katika ripoti hiyo mengine
ni ya kweli na mengine siyo ya
kweli. “Katika ripoti hii sijaona sehemu
ambayo mimi nilitoa majembe na
katika mzunguko huu na mimi
nilipeleka majembe 58 kwa ajili ya
wananchi wangu, mimi nadhani
mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni...Mbona nimetoa
orodha ya vijiji ambavyo nimetoa
majembe yaliyotolewa kwa Mfuko
wa Jimbo na mengine ambayo
siyo ya mfuko,” alisema Badwel
na kuongeza: “Lazima nitendewe haki kwani
sikushinikiza aina ya majembe na
huu ni mwaka wa tatu tangu
majembe ya Mfuko wa J imbo
yanatolewa kwa Sh. 100,000.
Mimi nilipoulizwa kuhusu fedha zilizotolewa kwa vikundi nilisema
fedha zote zimetolewa na zimefika
katika vikundi, nashangaa hapa
kwenye taarifa haijaelezwa, vitu
nilivyovisema havijatolewa, vitu
vimepangwa na kamati,” alisema na kuongeza:
“Sasa mimi nitasema nini kuna
vikundi vitatu kweli hatujavipa
fedha kwa sababu vilikuwa na Sh.
milioni moja kila kimoja kutoka
maendeleo ya jamii, hii taarifa haijanitendea haki, imejaa siasa
imenidhalilisha ili nijiuzulu, lakini
leo nasema hajiuzuru mtu na hii
haijafanywa leo, imeanza tangu
nikiwa mwenyekiti wa halmashauri
na nilijiuzulu.” Alisema kuwa anamshukuru
Mungu kwa yote anayofanyiwa
katika halmashauri hiyo na
kuonekana katika nafasi yake ya
ubunge hana nafasi hata akienda
kukabidhi majembe inakuwa nongwa.
“Mimi nimeenda kukabidhi kama
mwanasiasa Chibelela,
niliwahamasisha kila wiki
wakachanga fedha na kunikabidhi
kwani tulikubaliana watoe Sh. milioni mbili na mimi ni niongeze
milioni mbili na halmashauri
inajua,” alisema.
“Safari hii hajiuzulu mtu na mtu
kama ana matarajio ya ubunge
afute, maana kuna watu wanaota tu ubunge, watu hawatoki hivyo
alisema na kuongeza:“Mjinga ni
kwenda tu, lakini wakati wa kurudi
siyo mjinga, yaliyotokea ni ya
kupandikizwa tu.”
Baada ya kuwasilishwa ripoti hiyo, ulitokea mvutano miongoni mwa
madiwani huku baadhi wakidai
kuwa wanataka kujua kanuni na
taratibu za fedha za Mfuko wa
Jimbo na wengine wakitaka ripoti
hiyo ipelekwe kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) ili uchunguzi wa
kina ufanyike kuwabaini wote
waliohusika na kuchukuliwa hatua.
Sakata la Mbunge huyo liliibuliwa
mwishoni mwa mwaka jana na Diwani wa Kata ya Lamaiti, Donald
Mejitii, alipowasilisha hoja binafsi
iliyomhusisha Badwel kudaiwa
kutumia vibaya fedha za mfuko wa
jimbo.
Fedha hizo zilitolewa kwa vikundi, ununuzi na usambazaji wa
majembe ya kukokotwa na
ng’ombe kwa kipindi cha Aprili
mwaka jana.
Badwel pia anakabiliwa na kesi
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam
ya kushawishi na kuomba rushwa
kutoka Halmashauri ya Mkuranga,
Mkoani Pwani alipokuwa Mjumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC)
 
Mbunge jimbo la Bahi(CCM) anakabiliwa na Kashifa ya rushwa kwa kuanzisha vikundi hewa vya kukopesha na kuchukua hela za mfuko wa jimbo! Tayari Takukuru imemkamata Msaidizi wake na mpaka sasa yupo rumande kituo kikuu cha Polisi Mkoani Dodoma,ikumbukwe Mheshimiwa Baduel mpaka sasa anaendelea na kesi mahakama ya kisutu akituhumiwa kuomba rushwa kwa alie kua mkurugenzi wa halmashauri ya Mkurugenzi wa Mkuranga. Mbunge huyo bado hajakamatwa kwa sasa ana hudhulia vikao vya kamati vya bunge jijini dar es salaam.

Anataka achukue chake mapema
 
cha ajabu nini hapo kwa chama cha masogange!?
 
MBUNGE wa Jimbo la Bahi(CCM), Omary Ahmed Badwel(43) akiwa chini ya ulinzi wakati alipofikishwa .jpg
 
Bahi kuna uranium.... ushanfahamu?
Mie ningehama jimbo
 
huyu bwana na mbunge wa viti maalum Mbeya watakuwa na pepo wa wizi.
 
Mbunge jimbo la Bahi(CCM) anakabiliwa na Kashifa ya rushwa kwa kuanzisha vikundi hewa vya kukopesha na kuchukua hela za mfuko wa jimbo! Tayari Takukuru imemkamata Msaidizi wake na mpaka sasa yupo rumande kituo kikuu cha Polisi Mkoani Dodoma,ikumbukwe Mheshimiwa Baduel mpaka sasa anaendelea na kesi mahakama ya kisutu akituhumiwa kuomba rushwa kwa alie kua mkurugenzi wa halmashauri ya Mkurugenzi wa Mkuranga. Mbunge huyo bado hajakamatwa kwa sasa ana hudhulia vikao vya kamati vya bunge jijini dar es salaam.
duchi
Haya soma hapa uone hiyo gvt unatoitetea inafanya madudu gani.
 
Last edited by a moderator:
Baduweri.



Anapenda rushwa sana kila uchao ni % tu.


Mary Mwanjelwa


Mtaalam wa kuiba mataulo Hotelini
Juzi uzi ulisema kaiba mkufu wa dhahabu Ughaibuni halafu akakimbia haraka


Hawa hawakutakiwa kubembelezwa katika haya
wayafanyayo ni Ccm tu wanawalea kiaina.
 
huwezi kuwa mwanaccm kama siyo mwizi ! Kumbuka kwamba kuitumikia ccm tu inakupelekea moja kwa moja kumkiri mwovu shetani .
 
huwezi kuwa mwanaccm kama siyo mwizi ! Kumbuka kwamba kuitumikia ccm tu inakupelekea moja kwa moja kumkiri mwovu shetani .

Kweli kabisa. CCM haikupi cheo kama ww sio mwizi,jangili,muuza unga,mla kucha za watu, fisadi, au malaya aliyekubuhu
 
Huyo hashirikiani na wenzake, anataka kupata peke yake ndiyo maana analengeshwa
sina hakika na ulichokipost, tuko hapa kwa kutetea maslai ya Taifa, huo mfuko wa jimbo pesa zinawekwa almashauli husika, na mbunge ni msimamizi mkuu akisaidiana na mkuu wa wilaya, tunaomba kujua Bety Mkwasa anatambua ubadhilifu huu? na kama anatambua amechukua hatua gani? wilaya ya bahi haina ata mochwari kama kunapesa wanakopesha kwanini asijenge mochwari? acheni kukidhalilisha chama Tawala.
 
Kweli kabisa. CCM haikupi cheo kama ww sio mwizi,jangili,muuza unga,mla kucha za watu, fisadi, au malaya aliyekubuhu
kweli kamanda hayo yote uliyoyapost yanamuhusu Lema, Wenje, Mbowe, Lwakatare, Sugu na Nasari, Dr Willbrod Slaa kwa kutokana na hayo maneno ulivyoyapost.
 
Back
Top Bottom