PreGE2025 Mbunge Sophia Mwakagenda aitema CHADEMA, Ajiunga rasmi na CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Sophia Mwakagenda, ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM), akisema uamuzi huo unalenga kuendeleza jitihada zake za kuwatumikia wananchi kwa ufanisi zaidi.

Akizungumza mbele ya mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Bulyaga iliyopo Tukuyu, mkoani Mbeya, ametumia nafasi yake kuwaaga wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akikipongeza kwa kumlea na kumjenga kisiasa tangu aanze safari yake ya uongozi.

“Ninashukuru CHADEMA kwa malezi na mafunzo ya kisiasa niliyoyapata, kuanzia saa tano asubuhi ya Juni 28, 2025, nitajiunga rasmi na CCM ili kuendelea kuhudumia wananchi,” amesema Sophia.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Hata hivyo, Mwakagenda bado hajafichua kama atawania Ubunge wa Jimbo la Rungwe katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Mwakagenda ni miongoni mwa wabunge 19 wa Viti Maalum waliovuliwa uanachama na CHADEMA. Katika uchaguzi wa mwaka 2020, aliwania Ubunge wa Jimbo la Rungwe kupitia tiketi ya CHADEMA, akichuana na mbunge wa sasa, Antony Mwantona wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
 
Amejazwa ujinga kwamba hamia huku ili kuhamisha attention ya wanachama wa CHADEMA kwa ahadi ya kuteuliwa kugombea kiti cha ubunge kupitia ccm hapo Oct,atakuwa surprised pale hata kuingia vikao vya kamati kuu kushiriki uchaguzi wa ndani atatemwa.

Ccm ukiwa mgeni siyo wa kuwaamini hata kidogo akamuulize Ndugai anaielewa hiyo michezo.
 
Waandishi wetu bwana, sasa kaitema au alitemwa kitambo tu katangaza tu bwana anayemtumikia tu tangu alipotemwa na sio kitu kipya! Eti akatumikie wananchi yani makada wa sisiemu waliojipanga foleni wanasubiri ndo waje wamuachie ubunge, hapo ndo ishatoka hiyo akatumie fungu lake kuanzisha biashara maisha yaendelee, jiwe mnunuzi wa wanasiasa hayupo tena sadly!
 
Waandishi wa kutumwa hao
 
Kwa wanaomjua ni chawa tangu tumboni mwa mama yake mke wangu.
 
Huyu Alifukuzwa Chadema pamoja na Halima Mdee na wenzake

View attachment 3320168

Hata hivyo hatoondolewa Bungeni na atalipwa hela za umma zote za mafao
Bunge linavunjwa tarehe 27 Juni, kesho yake anajiunga rasmi na CCM. Angeweza tu kusema kuwa hatagombea tena na mara baada ya kuvunjwa Bunge ndio akajiunga na CCM. Anafanya hivi kuwaonyesha CDM kuwa hamna kitu wanachoweza kumfanya. Lakini pengine bila kujua anashusha heshima ya Bunge.

Amandla...
 
🤣🤣Kaona aage mashindano Kash Kash hazitaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…