Mbunge Nyalandu yuko wapi?

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,295
Wanajanvi,

Japokuwa vikao vya Bunge serikali imedai hawataweza kutuonyesha live kutokana na ufinyu wa bajeti lakini wameamua kutuonyesha kiduchu.

Naomba kuuliza je aliyekuwa Waziri wa Mali Asili na Utalii kwenye awamu ya Kikwete yuko wapi? Bungeni haonekani au naye ana adhabu kama wabunge kama kina Tundu Lisu?

Nawasilisha!
 
Kwani umefuatilia bunge ukabaini kwamba hayupo bungeni au umeanzisha Uzi baada ya kummiss ghafla?
 
File lake kwa dpp linasubiriwa kupelekwa mahakamani baada ya rais kuwa mwenyekiti wa chama
 
Wanajanvi Japokuwa vikao vya Bunge serikali imedai hawataweza kutuonyesha live kutokana na ufinyu wa bajeti lakini wameamua kutuonyesha kiduchu, naomba kuuliza je aliyekuwa waziri wa Mali Asili na utalii kwenye awamu ya Kikwete yuko wapi? Bungeni haonekani au naye ana adhabu kama wabunge kama kina Tundu Lisu?

Nawasilisha!
Mkuu usidanganyike kuwa bunge kutoonekana live ni ufinyu wa bajeti, la hasha! Wamekataza hata media binafsi zilizo kuwa tayari kurusha mijadala ya bunge!.
 
Nyalandu hakuwahi kuwa na muda bungeni alikuwa anaonekana pale tu bajeti ya wizara yake inaposomwa, yuko busy kuwinda tembo na kuingia ubia wa kumaliza rasilimali zetu na wazungu.
 
Anamalizia kwanza kukusanya madeni aliyoyaacha kwa waarabu then atarudi bungeni
 
Nyalandu ana duo citizenship, mara nyingi yupo Marekani nchi yake ya moyo, Tanzania huja kwa biashara aidha ya siasa au utalii. Usicheze na diaspora.

Hivi Tanzania tuna duo citizenship sivyo...

Maneno ya kijiweni matamu sana buraza....:D:D:D:D
 
Nyalandu kapiga mihela sana enzi zake mpaka akajisahau akaanza kujiona mungu-mtu.

Haamini u-turn iliyotokea mpaka kufikia hatua ya kuanza kuuliza maswali ya nyongeza bungeni.

Amejificha America wa sasa, mwezi ujao anaburuzwa mahakamani, mahakama yetu ile ikianza kazi.
 
Mbunge mzigo, jimboni kwake hakuna hata moja la kujivunia alilolifanya kwa miaka 16 ya ubunge wake, sekta zote ni hovyo, barabara toka singida mjini kwenda ILONGERO na MTINKO imeshindikana kabisa, huu ndio mwisho wake kisiasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom