Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,896
MBUNGE wa Ludewa mkoani Iringa, Deo Filikunjombe amejitolea kuwalipa mishahara waganga wa zahanati mbili za Kilondo na Lifuma jimboni humo ili kusogeza huduma ya afya kwa wananchi wa maeneo hayo. Ahadi hiyo imekuja siku chache baada ya Mbunge huyo kutumia Sh milioni 90 alizokopeshwa kwa ajili ya kununua gari la ubunge, kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake jimbo humo. Kwa kupitia fedha hizo, Filikunjombe aliyesema hahitaji gari jipya katika kipindi hiki ambacho wananchi wake wanasumbuliwa na kero nyingi; hivyo alinunua gari la wagonjwa lenye vifaa vya kisasa, trekta kubwa la kulimia, mabati, saruji na vifaa mbalimbali vya michezo na kuwakabidhi wananchi wake hivi karibuni.
Juhudi zote za Halmashauri yetu ya Wilaya ya Ludewa za kumpata mganga kwa ajili ya Zahanati ya Kilondo zilishindikana. Safari hii nilipokwenda kuwatembelea nimewatafutia mganga, alisema Filikunjombe. Alisema ametafuta mganga kwa ajili ya Zahanati ya Lifuma ambao kwa pamoja na yule wa Kilondo, atabeba mzigo wa kuwalipa mshahara mpaka pale Halmashauri itakapobeba jukumu hilo. Alisema watumishi wa afya wamekuwa wakikataa kwenda kufanya kazi katika maeneo hayo kwa kisingizio cha mazingira magumu na kwamba katika kipindi chake chote atakachokuwa mbunge wa jimbo hilo, hatakuwa tayari kuona watu wake wakifa kwa kisingizio hicho.
Nipo tayari kuwalipa mishahara mizuri ili mradi watu wangu wafikiwe na huduma stahiki za afya kama ilivyo kwa watu katika maeneo mengine, alisema. Alisema anayafanya hayo yote huku akiamini kwamba muda wa wanasiasa kuendelea kulumbana umekwisha, na wanachotakiwa kufanya ni kutekeleza ahadi walizowaahidi wananchi wao. Alivitaja vipaumbele vyake vikuu katika kipindi cha miaka mitano ya ubunge wake kuwa ni kuhakikisha barabara ya Ludewa - Njombe inajengwa kwa kiwango cha lami na miradi ya makaa ya mawe na chuma cha Liganga inaanza kufanya kazi.
Source" Habari Leo