JAMHURI
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 449
- 60
Mbunge wa Jimbo Kiteto, Emmanuel Papiani, amekitaka kikosi cha kupambana na rushwa PCCB kuingilia kati kubaini wizi wa fedha za wananchi kiasi cha mil 7 zilipo.
Mhe Papiani aliyesema hayo wakati akizungumza na baraza la madiwani kuwa miradi ya maji mingi inasuasua kutokana na wizi unaofanywa na wasimamizi.
Alitolea mfano wa mradi wa maji Kijiji cha Kijungu Wilayani Kiteto kuwa zimeliwa kiasi cha mil 7 na hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi ya kuhamishwa mtendaji wa kijiji mara kadhaa kutaka kupoteza ushahidi
Alisema ili kukomesha vitendo hivi kikosi cha kupambana na Rushwa Takukuru Kiteto kifike na kujionea hali ilivyo kisha sheria ifuate mkondo wake.
Baadhi ya wananchi wa Kijungu hicho walisema, pamoja na kuwa na kisima cha maji bado wanatatizo la usimamizi wa fedha kwani kinapo haribika hupata taabu kurejesha huduma hiyo..