Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,549
Wasalaam wapenzi wa jukwaa hili!
Ndugu zangu huwa napata ukakasi sana ninapoona mtu ambaye anaonekana anajiita msomi lakini anyoongea hayana reflection na usomi wake. Tena kijana ambaye nafikiri kesho angeweza kua Key figure kwenye ujenzi wa taifa. Ndugu yangu bwanamdogo Jery Slaa ni mpotoshaji mkubwa sana kuhusu ATCL, Sijui ni kujikakamua aonekane kwamba anajua au anatafuta sifa za kitoto.
Kwa haraka haraka nimshauri ndugu yangu Jerry Silaa kama hana uelewa na masuala ya biashara na uchumi akae kimya hata kama baba yake alikua rubani, kua rubani hakukufanyi wewe kua mtaalamu wa biashara za ndege.
ANAVYOPOTOSHA BUNGE
Msomi mzima huwezi kusema kuwa hakuna tatizo kusikia shirika miaka 10 mfululizo linapata hasara ya mabilioni ya shilingi ukafurahia ati kwa sababu ni kawaida kwa mashirika ya ndege kupata hasara, kwahiyo wananchi waendelee kukosa miradi ya maji na madawa kwa sababu kuna shirika limegeuka kua mchwa wa kumaliza pesa?
Jery anapotosha kua hasara ya ndege zetu ni kwa sababu ya COVID-19, haelewi na wala hakumbuki kwamba kua ugonjwa huu ulianza mwaka 2019 mwishoni, inahusiana vipi na hasara ya miaka ya nyuma? Huyu mtu wa aina hii tumpe jina gani?
USHAURI UNAWEZA KUMSAIDIA NDUGU HUYU NA WATU WENGINE WA AINA YAKE
Kanuni zote za kibiashara duniani hua zinataka mradi wowote katika taifa lolote lile ufunguliwe ikiwa kuna economic stability katika taifa. Una bajeti yako ndogo katika taifa halafu unachukua sehemu yake unaaanzisha mradi ambao utakuingizia hasara tena irudi kuendelea kufidia hasara ile ile kwa bajeti ile ile ndogo, hivi hii ni kitu gani kama siyo kuumiza wananchi ambao ndio walipa kodi?
Huwezi kufurahia hasara miaka mitano mfululizo ati inafufua shirika wakati unajua kabisa kua shirika lina madeni kibao, yaani unataka upae angani unapata hasara halafu bado una madeni yanazidi hata hiyo hasara unayopata, ni lini utapata faida kama utaendekeza mawazo haya ya kina Jerry Slaa?
Kama tulikua tunajua kua shirika lina madeni megi, basi tungeweza kumalizana nayo kwanza na kuweka sawa mikataba ya kimataifa lady ndio tuje tuanze kufanya maboresho ya shirika letu ili hata tunapopata hasara lakini wakati wa kuifidia kusiwe na maumivu makubwa. Au tungesibiri uchumi wetu utengamae ili tuweze kulisafisha shirika halafu tuanze na mtaji wetu wa hizo ndege huku kwenye anga la kimataifa hatuna tatizo.
Huwezi kufananisha hasara ya Shirika la ndege la Ethiopia, Kenya, Qatar au South Afrika wakati uchumi wao una ahueni wanaweza kufidia hasara hiyo.
Ifike mahali tuwe wakweli tuache kujipendekeza pendekeza ili kulisaidia taifa, unafki haujengi na hauna msaada wowote kwenye ustawi wa taifa pia. Tuwe wazalendo kama kuna hasara tukubali kua ni tatizo na ni lazima litatuliwe.