Mbunge huyu hatufai

hizo picha nadhani zimekufunga mdomo. ulitaka aje akulimie bustani.......................wewe
 
Join Date : 30th April 2012
Posts : 1
Rep Power : 0
Likes Received0
Likes Given0
ipo haja kuwascreen hawa wageni kabla ya kuanza kupost wawe wachangiaji kwanza.
 
Duu huyu mtu harudi humu na akirudi lazima aje na jina lingine maana amesharudisha kadi ya CCM.
 
Ama hakika uwezo wa kufikiri wa chama cha magamba inaonekana umetoweka kabisa! Namshangaa sana huyu ndugu anajiita wambuni kwa kutoa taarifa za kuonyesha mhe. Mchg. Peter s msigwa hafai kwa madai amekuwa akidai ana majukumu ya kitaifa, lakini naomba kukukumbusha mambo kwa uchache tu yaliyofanywa na mhe. Msigwa na ambayo hayajawahi kufanywa na mbunge yeyote wa ccm katika historia ya jimbo hili 1. Aligawa jenzi kwa timu 30 ndani ya manispaa ya iringa 2. Alitembelea magereza na kula chakula na wafungwa ikiwa ni pamoja na kujua matatizo yanayowakabili 3. Aligawa vyandarua zaidi ya 100 katika hospitali ya mkoa 4. Alitoa fedha milioni 30 kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa nduli 5. Alitoa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya milioni 100 katika hospitali ya wilaya iliyopo maeneo ya frelimo mjini iringa kama vile vitanda vya kisasa vinavyotumia rimoti, wheel chairs n.K. 6. Ametembelea na kuchangia saccoss mbalimbali ndani ya manispaa ya iringa 7. Ametembelea na kutoa misaada mbalimbali kwenye vituo vya watoto yatima. 8. Amemuweka mwanasheria katika ofisi yake anaepatikana kila siku ya ijumaa kwaajili ya kutoa ushauri kwa wananchi juu ya mambo ya kisheria! Haya yote ameyafanya ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tu. Je, ni mbunge gani wa ccm kayafanya haya mpaka sasa? Acheni ushabiki usiokuwa na maana, kwa maendeleo ya jimbo letu msigwa ni chaguo sahihi! Narejesha kwa wana jf.
 
Mbunge wa Iringa mjini hafanyi kazi za wananchi kila siku anasema anafanya kazi za kitaifa sisi wananchi tulio mchagua tukiamini mageuzi inatufedhehesha.

Mnaambiwa kila siku kuwa uzushi hauwezi kuwasaidia. Kwani si kila mara mnazusha lakini mnazidi kupewa za uso mfululizo?
Hebu tupe tathmini ya zile ziara za mawaziri wenu kuelezea wananchi uzuri wa bajeti ya mwaka ulee!
 
ama kweli msigwa ni jembe,big up baba mchungaji.natamani msigwa ndio angekuwa mbunge jimboni kwangu,kule mwanga kilimanjaro
 
Ni kweli mbunge anachaguliwa kuwakilisha wananchi wa eneo mahsusi.
Lakini Mbunge makini & mahiri anatarajiwa kushughulikia masuala ya kitaifa, ikiwemo kutembelea maeneo mbalimbali nchini.
Tunapokuwa na mbunge dhaifu lakini anayewakilisha eneo lenye maslahi ya taifa, lenye madini ama rasilimali zingine unataka wabunge wote wanyamaze kwa kuwa 'hayawahusu'?
Bajeti ya Wizara ya Fedha & Uchumi ijadiliwe kwa mtazamo wa eneo mahsusi?
Sheria na mikataba mbalimbali ya kimataifa unataka ijafiliwe kwa mtazamo wa wananchi wa eneo fulani tu?
Jibu umeshapata.
 
Akili ya lukuvi kizazi cha magamba,shemeji ya mwigulu mjukuu wa chiligati
Mbunge wa Iringa mjini hafanyi kazi za wananchi kila siku anasema anafanya kazi za kitaifa sisi wananchi tulio mchagua tukiamini mageuzi inatufedhehesha.
 
hATA HII NI KAZI YA KITAIFA HUYU JAMAA AJUE KILA KAZI YA JIMBO NI YA TAIFA WATAKAO NUFAIKA NI WATANZANIA SIO ENEO HILO LEO ATALAZWA HOSPITALINI MTU KUTOKA MKOA MWINGINE
 
Mbunge wa Iringa mjini hafanyi kazi za wananchi kila siku anasema anafanya kazi za kitaifa sisi wananchi tulio mchagua tukiamini mageuzi inatufedhehesha.

kwa uthibitisho niliouona hapo juu.. naomba nikuase ndugu yangu uwe unachamba hata mara moja moja!
 
Join Date : 30th April 2012
Posts : 1
Rep Power : 0
Likes Received0
Likes Given0

Sikushangai, kumbe umezaliwa jana alafu leo tuu unapiga kelele, alafu umeingia JF hata bila hodi, duh, kilaza mkubwa wewe.

Huyo ni msukule...Asome na hii
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) Mchungaji Peter Msigwa atenda miujiza mikubwa kwa wapiga kura wake wa jimbo la Iringa mjini baada ya kumwaga misaada ya mamilioni ya shilingi kwa ajili ya Hospitali mpya ya Manispaa ya Iringa.Wengi washikwa bumbuwazi wadai haijapata kutokea kwa mbunge wa jimbo hilo la Iringa mjini kumwaga msaada wa vifaa kama hivyo .
 
Mbuni hongera kwa kuleta huu umbeya wako, umefanya Rev. Msigwa ajulikane kwa maneno na matendo. Hongera baba mchungaji kazi inaonekana jimboni na kitaifa pia. Wenye wivu.. ...
 
Asome kwenye RED hapo ndio ataelewa maendeleo ni nini kwa jimbo?
MBUNGE wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) amekabidhi vitanda vya kisasa 30 pamoja na magodoro yake kwa ajili ya kusaidia kulalia wagonjwa na Baiskeli za walemavu (Wheel chairs) 19 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya milioni 50 na kuwapon
geza wabunge waliomtangulia akiwemo Monica Mbega (CCM) kwa kazi nzuri.

Akikabidhi msaada huo leo kwa kaimu meya wa Manispaa ya Iringa Victor Mushi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika viwanja vya Hospitali mpya ya Manispaa ya Iringa iliyopo eneo la Frelimo mjini hapa ,mbunge Msigwa alisema kuwa amelazimika kutoa msaada huo kama njia ya kushirikiana na wananchi wa jimbo hilo katika kuboresha huduma za afya.

Hivyo alisema kuwa kwa upande wake ataendelea kufanya mambo ya kimaendeleo zaidi badala ya kutoa fedha za kula kwa mwananchi mmoja mmoja japo ambalo halitasaidia kuharakisha maendeleo ya jimbo hilo la Iringa mjini.

"Kiukweli kama rafiki zangu ninao wengi sana na leo hii nikaamua kugawa fedha shilingi 10,000 kwa kila rafiki yangu kama sehemu ya ahsante kwa kunichagua nitakuwa siwasaidii na njia sahihi ya kuwasaidia rafiki zangu na wapiga kura wangu ni kuwasogezea maendeleo kama hivi....hivi vitanda leo vitatumiwa na wana Chadema, CCM ,CUF ,TLP ,NCCR Mageuzi na wanachama wa vyama vyote na wasio na chama ambapo ni jambo la msingi zaidi kuliko kuwa mbunge wa kugawa fedha za kula...kweli wananchi wangu naomba mnisamehe kama nitawakwaza kwa kufanya shughuli za kimaendeleo"alisisitiza mbunge Msigwa.

Hata hivyo alisema kuwa si kwamba amekuwa akichangia shughuli za kimaendeleo kwa kutumia uwezo na maamuzi yake pekee bali amekuwa akifanya hivyo kwa kuzingatia zaidi mawazo na maagizo ya wananchi waliomchagua kupitia ofisi yake na mikutano mbali mbali ya hadhara aliyopata kuifanya kabla ya baada ya vikao vya bunge na mabaraza ya Halmashauri ya Manispaa.

"Katika mazingira hayo jukumu la mbunge na diwani makini si kuwapoza wananchi kwa kuwapa vijisenti na vizawadi vya kula leo na kumalizika leo ,au kuwadanganya kwamba naweza kuwaletea maendeleo kwa kutumia mshahara wangu wa ubunge ambao sote tunajua kuwa hautoshelezi watu wa jimbo hili ,bali ni kuhudhuria kwenye vikao hivi na kuhakikisha kuwa vinapitisha maamuzi na kutenga fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo yenu ...nashukuru kwa kunielewa kwani wajibu wangu kikatiba ni kuishauri na kuibana serikali kwa manufaa ya maendeleo yetu"

Mbunge Msigwa alisema kuwa mbali ya kukabidhi msaada huo katika Hospitali hiyo ya wilaya ya Iringa mjini kama njia ya kupunguza msongamano katika Hospitali ya mkoa wa Iringa bado amekuwa mbele kuchangia shughuli mbali mbali zikiwemo za michezo na kuona kuwa ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni zinatimizwa kwa wakati ikiwemo ahadi ya kuchangia shilingi milioni 12 kila mwaka kutoka katika familia yake kwa ajili kusaidia watu wenye matatizo .

Akielezea juu ya msaada huo alisema kuwa kila kitanda kimoja kinagharimu zaidi ya shilingi milioni 1.5 wakati baiskeli kila moja ni zaidi ya shilingi 700,000 pamoja na vikabati vya kuhifadhiwa vifaa vya wagonjwa katika mawodi na kuwa msaada huo ameupata kupitia wahisani wake R.T.C.O japo alisema hakupenda sana kutumia kutafuta sifa kwa msaada huo kwa kuweka thamani ya fedha kama ambavyo wanasiasa wengine wanavyofanya.

Pia alitaka wananchi wa jimbo la Iringa mjini mbali ya kusubiri kusaidia na serikali kwa kila jambo bado wanaweza kujitolea kusaidia huduma za afya ,elimu na maendeleo mengine katika maeneo yao na kuwa ofisi yake kuanzia sasa itafanya kazi ya kupokea misaada na michango mbali mbali kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya jimbo la Iringa mjini.

Kwa upande kaimu meya wa Mnaispaa ya Iringa diwani wa kata ya Mtwivila Victor Mushi (CCM) mbali ya kumpongeza mbunge Msigwa kwa msaada huo mkubwa bado alitaka vifaa hivyo kutunzwa zaidi ili kuweza kuendelea kusaidia katika Hospitali hiyo .

Huku kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) alisema kuwa msaada huo utasaidia kupunguza matatizo ya akina mama wajawazito ambao wamekuwa wakipata shida na kuwa tukio hilo la kukabidhi vitendea kazi katika Hospitali hiyo ni tukio la kupongezwa na kuwa katika shughuli za kimaendeleo wanasiasa wanapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja katika kuharakisha maendeleo badala ya kuingiza mivutano ya kisiasa isiyo na tija katika maendeleo ya wananchi

Huku wananchi wa jimbo la Iringa mjini wakiwemo wana CCM na wanachama wa vyama vya upinzani wamepongeza jitihada za mbunge wao Msigwa kwa msaada huo na kutaka wabunge wa CCM kuiga mfano huo katika kuchangia maendeleo badala ya kutoa takrima kwa wapiga kura.

John Kalinga ni mwana CCM mkazi wa Frelimo amesema kuwa wengi walikuwa wakishindwa kumuelewa mbunge Msigwa ila sasa wamemtambua vema kuwa ni mbunge wa kazi katika jimbo hilo na kuwa jitihada hizo zinaweza kuja kuwa mwiba kwa CCM kulichukua jimbo hilo kutokana na mambo ambayo anayafanya kuwa makubwa zaidi ukilinganisha na yale ya CCM.

Huku Sarah Sanga mwana TLP amepongeza jitihada hizo na kutaka wana CCM kuacha kuelekeza mashambulizi kwa mbunge Msigwa badala ya kuelekeza mashambulizi ya kimaendeleo kwa wananchi .
 
Back
Top Bottom