Mbunge Elibariki Kingu alalamikiwa kutukana, kutishia kudhalilisha viongozi wa dini

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Kumekua na malalamiko mengi sana ambayo yanatajwa kukidhalilisha Chama cha Mapinduzi CCM ambayo yanasababishwa na Mbunge wa jimbo la Singida Magharibi Elibariki Kingu.

Tabia hii inatajwa kukifanya chama kuanza kuchukiwa sana katika Jimbo hilo ambapo wananchi wamedai kwamba iwapo CCM watamrudisha tena kugombea kiti hicho 2020 ni bora kutopiga kura kabisa au kukipigia kura chama chochote cha upinzani chenye ushawishi jimboni humo kuliko kuchagua kisima cha matusi na udhalilishaji.

Tabia hii inatajwa kuwakera hata wanaCCM wenzeke ambao kila mara na kutishia kukihama Chama ikiwa viongozi wao wa juu hawamkei na kumuonya.

Mbunge huyu anatajwa kuogopwa na kubebwa na Mwyekiti wa CCM Wilaya ndugu Mika Likapakapa pamoja na katibu wa CCM Wilaya ndugu Pius Sankha.

Kuna ujumbe wa matusi ambao sio vyema kuweka humu kwa heshima ya forum hii umekua ukisambaa kwenye baadhi ya makundi ya Whatapp ukionesha Kiongozi mmoja wa dini ya Kiislam mkoa wa Singida ambaye ni KADHI wa mkoa akimlalamikia Mbunge huyo kwa kumtukana na kunitishia maisha.

Sambamba na hilo kuna viongozi wa kiimani katika Tarafa ya Sepuka nao wanalia na Mbunge huyu kuwatukana na kuwadhalilisha kila mara.
 
Acha umbea sema unataka ubunge sio kupika maneno au kwa sababu yeye sio muislam mmeanza kuja na swaga za anawatukana mbona mkichinjiwa ngombe hapo msktn hamlalamiki sema nae mlimzoea Misanga eeeh

Kijana ana heshima sana kwa wakubwa zake tena hana ubaguzi

Tatizo lake ni ahadi hewaa maneno meengi utekelezaji ghulihee lkn msilete hoja nyepesi za kinafiki
 
Mleta mada kosa la huyo mbunge ni kusema kweli, kwahiyo wewe na waliokutuma mnataka aendelee kuwa na roho ya kishetani kufumbia macho uonevu unaoendelea Tz.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama huelewi kitu kaa kimya.No research no right to speak
 
Mleta mada kosa la huyo mbunge ni kusema kweli, kwahiyo wewe na waliokutuma mnataka aendelee kuwa na roho ya kishetani kufumbia macho uonevu unaoendelea Tz.

Sent using Jamii Forums mobile app
Anatukana viongozi wa dini watu wazima ndio ukweli? Huo ni ukweli upi wa mdomo mchafu hivyo?
 
Back
Top Bottom