MBUNGE CONDESTER Atembelea Eneo Lenye Madini ya Sodalite Kukagua Utafiti Unaoendelea Kijiji cha Chindi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,960
954

MBUNGE CONDESTER Atembelea Eneo Lenye Madini ya Sodalite Kukagua Utafiti Unaoendelea Kijiji cha Chindi

Mbunge wa Jimbo la Momba, Condester Sichalwe (Mundy) ameambatana na Afisa Madini mkazi Mkoa wa Songwe, Chone Malembo, ametumia mtubwi kuvuka mto Nkana kuelekea Kijiji cha Chindi kwenda kujionea utafiti wa madini aina ya Sodalite yanayodaiwa kugundulika eneo hilo

Mhe. Condester Sichalwe (Mundy) amempongeza mchimbaji mdogo wa madini ya Sodalite bwana Nickolaus Buseni kwa kuamua kufanya utafiti wa madini hayo ndani ya Jimbo lake na kueleza kuwa yupo tayari kumuunga mkono, ikiwa ni pamoja na kumkutanisha na taasisi za kifedha ili apatiwe Mkopo

Mhe. Condester Sichalwe (Mundy) amewasihi wananchi wa kijiji cha Ntinga na wana Momba kwa ujumla kuchangamkia fursa ya kupata leseni kwa ajili ya uwekezaji wa madini ya Sodalite ambayo yanadaiwa kugundulika kijiji cha Chindi Kata ya Msangano.

Afisa Madini Mkazi mkoa wa Songwe, Chone Malembo, amesema madini ya Sodalite, ambayo yanafanyiwa utafiti kijiji cha Chindi Kata ya Msangano Wilaya ya Momba, yatakuwa ni madini mapya kupatikana ndani ya Mkoa huo, kwani hakuna eneo lingine ambayo yanapatikana ndani ya Mkoa wa Songwe
Your browser is not able to display this video.
 
Aibu ya mbunge, hata kuweka kivuko cha kuvuta kwa kamba ameshindwa.

Pesa ya mfuko wa jimbo inaishia wapi
 
Mimi naona kwenye huu ulimwengu wa kidigitali kazi ya mbunge haina maana yoyote. Uwakilishi wa wananchi kivipi wakati kila kitu kipo wazi mitandaoni? Kwa mfano mtu wa Arusha anaweza kujua nini kinaendelea Ruvuma... na kama wabunge wakisema wanatunga sheria bado watakuwa wanadanganya kwasababu sheria zinatungwa na wataalamu huku kazi kubwa ya wabunge ikiwa ni kujadili tu vifungu ambapo nako huzipitisha tu. Mimi mbunge wangu aliyeishia darasa la 7 ataweza vipi kung'amua kasoro kwenye muswada ulioandikwa kitaalamu? Wabunge kwa sasa wanatuwakilisha kwenye kufakamia keki ya taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…