Mbunge CCM: Bajeti si yenyewe imechakachuliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge CCM: Bajeti si yenyewe imechakachuliwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, Jun 16, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Dk. William Mgimwa, anadaiwa kusoma hotuba ya bajeti iliyojaa kasoro nyingi, ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa vipengele muhimu vilivyokubaliwa na Kamati ya Uchumi na Fedha.

  Kwa kufanya hivyo, waziri huyo sasa anashutumiwa kwa kuidharau na kukiuka kwa makusudi maagizo ya kamati hiyo yaliyokuwa na lengo la kuiboresha bajeti ili ilete manufaa kwa wananchi.

  Tuhuma hizo nzito zilitolewa jana na mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM), mbele ya waandishi wa habari, na kutangaza rasmi kuipinga bajeti hiyo kwa madai kuwa haina tija kwa wananchi wanyonge.

  Aidha alisema kuwa bajeti iliyosomwa bungeni ilikataliwa na kamati hiyo bungeni kutokana na kubaini kuwa ni mbovu na haikidhi vigezo na malengo ya kumkomboa Mtanzania maskini.

  Mpina ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo, alisema kuwa walimtaka Waziri Mgimwa kwenda kuifumua upya na kufanya marekebisho, lakini serikali imekataa ikitoa sababu na visingizo vingi.

  Kwa kujiamini, Mpina alisema kitendo cha waziri Mgimwa kutojali mapendekezo yao, kimeifanya bajeti hiyo kuonyesha kuwa serikali haina nia njema ya kuboresha maisha ya Watanzania ambao kila siku wanapiga kelele juu ya kuwepo kwa umaskini uliokithiri.

  Mpina alisema kuwa anajua msimamo wake huo, unaweza kumletea matata ndani ya CCM, lakini akadai kuwa yuko tayari kwa lolote hata ikiwa ni kufukuzwa ndani ya chama hicho.

  Mpina alisema bajeti hiyo imejaa upungufu mwingi, ikiwemo kuelekeza fedha nyingi katika matumizi makubwa ambayo siyo ya msingi na kuyaacha mambo ya maendeleo.

  Alifichua kuwa bajeti hiyo, pia imekiuka makubaliano ya wabunge ya utekelezaji wa mpango wa miaka mitano wa maendeleo ambao unalenga kuboresha maisha ya Watanzania ambao wamekata tamaa kutokana na umaskini walionao.

  Mpina alibainisha kasoro nyingine kubwa kuwa ni ukiukwaji wa maagizo ya wabunge ambao waliitaka serikali kuhakikisha kila mwaka wa fedha inatenga sh tirilioni 2.7 kutoka katika fedha za ndani kugharamia miradi ya maendeleo na kutenga asilimia nyingine 35 ya bajeti kwa ajili hiyo.

  Mbunge huyo alisema pia katika makubaliano ya wabunge na serikali yaliyokiukwa katika bajeti hiyo ni kuhakikisha kuwa fedha za umma zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo hazitumiki kwa ajili ya mambo mengine.

  Mpina alizidi kufichua kuwa wakati wa kujadili mpango wa maendeleo wa miaka mitano, aliyekuwa Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo, aliwahakikishia wabunge kuwa mambo hayo yangezingatiwa kikamilifu na fedha hizo zingetengwa kila mwaka, ikianza na bajeti ya mwaka huu.

  "Lakini ukisoma bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Uchumi inaonesha kuwa matumizi ya kawaida yametengewa trilioni 10.5, sawa na asilimia 70, na matumizi ya maendeleo yametengewa trilioni 4.5, sawa na asilimia 30, wakati fedha za ndani zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ni trilioni 2.2 tu, badala ya 2.7," alisema.

  Alisema kitendo cha serikali kutenga trilioni 2.2 badala ya trilioni 2.7 ambayo inaleta tofauti ya sh bilioni 500, iliyoainishwa awali katika mpango wa maendeleo, kimeifanya miradi mingi kutengewa fedha kidogo huku mingine mingi ikikosa fedha kabisa.

  "Kibaya zaidi katika bajeti hii, mapato ya ndani kwa sasa yameongezeka kwa trilioni 1.5, huku matumizi ya kawaida yakipanda kwa trilioni 1.9 wakati fedha za maendeleo zikipungua kwa bilioni 397.8 ikilinganishwa na mwaka wa fedha 2011/12.

  "Hapa inadhihirisha dhahiri kuwa serikali haina nia ya dhati ya kupunguza matumizi ya kawaida," alisema Mpina.

  Mbunge huyo alizidi kusisitiza kuwa wakati serikali ikiendeleza matumizi makubwa yasiyokuwa na tija, Watanzania wengi wanakufa kwa kukosa matibabu kutokana na kukosekana kwa zahanati, dawa na waganga na wengine wakikabiliwa na ukosefu wa maji safi na salama, elimu bora kutokana na upungufu mkubwa wa madarasa na nyumba za walimu.

  Mpina aliongeza kuwa kwa kipindi kirefu serikali imekuwa ikitoa ahadi za kupunguza matumizi ya kawaida ili kuongeza kasi ya utoaji huduma na uwekezaji katika sekta zinazokuza uchumi na kupunguza umaskini.

  Alitoa mfano wa wizara mbili za Nishati na Madini na Fedha na Uchumi ambazo zimejipangia kiasi kikubwa cha fedha kwa matumizi aliyoyaita kuwa si ya lazima.

  Kwa Wizara ya Nishati na Madini, Mpina alibainisha kuwa imejitengea sh milioni 142 kwa mwaka huu wa fedha kwa ajili ya mafunzo ya nje, wakati mwaka jana ilitenga sh milioni 34, hivyo kuwa na ongezeko la milioni 108.

  Wizara hiyo itatumia sh milioni 567 kwa ajili ya mawasiliano, badala ya milioni 71.76 ilizotumia katika mwaka wa fedha 2011/12, wakati katika kile kilichoitwa Kitengo cha Utawala na Mawasiliano kitatumia sh bilioni 2.003 badala ya sh milioni 53.87 za mwaka jana.

  Nayo Wizara ya Fedha na Uchumi imejitengea sh milioni 582.3 kwa safari za wakubwa za ndani, katika Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, wakati mwaka jana ilitumia sh milioni 283, na safari za nje itatumia sh milioni 874,wakati mwaka jana ilitumia sh milioni 532.


  Chanzo: Tanzania Daima
   
 2. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  nimemsikia ITV!
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Bora huyo mbunge kaamua kujilipua na bajeti!
   
 4. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,182
  Likes Received: 10,534
  Trophy Points: 280
  Shkamoo!
   
 5. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kasoma alama za nyakati!
   
 6. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Ukiona mabeki hawaelewani na viungo, ujue kinachofuatia ni kufungwa.
   
 7. m

  man maswi Member

  #7
  Jun 16, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tukipata kama hawa watano wa CCM itakuwa pwaaaaaaaaaaaa kwa Peopleeeeeeeeee
   
 8. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  kweli baba hii iliyoongea ina mantiki sana
   
 9. K

  Katalyeba Member

  #9
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tanzania wabunge wa kusema ukweli, kama mmekubaliana lakini waziri anafanya yake mwumbue hadharani.

  Kwa maelezo machache niliyoyasoma hapo juu hayahitaji uwe CCM wala CHadema kukakataa bajeti hiyo, swala Muhimu ni uzalendo. Tukubaliane kwamba tunahitaji wabunge waseme hapana tuanze na moja.

  Kilimo ndo kingetutoa lakini bajeti haisemi tufanye nini ili tuweze kutoka kwenye lindi la umasikini.

  Naomba wadau wa Jamii, tuwaombe wabunge wetu waikatae bajeti, ieleze katika kilimo zimepelekwa ngapi, na zinatafanya nini, siyo washa tu, watueleze wametenga shiling ingapi kwa ajili ya kilimo cha Umwagiaji, na nishati ya uhakika, nilimsikia Filiokujombe siku moja akiuliza, watanzania hawahitaji vitambulisho, kipambele ingekuwa Umeme wa uhakika, then ndo watuambie vitambulisho. Bravo mbunge Mpina..

  Tupo pamoja na wewe hata ukifukuzwa kwenye Ugamba, Mungu atakupigania, utarudi Bungeni kwa tiketi ya Makamanda.
   
 10. W

  Welu JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 815
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  Aache uongo, tangu wote mzaliwe ni lini mmeawahi sikia budget kuu ikagomewa. Mlishaambiwa na spika kwamba hiyo kitu haiwezekani. Nawahakikishia, watarap sana, watapinga sana huku wakiunga kwa 100%. mwisho tutaambulia mayowe ya ndiyoooooooooooooooooooooooooooooo. Nani asiye juwa unafiki wa magamba.
   
 11. Msambaa mkweli

  Msambaa mkweli Senior Member

  #11
  Jun 16, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 193
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Uwazi na ukweli. Vua Gamba.
   
 12. N

  Njangula Senior Member

  #12
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Angekuwa mpinzani nisingeshangaa CCM wangesema anatafuta umaarufu. Hii inaonesha kuna patriots wengi ndani ya chama tawala wenye uchungu na nchi hii. Jamaa alilosema ni jema kabisa tena amepinga ktk pre-budget meeting na tena ktk mkutano wa budget. Binafsi naipinga imeongeza matumizi yasiyo tija.
   
 13. K

  Kazi Deo Member

  #13
  Jun 16, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hao ndio wanaohitajika sasa.Big up Mpina
   
 14. M

  Makupa JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  afadhali hoja nzito kama hii imetolewa na mbunge wa ccm
   
 15. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145

  Utawaona baada ya Mtikila kushinda kesi yake huko Arusha na kiama cha CCM kitakuwa 2015, jiulize kwa nini Wabunge wengi wa CCM wanapigia chapuo mgombea binafsi hivi sasa? tayari wameshasoma alama za nyakati ukutani hivyo hawaoni shida kuja kumtosa CCM dakika za lala salama
   
 16. M

  Malipo kwamungu JF-Expert Member

  #16
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Wasiwasi wangu baada ya bajeti itafuata itikadi makini ya Jairo kuwapongeza wabunge wote kwa sherehe zitakazo fanyika ..... na kila 1 kuondoka na bahasha ya AHSANTE aah nanii siyo rushwa hii ni kama zamani tuliita takrima kwa waheshimiwa kutusaidia kupitisha bajeti yetu sisiemu twawala bana
   
 17. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,954
  Likes Received: 1,279
  Trophy Points: 280
  mnafiki tu huyu!
   
 18. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Safi sana!
   
 19. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #19
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu uko sawa, kama kitu hukubaliani nacho ni bora uonyeshe hisia zako hadharani kuliko kuwa mnafiki.
   
 20. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #20
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nampongeza kwa kusimamia anacho kiamini bila kujali gharama zake.
   
Loading...