Mbunge awaficha waliofiwa Tarime | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge awaficha waliofiwa Tarime

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, May 21, 2011.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  May 21, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Na Anna Mrosso  21st May 2011
  [​IMG]
  Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema


  Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, amewaweka wafiwa katika kambi ya pamoja hadi mtafaruku wa kutozika watu waliokufa katika mapambano na polisi.

  Lema alisema jana kuwa yeye kwa kushirikiana na viongozi wa Chadema wilaya ya Tarime wamechukua uamuzi huo kwasababu baadhi ya viongozi wa serikali wamekuwa wakiwafuata wafiwa hao na kuwashawishi kwa fedha ili wakubali kuzika ndugu zao.

  Alisema baadhi ya wafiwa walimweleza kuwa viongozi wa serikali wamekuwa wakiwaeleza kuwa endapo watakubali kuzika watawasaidia kugharamia mazishi ikiwa ni pamoja na usafiri na chakula,pamoja na hayo waliahidiwa kupewa kiasi cha zaidi ya Sh. milioni tatu kama pole kwa kila familia iliyofiwa.

  Waziri huyo alisema baada ya kupata taarifa hizo, aliwakataza wafiwa kupokea fedha wala kukubali serikali kugharamia mazishi kwa kile alichosema kuwa wakifanya hivyo vitendo holela vya mauaji kwa watu wanaoishi jirani na mgodi wa dhahabu wa North Mara(Nyamongo) vitakuwa kawaida.

  Katika hatua nyingine, Lema alisema kuwa Jeshi la Polisi nchini linatakiwa kuwa makini la sivyo wataendelea kutumiwa vibaya na serikali hali itakayofanya Jeshi hilo kudharaulika kwa jamii japo wao wanapokea maelekezo kutoka kwa viongozi wa serikali.

  Alisema kufuatia mauaji yanayotokea mara kwa mara katika mgodi huo si kwamba wawekezaji wanafurahia bali wao pia wanasikitika kwavile wanaona ni vigumu sana kukaa katika eneo ambalo jamii inayowazunguka hawawakubali.

  "Vitendo vinavyofanywa na Jeshi la Polisi vinaweza kuhatarisha hata wawekezaji kukimbia,serikali inatakiwa kuwa makini na hilo,"alisema Lema. Naye Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema, Ester Matiko alitaka serikali ikae chini itafakari ni kwanini mauaji ya mara kwa mara yanatokea katika maeneo yaliyo na wawekezaji.

  Matiko alisema mauaji hayo hutokea kwa sababu jamii inayoishi jirani na wawekezaji wanakuwa na hali ngumu ya kimaisha ambpo serikali haijafikiria ifanye nini ili jamii inayoishi katika maeneo kama hayo zijione nazo ni sehemu ya malighafi zinazozalishwa katika eneo husika.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Watanzania maendeleo yenu yataletwa na nyie wenyewe,endeleeni kuichagua ccm kama hamjaisha kwa kuuwawa kila siku na polisi wanaotekeleza majukumu ya maboss wao.Hakikisheni mnakiunga mikono Chadema sbb kimeonyesha nia ya dhati kwa kupambana na mafisadi hao hao walioingia mikataba mibovu na Wawekezaji(kisa kitu kidogo)
   
 3. c

  chelenje JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Source nipashe ukurasa wa ngapi?????:biggrin1:
   
 4. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,135
  Likes Received: 2,159
  Trophy Points: 280
  Naomba nijulishwe Majina ya Askari waliohusika kuua...
   
 5. Binti Magufuli

  Binti Magufuli JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 7,455
  Likes Received: 756
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Mwananchi la May 20 2011 limeandika kuhusu kufichwa kwa wananchi lakini halikumhusisha Mbunge Lema moja kwa moja na tuhuma hizi. Yafuatayo ni maelezo kutoka gazeti la mwananchi.

  Friday, 20 May 2011 21:20
  Anthony Mayunga-Tarime
  "WANANCHI wa Nyamongo wilayani Tarime, wamewaficha na kuwapa ulinzi mkali, ndugu wa marehemu waliouawa na polisi katika jaribio la kuvamia Mgodi wa Barrick, ili kuepuka kile kinachodaiwa kuwa ni uwezekano wa serikali kuwarubuni ili wakubali kuzika.

  Mei 16 mwaka huu polisi wilayani Tarime, waliwaua kwa kuwapiga risasi, watu watano kati ya zaidi ya watu 1,000 waliovamia mgodi huo kwa lengo la kupora mchanga wa dhahabu.


  Hivyo tukio hilo lililotokea katika Kijiji cha Matongo, wilayani humo limesababisha msuguano mkali kati ya polisi na wananchi wa eneo hilo ambao juzi, waligoma kuzika miili ya marehemu hao na kukataa rambirambi ya polisi.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana, zilisema uamuzi wa kufichwa ndugu wa marehemu, unalenga katika kuhakikisha kuwa hawarubuniwi na vyombo vya serikali, inayotaka miili hiyo izikwe.

  Jeshi la Polisi limeonyesha nia ya kutaka kuzika miili hiyo kwa gharama zake na kutoa rambirambi kwa wafiwa, hatua ambayo wananchi wameipinga.


  "Tumelazimika kuwaweka ndugu wa marehemu katika kambi maalumu na kuwapa ulinzi mkali. Tunawagharimia kila kitu ili kuvunja nguvu za ushawishi zinafanywa na vyombo vya dola kwa kuwatumia wafanya biashara maarufu wa hapa,"alisema mmoja wa wananchi hao.

  "Tumefia hatua hiyo baada ya kuona serikali inataka kulifanya tukio hilo dili. Tumeanza kuona ikiwaita ndugu hao kwenye vikao vya siri juzi usiku na kuwashawishi wakubali kuzika na kupewa rambirambi ya Sh3 milioni kwa kila mfiwa," alisisitiza mwananchi huyo.

  "Suala kubwa ni kwamba fedha hizo zimetoka wapi, sSerikalini ama mgodini," alihoji.Alisema kitendo hicho kinaashiria kuwa watu wengi wanaouawa na polisi na kuwahi kutangazwa kuwa walikuwa kwenye mapambano, wanauawa kimakosa.

  Kauli ya mwanakijiji huyo iliungwa mkono na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, ambaye alisisitiza kuwa ndugu wa wafiwa wamefichwa.

  Lema pia ni Waziri kivuli wa Mambo ya ndani aliliambia gazeti hili jana kuwa watu hao wamefichwa ili kudhibiti rushwa inayolenga katika kuwashawisihi wakubali mazishi."Haiingii akilini kuona serikali hii inaua kisha inahaha kutoa rushwa kwa wafiwa, wanaficha nini kama walitekeleza wajibu wao wa kuua
  waharifu, majambazi wavamizi, hizi fedha nani katoa, je kwa kufanya hivyo inamwekea mazingira gani mwekezaji maana hilo si suluhu la
  matatizo,"alisema.

  Kamishina Chagonja aendelea kubanwa

  Katika hatua nyingine, Mkuu wa Idara ya Operesheni katika Jeshi la Polisi, Paulo Chagonja jana alibanwa na ndugu wa majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Bugando wakitaka msaada.


  "Mkuu sisi ndugu zetu wako Bugando wana hali mbaya sana, gharama ni kubwa hakuna msaada wowote uliotolewa, tuligharamia wenyewe kuwapeleka mbona hamuwazungumzii wanapataje hizo fedha lakini mnasema
  mna ubani wa waliokufa, mpaka wafe ndipo uje utoe,"alihoji mmoja wao.

  Hata hivyo Chagonja hakujibu hoja hiyo na badala yake alisema "hapa kuna majeruhi wangapi,ooh wako Bugando wako wangapi,ok sawa."

  Mbunge watia neno
  Mbunge wa Viti Maalumu Chadema na ambaye PIA ni Waziri kivuli wa Mambo ya Uwekezaji, Esther Matiko, alisema, mpango wa serikali wa kuunda tume hauna manufaa kwa jamii na kuwataka watoe ripoti ya watu sita wanaodaiwa kuuawa mwaka jana katika Hifadhi ya Serengeti".

  Sasa sijui tushike lipi tuache lipi kati ya nipashe na mwananchi.
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Wanasiasa siku zote hutafuta umaarufu kwenye balaa. Hao cdm wanatafuta kupinda ukweli, hivi unavamiwa na kundi la watu, nawe una silaha, uwache wakuue? Loh! Haiyumkiniki kabisa. Unavamiwa na kundi la watu unafyatua risasi, kama arusha, wanataka kufanya hii dili ya umaarufu. "Mshindwe na mlegee".

  Hao wawekezaji kabla ya kuwekeza huwa kitu cha kwanza wanaulizia usalama wao na mali zao utakuwaje wakiiwekeza? Ukishindwa kuwalinda hawawekezi. Na Serikali imekubali kuwalinda na imefanya vyema. Wanasias uchwara wasitake mtaji wa bure kwa hili.
   
 7. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,823
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  wewe akili zako ni robo kibaba hivi angeuwawa mdogo wako ungesema haya unayoyasema?!! unawaza kwa kutumia makalio hilo ni tatizo sana...hujui hata katiba inasema nn?!! hujui wajibu wa serikali yeyote duniani acha hii yenu ya Magamba ni kulinda wananchi wake sio wawekezaji!!! shame..eti serikali ilinde wawekezaji una akili za wapi wewe?!! kanye huko CCM magamba halafu uje hapa useme huu utoko wako!!!

  Unadhani sisi tunafurahia watu wetu kuuwawa kila mara halafu mnasema wakurya wakorofi..ovyooo
   
 8. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Polisi wamefundishwa njia nyingi za kujihami na waandamanaji, hata kama wa mapanga, siyo kuua!! vingievyo mauaji yangekuwa mengi ulaya maana ndo kwenye maandamano ya mara kwa mara. Hatuelezwi km mapanga unayoyasema waliyokuwa nayo wananchi yalimkata askari yeyote!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Siku zote polisi waogope kuua raia wao walioapa kulinda usalama wao na mali zao.
   
 9. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Wacha mdogo wangu, hata babangu. Kama anavamia sehemu ya watu kwa kuiba na auawe na mazikoni siendi. Mwizi, Jambazi.

  Unataka sema nini wewe, watu wakusanyike, waende kwa nia ya kupora na kudhuru wengine halafu wakae wanatizamwa macho tu? Nashanga! Piga ua, yeyote anae trespass, au hujui sheria za trespassing? Tena kundi zima, mnavamia sehemu waliopewa wawekezaji wafanye shughuli zao? Halafu muwachiwe, eti kwa nini? Kwa kuwa ni mdogo wake FF? Hata aingie mmoja tu uwani kwangu bila kuruhusiwa, wallahi nnamtia risasi halafu tutajuana mbele labda nisimuone! Haa, mtu aingie kwangu bila taarifa akinibaka? Na mie silaha nnayo nimuachie? Hapo hujanambia kitu babuwee.
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nilitaka kukushambulia ila nilipoangalia picha yako na huyo NINJA mweupe nyuma yako, nikakata tamaa na kuona si kosa lako.
   
 11. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ila mheshimiwa Lema mjanja sana jaman teh! Safi sana Kamanda!
   
 12. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Sijasikiapo waandamanaji wa ulaya wakienda polisi kutaka watoa wahalifu kwa maandamano, ikitokea hivyo hata ulaya hawataachiwa. We waandamana kuelekea polisi, na mule kuna watuhumiwa wa chama chako, na wengine na silaha za serikali, halafu uachiwe tu au upigwe na chelewa au henkachifu? Basi hao polisi watakuwa mabaradhuli, Unanshangaza!
   
 13. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Waona stara za ninja? Heheee! Umenikosha wallaahi! Wengi hawalijui hilo.
   
 14. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,823
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Huna uninja wowote wewe ni Gamba na njaa ndio zinakupa shida..njoo Tarime hapa tukunyoroshe na uninja wako wa kigamba hutapiga mtu risasi hata mmoja...
   
 15. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo mtu akija na kuipa Serikali pesa, na hapo unapoishi unatimuliwa na kuambiwa utapewa pesa. Mashamba yako wanachukua kwa nguvu na bila kukulipa. Wewe ukianza kudai unaambiwa umekuwa jambazi, UTAFURAHI SIYO?

  Mbona una mawazo kama Makaburu ya South Africa miaka ilee..... Yanavamia nchi za watu na kujimilikisha na Mandela akidai haki, wanamtupa JELA na mijitu kama (Ninja weupe wa Kike) wewee inakuja hapa na kusema "Majambazi ya ANC yalivamia mgodi, inabidi kupiga risasi....."

  Barrick Gold kwao Canada na huku wamekuja kuiba na kufanya uharibifu........ Hebu angalia hizi picha na useme hawa MAJAMBAZI na WAVAMIZI unaowaita, wamemkosea nani hadi kuumizwa na ma Chemical ya hawa WASHENZI unaowatetea?

  Kama wewe wafanya kazi huko au Mumueo, basi muanze kutafuta kazi mpya maana tutawachomelea mkiwa ndani ya hiyo migodi na kuwafukia kama mlivyowahi kuwafukia Watanzania wakiwa hai.....

  [​IMG][​IMG]
  Ninja niliyesema ni wale wanaobeba Mabomu na Kujilipua. U-Ninja wa Kijapan, hamuuwezi.
   
 16. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Huna lolote, mvamie kwa watu halafu mwataka migwe kwa henkachifu? Unanini babuwee?
   
 17. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #17
  May 21, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  faizal hao wanakijiji miaka nenda rudi iliyopita walikua na ardhi yao yenye dhahabu!waliishi raha mstarehe!jee ujio wa mwekezaji umewanufaisha kwa lolote?maisha yao yamekua bora zaidi?jee unaruhusa ya kuua mtu kisa dhahabu tena si yako!mbona wakulima huwa hawalindwi namna hiyo mashamba yao yanapovamiwa na tembo,nyani au wafugaji?
   
 18. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #18
  May 21, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Huna lolote, mvamie kwa watu halafu mwataka mpigwe kwa henkachifu? Unanini babuwee? Huku kwetu hata ukiianua kufuli uani tukikumata twakutia tairi la shingo, njoo na wewe ujaribu. Nashanga!
   
 19. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #19
  May 21, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,635
  Likes Received: 1,409
  Trophy Points: 280
  sasa hicho kimbele mbele cha serikali kutaka kuzika na kutoa milioni tatu kinatoka wapi? wawaachie wenye wafu wazike wafu wao

  wao kinawahusu nini? kama wanajua ni tresspasers wameuwawa wawachie ndugu wazike ndugu zao.. wanajishaua nini na kutaka kutoa msaada wa usafiri, rambi rambi na usafiri kwa wezi?
   
 20. M

  Makupa JF-Expert Member

  #20
  May 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hana lolote zaidi ya uwendawazimu alionao unaosababishwa na hicho kitu anachovuta na tunaamini ya kwamba hatamaliza muda wa kipindi chake cha ubunge kabla ya kuwa chizi moja kwa moja mwambieni ache kuvuta ukubwani haipendezi
   
Loading...