Mbunge atakayeingia Kamati ya kuichunguza TISS atakuwa amejiteka mwenyewe

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,587
Itakuwa ni kichekesho cha mwaka kwa idara ya MASHUSHU Kuchungzwa na wasio na weledi wa kishushu. Yaani wewe unatumwa na Zitto uende ukawachunguze wana usalama wa taifa na wewe unaenda hahahahaha.

Kwa kifupi bunge hiyo kamati zito anayotaka iundwe kwenda kuwachunguza mashushu itajikuta inajichunguza yenyewe badala ya kuchunguza wanausalama hao.

Kwanza mkumbuke kuwa hawa mashushu sifa kuu ya kuajiriwa ni Lazima uwe na uwezo mkubwa wa kiakili Darasani. Kwa maana hiyo hawa ni mkusanyiko wa wale waliokuwa wanatuongoza darasani ndio maana upatikanaji wao mara nyingi hufanyika kwa kuwatafuta mashuleni tena kwenyenzile Shule bora na za Vipaji.

Hawa ndio mnaotaka kwenda kuwachunguza??? Sifa ya kuwa mbunge ni wewe ujue tu kusoma na kuandika unataka kwenda kumchunguza Shushushu. Kama wamewateka kuliko muende kuwachunguza bora muwaombe msamaha tu wasiwateke tena.

Itakuwa ni ajabu kama Mashushu wetu watakubali kufuatiliwa kirahisi na itaonyesha udhaifu mkubwa sana. Hapa ndipo mnapotakiwa muuonyeshe umma kuwa kweli nyie mlikuwa bora darasani......

Na kama mtachunguzwa na kamati zetu za bunge zenye sample ya wabunge aina ya kina Mbowe walioshindwa kutafsiri maswali ya form six hadi akalamba ziro na kweli mkakamatika na kosa basi nchi haitakuwa Salama. Kama hawa wakifnikiwa vipi wenye sifa kama za kwennu toka mataifa mengine si watakuwa wanatujua hadi tunavyolala?

Dhihirisheni ubora wenu
 
Kina zitto huwa wanajiongelea tu lolote linalokuja kichwani..unajua siku hizi hawana loophole wa kupata udhaifu wa serikali ili wateñgeneze hoja za msingi..ndio maana utasikia mara vyeti, mara njia za kuwataja watu wa unga sio nzuri, mara tunatekwa..huyu si alijificha bungeni kuwa akitoka Nje atakamatwa hivi watekaji wanakusubiria Nje kweli huku unajua unasubiriwa?? Hapo ndipo upinzani ulipofikia.
 
" eti wale wenye akili darasani" acha uongo wewe.
Moja ya kigezo huko kwa sasa ni undugu na kujuana..

Binafsi nilikuwa kipanga darasani na ninawajua vipanga wengi sana wa miaka mitatu mbele yangu lakini wengi wao wako kwenye makampuni binafsi na nje ya nchi wakijenga mataifa ya wenzetu...

Sidhani kama hawa mashushu wa Tanzania wangekuwa na akili wangekuwa wanafanya matukio kama haya wafanyayo sasa au tungekuwa na majanga kama escrow, richmond, rushwa kila mahali, radar mbovu,,,nk..
 
zitto alitaka Rais atangaze baa la njaa...Rais akamuona mjinga
Kijijini kwetu watu walishangaa kusikia njaa wakati mkulima aliyepata mavuno kidogo alikuwa na gunia hamsini za mahindi ndani ya nyumba. Kina zitto walizoea kumtisha Mizengo Pinda sasa wamekwama, kwa vile vichwa, JPM na Kassimu Majariwa
 
Bunge Hawana Uwezo Wala Nyenzo za Kuichunguza TISS na hawataweza kulazimisha kuwahoji Watendaji wa TISS maana wana kinga katika sheria yao. Watu wanafanya mambo kwa mihemko na chuki - hawazisomi sheria vizuri. Anachotaka Kifanyike Zitto HAKITAFANYIKA HAPA TANZANIA: MUDA UTAMFUNDISHA
 
Hivi punde nazan hao mashushushu unaowasemea sio wa nchi hii au hujawai waona wa kwetu. Asilimia flani yao ujue either mmoja wa ndugu wake yupo kule ivyo aliingia kwa kuwa hakuna kazi kitaani. Anyway jua ni wa kawaida tu
 
Idara imeoza na JK ndo alianza kuonyasha udhaifu hadharan kwenye swala la ulimboka kibanda na Dr Mvungi!!! Sasa ni dhahiri inabidi kufumuliwa
 
Hivi punde nazan hao mashushushu unaowasemea sio wa nchi hii au hujawai waona wa kwetu. Asilimia flani yao ujue either mmoja wa ndugu wake yupo kule ivyo aliingia kwa kuwa hakuna kazi kitaani. Anyway jua ni wa kawaida tu
jamaa ameklemishwa sijui wapi bora umemkumbusha
 
Wewe ni lumaga kama jina lako hasa. Zitto amekosea nini. Je watu hawakuw na njaa mwaka jana. Ni kosa gani kuwa na njaa nchini. Mvua ikikosekana siyo kosa la ntu. Mkuu alihitaji tu kutambua hilo na kuwasaidia wenye shida. Mbona unaongelea mavuno ya sasa. Acha unafiki
 
nitajie best student alieingia national top ten o level au alevel au kiongoza chuo kikuu mmoja tu ambaye yupo tiss..

best student wengi wapo vyuoni ma lecture.. na wengine wengi wapo kpmg, pwc, delloitte, ernst and young na makampuni mengine makubwa ya kimataifa ambapo hakuna kujuana..

tiss watu wanawekana ndugu tu
 
Back
Top Bottom