Mbunge Abdulwakil: Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi italinda utu, heshima na faragha yetu

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Akichangia hoja kupitia mjadala wa Muswada wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Mbunge Ahmed Abdulwakil amesema kuwa Sheria hiyo ni muhimu na endapo itapitishwa na Bunge italinda utu, heshima na faragha ya wananchi.

Kutokana na Tanzania kutokuwa na sheria hii watu wengi wamekuwa wahanga wa taarifa zao binafsi kutumiwa kiholela, mfano kwa baadhi ya Wabunge ambao taarifa za mazungumzo yao binafsi zilitolewa hadharani bila ridhaa yao.

Muswada huo ukipitishwa na kuwa sheria utakomesha matumizi mabaya ya taarifa binfasi na watu watakuwa na amani linapokuja swala la taarifa zao na faragha zao kuwa salama.
 
Back
Top Bottom