Mbowe usiwachukue walioachwa na CCM

Mbowe usiwachukue walioachwa na CCM

Nashauri cdm isiwachukue wale wote waliotemwa na ccm dodoma. Lengo ni kuepusha minyukano ya chuki Na uhasama wa kivyama. Kwakua sikuzote wajue anaewatoa Kule ndiye mwenye nchi.
Na mienendo yake sio migeni kwa upinzani.

Pia Tumeona jinsi wabunge wa chamadola walivyotoa ushirikiano Katina Sakata la bashite.

Nadhani ni vyema kuwaheshimu kwa hatua walizochukua Katika Chami Chao ili huko bungeni waendelee kunyukana ili washindwe kujua Nani hasa anawatafuna.
Mkiwachukua mnawapa sababu ya wao kuwaona kue nyie ndio masnitchi wao. Mwishowe Wataungana na kuunga mkono hoja hata za kipuuzi ili kuwakomoa.

Nawasilisha
We! unataka samaki apishe chambo?
Fisi yake mizoga yakhe....umeshachoka kuwa 'kamanda' nini?
 
Mhe. Mbowe amani iwe kwako. Fukuzafukuza inayoendelea huko Dodoma itaathiri pa kubwa sana mwenendo wa chama hicho. Tutegemee kupata makapi mengi sana kutaka kujiunga na Chadema. Nikuombe usiwapokee wanachama hao maana yatavuruga sana chama chetu. MTU pekee ambaye anatakiwa kupewa kadi endapo atafukuzwa na CCM ni Bashe. Hussein Bashe ni mtu anayejitambua nadhani kwangu Mimi kati ya wachama wa ccm wote huyu ndiyo mwenye akili timamu. Mpokee kwa mikono miwili. Usijaribu kupokea wengine waliotemwa na kamati ya CCM.
Maoni yangu.
Sasa unaona hawafai wakati kipindi cha uchaguzi usiku walikuwa wanauzia ramani za kivita na nyeti yote? Au wakati wa uchaguzi 2015 ulikuwa hujapevuka?
 
  • Thanks
Reactions: Qj_
Sasa unaona hawafai wakati kipindi cha uchaguzi usiku walikuwa wanauzia ramani za kivita na nyeti yote? Au wakati wa uchaguzi 2015 ulikuwa hujapevuka?
Mkuu unaniweka kwenye kundi la watoto wa miaka ya 80's?
 
Kila mtu ana faida na hasara hapa duniani,hata angekuwa mtendaji wa kijiji ni wa kupokea maana anawafuasi kinachoangaliwa ni wafuasi wa mtu hata wakiwa wawili.
CDM pokea yoyote atakayekuja kujiunga na chama,Haba na haba hujaza kibaba!
CDM ni chama cha wote!
Wafuasi? Hamjajifunza kutokana na swali la Dr Slaa? EL alisema atakuja na wabunge 50 na madiwani na wakuu wa mikoa etc...mwisho wa siku wangapi walimfuata? Hivi huwa hamfikirii pale ambapo mnaleta mizoga miwili huku mnapoteza watu wenye akili timamu 50? And you call yourself an econometrician?
 
Tatizo la watu wengi mnafikili siasa kama simba na yanga na hili ndio linalotuumiza mpaka Leo nchi inashindwa kwenda mbele
 
Mtaji wa chama ni watu. Isitoshe, huko walikofukuzwa nako kumejaa wachafu tu. Namshauri Mbowe awapokee tu
Elezea pia impact yake kwenye chama pale ambapo wenye akili timamu wanapoamua kuondoka sababu mmeamua kuzoa makapi
 
Hoja dhaifu sana ,kila mtu wakati wa kutafuta mgombea anakuwa na mtu wake lakini baada ya hapo Maisha yanasonga .
 
Siasa ni watu .... nadhani ni busara kutumia silaha yoyote kumshinda adui ... CHADEMA wasifanye makosa , kama ambavyo wamemchukua WEMA SEPETU wafanye hivyo hivyo kuwachukua wote wanaotemwa CCM.... Sophia Simba anakundi kubwa la akina mama ....
Hivi unajua aina ya kina mama wanaomzunguka SS? Unajua waume zao ni kina nani, wako wapi na wanafanya nini? Unadhani watasaliti waume zao na familia zao wamfuate SS?
 
Wewe acha uzezeta,siasa ni timing,hao wote ni wetu chadema na watadumu chadema kwa sababu kuu mbili.
1.wamefukuzwa ccm moja kwa moja
2.wana hasira na mwenyekiti wa ccm dikteta magufuli.
Mbowe chukua wote tukianza na bashe ili jimbo lake liingie upinzani.
Afadhari umenisaidia kujibu. Mambo ya MANGE sio kuchukua kila neno analoongea,huko ni kushikiwa akiri.Eti uchaguzi uluopita tulishndwa kisa ya kumchukua lowasa,ni MTU mjinga tu anaweza kusema hivyo.Yaan ww hukuona jinsi mshikemshike ulivyo kuwa???
Makotena ya kura feki hamkuyaona yakiitwa mahindi???Hisani ya Lubuva hamkuiona kama ya refa aliyechezesha mechi ya PSG na Barcelona???Yaliyotokea Zanzibar mmesahau???
Je na ushindi WA kura million 8 kwa milioni 6mmesahau pamoja na hisani ya lubuva na kailima???
Watanzania mkoje ninyi??? Kwann msiwe na critical thinking, eti wasipokelewe????
Haya yatakuwa maajabu ya Dunia.
 
Nadhani yule mama Jesca wa Iringa atakuwa mtaji mkubwa katika kuizika ccm Iringa moja kwa moja,na tunaweza sema hivyo hivyo kwa Asa Simba aliyekuwa mwenyekiti Ilala huyu pia mtaji
 
  • Thanks
Reactions: Qj_
Hao walioachwa waanzishe chama chao wakiite CCM Asili.. Waachane na ccm dikteta
 
Hayo ni mawazo ya woga tu. Hakuna mnyukano wowote wa kisiasa. Na huo utakuwa uvunjaji wa katiba ya nchi. Kila mtu ana uhuru wa kujumika. Karibuni mlotemwa ccm, hakuna mahali pengine pa kufanya siasa za maana kama CDM. Njooni tuungane tuijenge nchi.

Nashauri cdm isiwachukue wale wote waliotemwa na ccm dodoma. Lengo ni kuepusha minyukano ya chuki Na uhasama wa kivyama. Kwakua sikuzote wajue anaewatoa Kule ndiye mwenye nchi.
Na mienendo yake sio migeni kwa upinzani.

Pia Tumeona jinsi wabunge wa chamadola walivyotoa ushirikiano Katina Sakata la bashite.

Nadhani ni vyema kuwaheshimu kwa hatua walizochukua Katika Chami Chao ili huko bungeni waendelee kunyukana ili washindwe kujua Nani hasa anawatafuna.
Mkiwachukua mnawapa sababu ya wao kuwaona kue nyie ndio masnitchi wao. Mwishowe Wataungana na kuunga mkono hoja hata za kipuuzi ili kuwakomoa.

Nawasilisha
 
Akili mfu ndo hizi yaani mtu akifukuzwa na rais basi asipokelewe kwenye chama kwa kuogopa uhasama!!?? Tuunganishe watanzania wote tuijenge Tanzania mpya tuache kugawa watanzania vinginevyo tuachane na vyama vingi basiii.
 
Chama hakiwezi kukataa wanachama wapya
CHADEMA kama cha siasa kiwapokee watakaotaka kujiunga,kiwachunguze kwanza wale wapya ambao watatakiwa kupewa nafasi za uongozi ndani ya chama
 
Nashauri cdm isiwachukue wale wote waliotemwa na ccm dodoma. Lengo ni kuepusha minyukano ya chuki Na uhasama wa kivyama. Kwakua sikuzote wajue anaewatoa Kule ndiye mwenye nchi.
Na mienendo yake sio migeni kwa upinzani.

Pia Tumeona jinsi wabunge wa chamadola walivyotoa ushirikiano Katina Sakata la bashite.

Nadhani ni vyema kuwaheshimu kwa hatua walizochukua Katika Chami Chao ili huko bungeni waendelee kunyukana ili washindwe kujua Nani hasa anawatafuna.
Mkiwachukua mnawapa sababu ya wao kuwaona kue nyie ndio masnitchi wao. Mwishowe Wataungana na kuunga mkono hoja hata za kipuuzi ili kuwakomoa.

Nawasilisha
Hawa ndio wale Edo alisema watamfuata wachukueni tu tena wote pamoja na yule aliyeshinda kesi ya ARV feki, na mahakama kuamuru walipwe bilioni 60
 
Back
Top Bottom