Mbowe: UKAWA Tutaondoa Mashangingi Serikalini!

Mbowe: UKAWA Tutaondoa Mashangingi Serikalini!

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,146
Reaction score
3,829
WanaJF,

Kwa kipindi chote ambacho nimekuwa nikimfahamu Mbowe sikuwahi kumchukulia kama ni mtu makini na anayepaswa kusikilizwa. Uwa nampuuza mara kwa mara kutokana na maamuzi yake ya ajabu ajabu.

Hivi wanaJF, wote hapa tunafahamu kuwa Mbowe alipoingia kwenye Bunge kwa mara ya kwanza aliahidi kuwa CHADEMA watasusia posho; watasusia magari ya kifahari na watasusia semina zenye lengo la kufanya anasa kwa kutumia pesa ya mlipa kodi. Je, walipoingia bungeni mmeona hayo yakitendeka?

Leo hii tena, mtu yule yule, kwenye chama kile kile, analaghai wakulima huko vijijini kuwa kama UKAWA itaingia madarakani basi mashangingi, posho za vikao na safari za rais, vyote hivi vitapigwa marufuku na pesa itakayookolewa yote itaelekezwa kuboresha kilimo nchini. Je, unamuamini mtu huyu?
 
Huwa simuelewi kabisa Mbowe.Hivi si alikuwa anatumia Shangingi la serikali kama kiongozi wa kambi ya upinzani,mbona hakulikataa ili kuonyesha mfano.Wapinzani wa Tanzania bado sana,itachukua muda kuingia Ikulu.
 
Bora tukaongozwa na mtu asiyeenda shule kuliko kuongozwa na mtu asiyeamini kama watanzania ni maskini sana! Miaka 53 ya uhuru tunakura mlo mmoja, miaka 53 ya uhuru wakati wa uchaguzi hospitali hazina dawa, miaka 53 ya uhuru ofc za umma hazina fedha za uendeshaji, miaka 53 ya uhuru akina balali wamefichwa, miaka 53 ya uhuru akina Babu Seya wamefichwa kwa husuda, miaka 53 ya uhuru tunajenga barabara zisizo na viwango! n.k
 
Mbowe alirudisha lile shangingi ili lipigwe mnada ila baadae akalifuata kimyakimya tena.
 
Mbowe alirudisha lile shangingi ili lipigwe mnada ila baadae akalifuata kimyakimya tena.

Halafu lilionekana likifanyakazi za kampeni za CHADEMA mahali, lol Mbowe haaminiki. Naweza kukubali kuwa jamaa kauza nafasi ya urais kwa Lowasa kwa blioni 10 na kumtupilia mbali Dr. Slaa.
 
Haa ha ha kweli Mbowe anatufanya watu wote poyoyo...hiyo hoja aliishaishindwa, sawa na ile ya posho.Zitto pekee ndiye ana moral authority ya kuzungumzia hayo.

Ni vyema sasa Mbowe aungane sasa na Lowassa kusema UFISADI SIO TATIZO.Kweli dunia haigandi, sikuwahi kudhan kama mgombea urais wa Chadema anaweza kusema ufisadi sio issue.

Kweli chadema sasa rasmi ni maficho ya mafisadi.
 
mbona inawezekana hakuna haja ya kuwa na gari la mil 200 kwenye wilaya wakat watoto wanakaa chini darasani au wakulima wanakopwa mazao,good focus
 
Huyu jamaa juha kweli, mbona hatemdelei zile ford za m4c? Slaa mwenyewe anashangingi ya chadema!
 
kwani mbowe anagombea uraisi?
Mbowe ni mwenyekiti wa chama kinachotaka kutoa raisi. Angali tamko lake hapa chini wakati analirudisha kabla hajaenda kulichukua kimya kimya. Siasa za kilaghai hazisaidii upinzani.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU BAJETI YA SERIKALI YA MWAKA 2011/2012


Utangulizi
Mnamo tarehe 21/06/2011 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha bajeti ya Makadirio na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2011/2012.

Pamoja na Bajeti ya Serikali kukubali na kuzingatia baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge wa Kambi ya Upinzani na hususani CHADEMA kama vile ;
a) Kupunguza kodi na tozo mbalimbali kwenye mafuta ya petrol na dizeli.

b) Kupunguza kiwango cha faini za makosa ya barabarani kutoka shilingi 300,000/50,000 hadi kufikia ukomo wa shilingi 30,000.

c) Kufuta leseni za biashara kwenye Majiji,Halimashauri za Wilaya na Vijiji.

d) Kufuta misamaha ya kodi kwenye makampuni yanayotafuta mafuta na gesi Nchini.
e) Kuongeza pesa kwenye bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu kwa kuhakikisha kuwa kodi ya skills development levy 2/3 inapelekwa kwenye bodi kwa ajili ya Mikopo.

Katika kupitisha bajeti hiyo wabunge wa Kambi ya Upinzani na hususani wa CHADEMA tuliamua kupiga kura za HAPANA kwenye mapendekezo hayo ya Serikali kutokana na sababu mbalimbali na haswa hizi zifuatazo;
1. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuondoa posho za vikao (sitting allowances) kwenye mfumo wa malipo ndani ya serikali.

2. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuhakikisha kuwa magari yote aina ya “Mashangingi” yanayotumiwa na viongozi na watumishi wa umma yauzwe kwa mnada ndani ya miezi sita na viongozi hao wakopeshwe magari kwa ajili ya kufanya majukumu yao mbalimbali.

3. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kufuta/kupunguza misamaha mikubwa ya kodi ambayo Makampuni ya Madini yanapata ili kuhakikisha kuwa serikali inapata mapato kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

4. Serikali imekataa kuingiza pensheni kwa ajili ya wazee wote nchini ya shilingi 20,000 kila mwezi ili kuweza kuwapunguzia ukali wa maisha wazee wetu .

5. Serikali imekataa Kufuta/kuondoa misamaha ya kodi kwa kipindi cha miaka 10 kwenye maeneo maalum ya uwekezaji (EPZ).

6. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuhakikisha kuwa tunapunguza gharama za safari na haswa kuhakikisha kuwa ni viongozi wakuu na wenzi wao tuu ndio waruhusiwe kusafiri kwa kutumia daraja la kwanza (first class) ambao ni ;

Rais
Makamu wa Rais
Waziri Mkuu
Spika
Jaji Mkuu

Mawaziri wasafiri kwa kutumia daraja la pili (bussines class) na viongozi wengine wote wa umma na watumishi wa umma wakiwemo wabunge wasafiri kwa kutumia daraja la kawaida (economy class).

Pia misafara ya viongozi wakuu ipunguzwe ili kupunguza gharama za kuhudumia misafara hiyo pindi wanaposafiri nje ya Nchi.

Hitimisho.
Tumeamua kumwandikia katibu wa Bunge barua ili aweze kutenganisha fomu kwa ajili ya mahudhurio na kwa ajili ya posho na wabunge wa CHADEMA hawatasaini fomu za posho.
Kuhusu magari, kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) Mhe. Freeman Mbowe ameamua kurejesha gari yake aina ya “Shangingi” alilopewa na Bunge ili liwe la kwanza kupigwa mnada.

Tunawataka wabunge wengine waunge mkono hoja hizi kwa masilahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Imetolewa na ;
………………………
Mhe. Freeman A. Mbowe (Mb),
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
21 Juni 2011
 
Mbowe yuko kibiashara zaidi. Ukimfuata kichwakichwa utajuta kama Dr. Slaa...
 
Hivi CCM haioni aibu tu,mbona topic ya picha za ku edit sijui photo shopisha nini imewaumbuaaa mwajeukia vengineee,aibu yakheee
 
lissu alishasema wakisusa posho magamba yatachukua na kuwaumiza kwenye kampeni. kutochukua ilikuwa hasara kwa ukawa. sema mbowe atuambie gari mbadala. unatoa shangingi na kuleta nini? tutaokoa sh ngapi kwa kufanya hivyo?
 
Mbowe ni mtu makini na ana akili sana. Maashangingi ni sera ya CCM kuwanunulia mawaziri na viongozi wakuu. Kwa taarifa yako gari la KUB ni lazima sio hiari. Halikopeshwi. Sera ya CDM sio mashangingi.UPO hapo?
 
Mbowe ni mtu makini na ana akili sana. Maashangingi ni sera ya CCM kuwanunulia mawaziri na viongozi wakuu. Kwa taarifa yako gari la KUB ni lazima sio hiari. Halikopeshwi. Sera ya CDM sio mashangingi.UPO hapo?

Ndio unavyodanganywa?kweli wewe zezeta.Serikali hailazimishi mtu kuchukua gari wala posho.


Ndio maana Zitto alikataa makalio na Mbowe alirudisha gari la Kiongozi wa Upinzani mbele ya waandishi wa habari, lakin kimyakimya akaenda kulichukua tena.
 
Back
Top Bottom