Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
Leo katika kuperuzi kwangu mtandaoni nikakutana posti inayosema Dkt Slaa na Lipumba wamenunuliwa na CCM kwa lengo la kuisaliti CHADEMA/CUF na UKAWA katika uchaguzi wa mwaka wa jana. Katika posti hiyo pia Zitto ametajwa miongoni mwa waliohongwa ili kufanya UKAWA isishinde.
Kwa kuchelea kuwa na maelezo mengi, leo naomba kumzungumzia Dkt Slaa tu, Lipumba na Zitto katika hili nitawazungumza siku nyingine inshallah.
Mosi
Wilbroad Slaa hakuisaliti chadema, bali kajitoa baada ya chama kupoteza mwelekeo. Baada ya chama kuacha mambo iliyo aamini na kufuata mambo iso yaamini.
Ujio wa Lowassa CHADEMA uliingia doa baada Dkt Slaa kujiuzulu ukatibu mkuu kwa kile alichodai utaribu uliotumika kumpokea Lowassa haukuwa mzuri na ungekipa wakati mgumu chama mbele ya wanachama na watanzania.
Pamoja na mambo mengine, Dkt Slaa alitaka kabla ya chama kumpokea Lowassa, ni lazima kwanza Lowassa atoke hadharani na ushahidi unao msafisha na tuhuma za ufisadi. Ushahidi utakao fanya nyaraka ambazo mwanahalisi ulizitumia kuandika habari za ufisadi ulio muhusu Lowassa kuwa si za halali na ya kwamba zilipikwa tu kwa lengo la kumchafua Lowassa.
Lowassa hakuita vyombo vya habari kuongelea usafi wake kwa kutumia nyaraka sahihi. Dkt Slaa aliamini, kwa nafasi ya uwaziri mkuu hasingekosa vimemo au nyaraka zozote zenye kuonesha muhusika mkuu wa Richmond tafauti na yeye(kama yupo tafauti na yeye).
Kutokana na hali ya kisiasa alokuwa nayo lowassa baada ya kukatwa CCM, hakuwa na cha kupoteza endapo MADUDU YA CCM na ya rais mstaafu yengewekwa hadharani kwa nyaraka sahihi. Kwa nafasi alofikia ya uwaziri mkuu, kama angekuwa msafi na suala la Richmond alisingiziwa, basi kwa vyovyote vile Dkt Slaa alitaraji nchi kutikisika na CCM kuanguka asubuhi na mapema kwa kuwekwa hadharani kila aina ya uchafu wa CCM na SERIKALI, na ndio maana alisisitiza, kabla ya kumpokea huyu mtu aandaliwe press.
Matokeo yake Chama kiliamua kumkaribisha na kumpokea mtu walio msema kuwa fisadi kwa miaka mingi, bila kuzingatia ushauri mzuri na wa maana wa Dkt Slaa. Wajumbe wa CC wa CHADEMA wakabeza hoja na mawazo ya Dkt Slaa wakamkaribisha Lowassa.
DKT SLAA ALITAKIWA KUFANYA NINI?
Dkt kama katibu mkuu, alitakiwa aendelee na majukumu ya utekelezaji maazimio ya CC ya kumkaribisha Lowassa hata kama utaratibu uliotumika kumpokea hakukubali.
AU
Ajiuzulu kwa kuona chama anacho kitumikia kimeacha misingi yake na sababu ya kuundwa kwake, au kwa kuchelea kutoleta ufanisi sababu kazi iliyo mbele yake imetokana na hoja au azimio alilolipinga katika kikao cha maamuzi.
Dkt Slaa akajiuzulu, kalinda heshima yake, kwa kujiuzulu kwake akajitoa katika kundi la wanafiki, na kwa kujiuzulu kwake akawa huru na kuendelea na shughuli zake. Alipojiuzulu Dkt Slaa hakutuacha hivihivi, akatueleza sababu za kujiuzulu kwake na sababu hizo ndio tukajua mengi ya nyuma ya pazia hasahasa unafiki, urongo, na usaliti wa Mbowe kwa watanzania na WANACHADEMA.
Pili.
CHADEMA ya Mbowe wanasema Lowassa ni mtu safi kabisa, ila alichafuka sababu alikuwa anailinda Serikali, CCM na Rais. Kikubwa walisema kuwa Rais mstaafu ndiye mwenye dili za kifisadi ikiwemo na dili la Richmond. Watu tukihoji usafi wa Lowassa, jibu lilikuwa, "nenda mahakamani" au "shut up!"
Sawa sisi hatuna ushahidi, lakini kwanini CHADEMA hawaweki hadharani ushahidi waliopewa na Lowassa wenye kuthibitisha kuwa YEYE SIO FISADI? badala yake sisi tunao hoji tunaambiwa twende Mahakamani? Au Lowassa alipowaambia kuwa yeye msafi walimkubalia kirahisi bila ushahidi?
Fauka ya hayo, hivi viongozi wetu hawa wa CHADEMA walipokuwa wanatumia majukwaa kumuita Lowassa fisadi hawakujua kuwa kuna mahakama? Kama walijua, kwanini hawakwenda wao kipindi hicho? Au nao hawakuwa na ushahidi?
Sisi kama wanachi wa kawaida, hatuna ushahidi wa ufisadi wa Lowassa, na tulikuwa hatujui kuwa Lowassa fisadi, ila CHADEMA kwa kushirikiana na gazeti la MWANAHALISI ndio walio tuambia kuwa Lowassa fisadi.
Kama ni kwenda mahakamani, CHADEMA na Mwanahalisi itupe kwanza ushahidi walio kuwa wanautumia kumuita Lowassa fisadi. La kama si fisadi, watupe ushahidi wa kumsafisha ufisadi wake, kinyume na hivyo wajue ni nyumbu pekee ndio watakao kubali KUDANGANYWA kuwa Lowassa ni msafi.
Tatu
Huenda kweli Slaa kanunuliwa na CCM, siwezi kulisemea hili, lakini pamoja na kununuliwa kwake, hoja zake alizo zisema katika press yake ya kwanza baada ya kujiuzulu hazikuwa hoja za kitoto hata kidogo kiasi tuwatilie shaka wale wanao sema kuwa Wilbroad Slaa kanunuliwa.
Sababu mtu ananunuliwa ili abadili msimamo au alegeze msimamo au awe na msimamo wa kinafiki.
Msimamo wa Slaa juu Lowassa uko palepale, ya kwamba Lowassa ni fisadi na amelitia hasara taifa hili. Lakini Mbowe na Tundu Lissu wamebadili msimamo wao dhidi ya Lowassa. Wamabadilika kwa kuumbatia ufisadi, na kitendo chao hicho wamekipa jina la "kubadili gia angani". Yaani Mavi unayaita pilau ili upate uhalali wa kuyala, hakika huu ni wazimu.
Nawakukumbusha, wakati Slaa yuko CCM wachungaji na wanafunzi wa UDOM walikwenda kwake kumuomba au kumshawishi achukue fomu ya kugombea urais kupitia CCM, huku kwenye mtandao vijana wa CHADEMA walisema Lowassa kawanunua wale wachungaji na wanachuo.
Hoja yao ilikuwa, kwa akili ya kawaida na ya kisomi na ya kichungaji, huwezi kwenda kumshawashi mtu mwenye tuhuma za UFISADI na WIZI kuwa rais wa nchi, akili ya kuhongwa ndio hufanya hivyo. VIONGOZI WACHADEMA wakiongozwa na Mbowe pia walikemea na kusema kuwa Lowassa anatumia fedha kusaka urais. Alipochukua Fomu Lowassa ya CCM, waliendelea kusema kuwa FISADI KAPEWA FOMU YA KUWANIA URAIS, kumbukumbu za video na maandiko mbalimbali juu maneno haya kwa Lowassa zipo katika mitandao.
CCM kwa mara ya kwanza katika historia ya vyama vingi, ikaweza kusimamia misingi na utamaduni wake bila kuingiliwa na nguvu ya fedha, IKAMKATA MTUMIA FEDHA kwa maslahi ya chama chao na taifa.
Mbowe na wajumbe wengi wa CC wakabadili msimamo wao juu ya Lowassa bila sababu za msingi, hata ushauri wa Dkt Slaa wa kumtaka Lowassa atoke katika vyombo vya habari aeleze usafi wake kwa ushahidi wa nyaraka na vimemo haukusikilizwa bali ulipuuzwa.
Sasa, nani KAHONGWA kati ya walio badili msimamo bila sababu za msingi, na yule ambaye hajabadili huku akiwa na sababu za msingi za kutobadili?
Ndio maana tunasema, kama vile Lowassa alivyokuwa anawanunua wachungaji, wenyebodaboda, wanavyuo, wajumbe wa NEC wa CCM, na ndio hivyohivyo alivyo wanunua Mbowe, Lissu, Msigwa, Lema na CHADEMA yote kwa ujumla. Sababu ni fedha tu ndio hufanya akili ya mtu timamu isifanye kazi sawasawa, ni fedha tu ndio humfanya mwenye macho mawili awe kipofu mbele ya ovu lililo mbele yake. Wenzetu hawa wamenunuliwa wenzetu hawa wametumiwa na Lowassa, lakini sifa zirudi kwa Mungu maana wameshindwa.
Nne.
Wanasema Dkt Slaa alichukia na mwishowe kaamua kujiuzulu sababu CHADEMA na UKAWA iliamua kumfanya Lowassa kuwa mgombea urais badala ya Dkt Slaa. Hii hoja dhaifu sana.
Mtiririko mzima wa matukio ya Lowassa kutoka CCM na kujiunga CHADEMA uliratibiwa Dkt Slaa na aliweka vigezo ambavyo Lowassa kama angevitimiza viongozi wa CHADEMA na CHADEMA yenyewe ingekuwa sehemu salama. Muda wote wakati Dkt Slaa anaratibu ujio wa Lowassa alikuwa anajua fika kuwa Lowassa anakuja kugombea urais na si kuja kuwa mwanachama tu.
Dkt Slaa ndio kiongozi kwanza wa CHADEMA kufuatwa na Gwajima kuelezwa nia ya Lowassa Kijiunga CHADEMA na kugombea urais. Dkt Slaa Akamkutanisha Gwajima na Mbowe, na katika mazungumzo yao ndio Dkt Slaa akaweka vigezo ambavyo Lowassa alitakiwa kuvitimiza na hatimaye suala hilo likatua kamati kuu, na huku Slaa akisisitiza vigezo alivyo viweka.
Kwahivyo si uroho wa urais ulio mfanya Dkt Slaa amkatae Lowassa na kujiuzulu, bali vigezo alivyo viweka Lowassa hakuvitimiza. Kamati Kuu pia iliamua kupuuza vigezo alivyo viweka Slaa pamoja na kwamba kabla ya KAMATI KUU Mbowe na Slaa walikubaliana juu ya vigezo hivyo.
Vigezo ambavyo Lowassa ameshindwa kuvitimiza ni viwili.
Moja kwenda katika vyombo vya habari na kumtaja muhusika wa Richmond kwa kutumia nyaraka na vimemo, na pia kutaja maovu ya serikali na CCM ambayo yeye kwa nafasi yake kama waziri mkuu na mjumbe wa kamati kuu ya CCM alikuwa anaujua. Ni ajabu hadi leo hii Lowassa hajailipua serikali ya CCM na wala hajamtaja muhusika wa Richmond hata kwa maneno matupu tu zaidi ya kusema "mama lishe rafiki zangu."
Pili Lowassa alitakiwa ataje majina ya vigogo ambao ataingia nao CHADEMA, na hao watu awe nao siku ya press na wajiunge na CHADEMA siku moja ambayo Lowassa atajiunga. Lowassa hakuwataja hao watu.
Ina maana kama Lowassa angetimiza haya Slaa angekuwa bado yuko CHADEMA, na kama CHADEMA ingemkataa Lowassa baada ya kushindwa kutimiza haya, basi Slaa bado angekiwa yupo CHADEMA. Kitu gani kilichomfanya Mbowe amkubali Lowassa pamoja na kwamba hakutimiza vigezo? Uzalendo au Rushwa?
MWISHO.
Hebu tujiulize Hivi Mnyika wa zaman ndio wasasa? itachukua muda sana kwa Mnyika kurudi katika hali ya kawaida ndani ya siasa za CHADEMA, sababu chama alicho kiamini kilipotoka na yeye na Slaa hawakuwa na sauti kuzidi fedha za Lowassa.
Ndio maana wengi tulitaraji mrithi wa Slaa Angekuwa Mnyika, lakini msimamo wa Mnyika dhidi ya ujio wa Lowassa ndio umemgharimu hata asiwe kiongozi ndani ya CHADEMA.
Kupotoka kwa CHADEMA kulikosabishwa na nguvu ya fedha za Lowassa, Yericko Nyerere, Malisa, Ben Saane na vijana wengi wanao kipigania chama hicho katika mtandao wanakujua vizuri, ila kwa upofu walojitia hata mambo yalo dhahiri kumpelekea wapate lakabu mpya, si makamanda tena, bali nyumbu wanao jiendea bila kushughulisha akili.
Heri CHADEMA/UKAWA ingeshindwa uchaguzi huku ikiwa na mgombea msafi na sahihi, kuliko ilivyoshindwa uchaguzi kwa kuwa na mgombea mchafu kiasi waone haya kuzungumzia ufisadi.
Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/Whatspp 0622845394 Morogoro.