MBOWE: Tumeshajipa kibali cha kutangulia mbele za haki

MBOWE: Tumeshajipa kibali cha kutangulia mbele za haki

Black Africans, still have a very long way to go! Sasa, issue ni maendeleo au siasa? Binafsi Naamini, shughuli za maendeleo zinazoendelea kutekelezwa Nchini ni Mipango ya Serikali yetu tena inasemekana mingine ipo tangu enzi za mzee wetu Nyerere. Si mtu fulani. Rais Magufuli ni msimamizi mkuu tu. Mipango ni mizuri na endelevu. Tuiunge mkono Serikali yetu kwa akili zetu zote na kwa nguvu zetu zote na uwezo wetu wote. Hizi siasa za uchochezi zinatoka wapi jamani? Sisi huku vijijini mbona tunaona Serikali inatekeleza wajibu ukilinganisha na awamu za Tawala zilizopita? Huduma za afya zinaboreshwa, karibu kila sehemu Nchi hii inafikika, elimu, nk. Tatizo ni nini wajameni? Rais Magufuli anayekejeliwa, ametenda lipi baya maskini? Mjue, mnatuvuruga wenzenu wa vijijini eti! Hotuba hii ya mhe. Mbowe unaonesha wazi kuwahamasisha wasikilizaji kuipinga Serikali yao kwa udi na uvumba, hata ikibidi kufa! Kweli wajameni? Kwa lipi! Ninyi "mangi" acheni hizo. Vita na machafuko ya kisiasa hususani ktk Nchi maskini kama hizi, Isikie kwa wengine huko DRC, South Sudan, Syria, nk. Unamfananisha mcha Mungu mtumishi wa Bwana Yesu kristo Rais Magufuli na wale waasherati wezi na mafisadi wa Afrika kusini na Zimbabwe?! Hapo ndiyo nimechefuka moyo. Ushauri wangu CDM achaneni na nia yenu ovu. Mkianza kutekeleza uovu wenu mjue hatutowaunga mkono. Mtakuwa peke yenu. Tuungane kuijenga Tanzania mpya yenye uchumi wa kati. Bwana Yesu kristo ibariki Tanzania!
Wewe ni mnufaika wa misukule inayolishwa na kunyweshwa! Akina Bashite wanayo haki ya kuiba, kukwapua na kufanya lolote!! Wewe ni mmoja wao!
 
Nenda ulaya utakuta askari hao.
Wanarushiwa mawe na hawarudushi kwa mibomu au risas lkn ninyi ndio mnajua sheria ya self defence hats NTU yupo 2 miles bila slaha

Ulaya ipi? Hiyo Ulaya polisi wake wana washoot wanaowahisi tu?

Toa mfano specific wa tukio la polisi wakarushiwa mpaka mawe na hawakurusha risasi.

Mambo siku hizi rahisi sana, kumbukumbu ya matukio yote yapo. Uongo haujengi.
 
hii speech ya Mbowe inauzito mithili ya speech ya martin lutherking
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe amewaambia Polisi kuwa wao tayari wameshajipa kibali cha kutangulia mbele za haki. Mbowe aliyasema hayo wakati akihutubia wananchi katika ufungaji wa kampeni Jimbo la Kinondoni.




Source: Muungwana Blog​

CALCULATED MOVES, THAT I GIVE YOU COMRADE MBOWE!
 
Mkuu huw unaangalia movies za vita? Sterling anasimama tu? Ukinipa jibu ndo nitakujibu vizuri swali lako.
Usilinginishe sinema na vitu halisi.Mbowe alisema kaweka rehani roho aliposikia mlipuko wa bunduki tu katimua mbio.Sikujua kama mbowe ana mbio kiasi kile,Chama cha riadha kuna watu hawavumi kwa mbio lakini wapo.Naomba mumusajili kwenye mbio mbowe aweza tusaidia hata kupata medali ya jiwe
 
Atakayesikiliza hii kauli atakua ameamua kuisaliti nafsi yake.

Huu mwaka wa 20 sasa huwa anasema hivyo ; Hakuna linalomkuta yeye; yanawakuta wengine tu kwa uzembe wao.

Uliza kilichomkuta Dr. Slaa hata baada ya kupata ulemavu wa mkono kukipigania chama; akaishia kuitwa msaliti.
Usaliti wake umekuwa verified kwa kupewa cheo ccm
 
Katika maisha lazima vitu viwili viwepo kuna ujinga na ujanja ili maisha yaendelee
 
Kwani Julius aliposema tutampiga Idd Amin ulimwona alitangulia mbele. Acheni ujinga.
Unajua Kambarage alipoteza watoto wangapi kwenye ile vita?

Mwenzenu watoto wake wapo US wanafanya elementary studies. Karagabao.
 
kwa mbio alizotimua mbowe aliposikia milio ya bunduki anastahili kupewa tuzo la mwasiasa mwenye mbio sana wa mwaka 2018.Hiyo tuzo yaweza kuwa hata ya jiwe LILILOOKOTWA pale alipoanzia mbio
 
Kiukweli chadema inawajambisha ccm, mbinu za kuiua chadema zimefeli kabisa
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe amewaambia Polisi kuwa wao tayari wameshajipa kibali cha kutangulia mbele za haki. Mbowe aliyasema hayo wakati akihutubia wananchi katika ufungaji wa kampeni Jimbo la Kinondoni.




Source: Muungwana Blog​

Mbona anakimbia na kufa wasio na hatia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom