Muwe mnatafakari wakati mwingine. Polisi walifanya kosa kubwa kufyatua risasi za moto. Nje ya unyang'au unaoendelea tanzania, polisi hawatakiwi kutumia silaha za moto hovyo, hata kama ni katika mapambano na majambazi wanapaswa kutumia silaha bila kudhamiria kuua.
Polisi wanapofyatulia risasi wananchi raia wasiokuwa na hatia wanakuwa wamevuka mipaka. Mbowe anapowaambia polisi kuwa wananchi watakomalia haki yao, haikutegemewa polisi wakimbilie kuua wananchi.
Mbele ya vyombo vya dola vinavyotumia silaha za moto kuua, wananchi wanakuwa hawana namna ila kukimbia. Mifano ipo mingi katika historia, hitler, apartheid, stalin, mao n.k.
Sasa mmeuwa mtoto aliyekuwa na matumaini ya maisha. Kasoma mpaka amebahatika kuingia chuo kikuu kizuri cha udsm. Tegemeo la wazazi na ndugu zake. Hana hatia. Mmenda mkamuua bila sababu.